Mh. Mohamed Mchengerwa utaweza kuvaa viatu vya Ummy TAMISEMI? TAMISEMI ni ngumu, walimu hawajalipwa pesa za likizo za mwaka jana.

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,173
6,157
Mohamed Mchengerwa unaaminika ni waziri mchapakazi, tumekuandikia mara nyingi humu kwamba kuna ubaguzi kwenye Halmashauri zetu, mm nimetoa mfano wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, hakuna mabadiliko yoyote mpaka sahivi, baadhi wamelipwa na wengine hawajalipwa. Wakati huo viongozi wanajigamba kuwa hakuna wa kuwafanya chochote, eti wamepeleka request BOT na hawahusiki tena na malipo yetu. Tumwamini nani, BOT wanatumia vigezo gani ktk kulipa? Kwanini walipwe baadhi na wengine waachwe? Hii ndio nchi ya mwl. Nyerere kweli? Iliyojaa ubaguzi wa namna hii? Mh. Waziri jitokeze acha kibri kisa mkwe wa mh. Rais wetu. Utamharibia mama yetu badala ya kumsaidia. Tuambie kwanini hatujalipwa mpaka sahivi? Sisi hatujui mambo ya BOT tunataka malipo yetu. Kwanini huu ubaguzi? Kwamba hatuna wakubwa tunaowafahamu? Binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu msitupuuze.
 
Bila kuathiri mada yako ni vema ujue yafuatayo
1. Naamini unajua sio kila likizo ina malipo, mtaenda wote likizo lakini watakaolipwa ni waliopangwa kulipwa kwa wakati huo.

2.Malipo ya fedha za Likizo hutegemea uwepo wa fedha. Kuna wakati fedha huletwa pungufu na Serikali na hivyo hulipwa kwa awamu. Zinaweza kuchelewa kufika lakini huingizwa kwenye arrears na kulipwa baadae.

3. Sina uhakika, lakini kuna uhaba wa fedha za kulipa matumizi ya kawaida kwa taasisi za umma. Hata taasisi niliyopo mimi kuna shida hiyo hiyo. Malipo yanakaa mwezi mzima bila Hazina kulipa. Yaani wahasibu wanalipa kwa wakati lakini Hazina (BOT) hawalipi kwa wakati. Hivyo, wahasibu wenu wako sahihi. Na kama hili ndio tatizo, kumlaum Waziri hakutasaidia kitu.

4. Naomba ufafanue vizuri hoja ili wengine wakushauri vizuri

4. Kitu pekee unachoweza kuilaum Serikali ni kama hujalipwa Mshahara wako. Haya mengine ni benefit tuu na sio rights, hivyo usipolipwa kwa wka
 
Back
Top Bottom