saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,250
- 6,218
Mohamed Mchengerwa unaaminika ni waziri mchapakazi, tumekuandikia mara nyingi humu kwamba kuna ubaguzi kwenye Halmashauri zetu, mm nimetoa mfano wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, hakuna mabadiliko yoyote mpaka sahivi, baadhi wamelipwa na wengine hawajalipwa. Wakati huo viongozi wanajigamba kuwa hakuna wa kuwafanya chochote, eti wamepeleka request BOT na hawahusiki tena na malipo yetu. Tumwamini nani, BOT wanatumia vigezo gani ktk kulipa? Kwanini walipwe baadhi na wengine waachwe? Hii ndio nchi ya mwl. Nyerere kweli? Iliyojaa ubaguzi wa namna hii? Mh. Waziri jitokeze acha kibri kisa mkwe wa mh. Rais wetu. Utamharibia mama yetu badala ya kumsaidia. Tuambie kwanini hatujalipwa mpaka sahivi? Sisi hatujui mambo ya BOT tunataka malipo yetu. Kwanini huu ubaguzi? Kwamba hatuna wakubwa tunaowafahamu? Binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu msitupuuze.