Joseph Matiko Matare
Member
- Oct 14, 2019
- 19
- 16
MH.MAGUFULI KATIKA VIATU VYA NYERERE.
Katika Makala yangu ya “Rais Magufuli na Goriathi wa Tanzania” katika Gazeti la “Nipashe” na kwenye mitandao ya “Jamii Forum” na Facebook” Nilieleza namna ambavyo mheshimiwa Magufuli alivyoingia Ikilu, Upinzani aliokutana nao na angefanya nini kwa Tanzania.Bahati nzuri yale yote niliyoyaeleza ametimiza na amefanya hivyo. Mungu ambariki sana.
Leo hii katika kukumbuka ya kifo cha Baba wa taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere tarehe 14 Oktoba 2019, ningependa tuangalie uhusiano wake na mheshimiwa Rais John Magufuli katika uwanda wa siasa za Tanzania. Naomba tusome kisa hiki kinachoonesha mazungumzo kati ya Nyerere na Magufuli kabla ya kuingia Ikulu ya Tanzania. Jukumu la kuamua kama mazungumzo haya ni ya kweli au ya kubuni ni lako msomaji. Sikiliza kwa makini halafu uamue kwa ajili ya hatima ya Tanzania.
JULIUS K. NYERERE: Mwanangu John Magufuli!
Leo hii nimekuita niongee na wewe mambo Fulani kuhusu familia yangu ya watanzania na mji wangu wa Ikulu ya Tanzania. Ninataka uwe msimamizi wa mirathi yangu kwa niaba ya watanzania wote kwa kipindi hiki cha awamu ya tano katika uongozi wa nchi yetu. Katika kusimamia mirathi hii naomba uvae viatu vyangu na uvitembelee siku zote. Kaka zako Mwinyi, Mkapa na Kikwete walijaribu kuvivaa lakini havikuwatosha viliwalegea na hivyo vikachomoka wakati wanatembea. Kabla viatu havijachomoka walijitahidi kulinda uhuru wetu, amani yetu,undugu wetu, umoja wetu, muungano wetu, kuepuka ukabila, udini na ubaguzi wa jinsia na pia kuwa na mahusiano mema na mataifa jirani zetu. Lakini viatu vilipolegea wakavivua waliogopa kutembea kwenye miiba ya kujenga uchumi unaojitegemea, miiba ya rushwa na ufisadi, miiba ya kuhamia Dodoma, miiba ya kutoa huduma kwa wananchi, miiba ya kuunda vyombo vya dola vyenye nidhamu na kuaminika, miiba ya kujenga miundo mbinu imara kwa ajili ya kuingia kwenye karne ya viwanda, miiba ya kuzuia ubinafsishaji holela, miiba ya ukosefu wa ajira na miiba ya kujenga elimu ya kujitegemea na kuzuia wimbi la madawa ya kulevya.
Najua wewe ni mtoto wangu wa mwisho niliyekuzaa kisiasa na kimalezi watakaofuata baadaye watakuwa wajukuu wangu ambao wengine wameniona tu na wengine wanasikia tu. Sasa mwanangu uko tayari kuvaa viatu vyangu muda wote na kukanyaga juu ya miiba ya hayo niliyokueleza? Je unanihakikishia vipi kwamba utaweza kufanya mambo hayo ambayo kaka zako waliotangulia wameshindwa kuyafikia? Na ukumbuke kwamba utakayoniahidi hapo uende mbele ya watanzania wote uziseme ahadi hizo ili baadaye ndio zitumike kukuhukumu kama hutafanya.
JOHN P. MAGUFULI: Baba, Samahani naomba niongee na mtu mmoja hapa kwanza ni rafiki yangu anisaidie wazo Fulani halafu nianze kukueleza(Nyerere anakubali) Halo! Kasimu Majaliwa! Naam John Magufuli lete habari! Baba Nyerere ameniita ameniambia nivae viatu vyake anikabidhi usimamizi wa mirathi yake ya uongozi wa awamu ya tano. Nataka unisaidie kuunda serikali itakayotembelea viatu vya Nyerere. Sharti la kunisaidia ni kwamba hatutaenda Ikulu kuchumbia na kwa hiyo hatutakuwa na mama mkwe, baba mkwe,shemeji, kaka,dada,mama, baba, shangazi wala mjomba huko katika utekelezaji wa majukumu yetu ya serikali. Je, uko tayari kukabiliana na hayo rafiki yangu? Na kwamba katika majukumu hayo hutakuwa rafiki tena bali mahusiano yetu ni mimi Rais na wewe Waziri mkuu ambaye nina mamlaka yote juu yako?
KASSIM MAJALIWA: Hapo tutaweza ndugu yangu, maana tatizo la nchi hii limekuwa kulindana. Nimekuwa humu TAMISEMI nimeyaona mengi. Nakubali kukusaidia kwa moyo wangu wote, roho yangu yote, akili zangu zote na nguvu zangu zote kuiletea nchi yetu maendeleo kwa wote. Ninaahidi nisipofanya hivyo usinifumbie macho wala usipoteze muda niondoe tu.
JOHN P. MAGUFULI: Sawa! Nitakapokanyaga na wewe kanyaga hapo hapo tutafika. Mbona tunaweza kubadili sura ya nchi hii? Baba,(Magufuli anamrudia Nyerere)nimekubali kwa moyo wote,akili yote,roho yote na nguvu zote kwa kuvaa viatu vyako siku zote.Ila naomba uniruhusu nisivivae hivyo hivyo vitakapoonekna kulegea nivikaze visichomoke(Nyerere anakubali).Sasa baba nitakuonyesha nitakavyovivaa hapa hapa.Nachukua kimoja kimoja.
KIATU 1.KUKANYAGA UCHUMI TEGEMEZI.
Baba,tunazo rasilimali nyingi sana ambazo mungu ametukirimia na nchi yetu ni tajiri ila sisi ni maskini kwa sababu tumeruhusu uchumi wetu kuchezewa na mataifa makubwa na tumekosa usimamizi mzuri wa rasilimali zetu na nitahakikisha kuwa:
KIATU 2:KUKANYAGA RUSHWA NA UFISADI.
Baba,nitafuata ahadi yako ya mwana- TANU na baadaye CCM kuwa”Rushwa ni adui wa haki sitapokea wala kutoa Rushwa”.Wala rushwa na mafisadi watashughulikiwa kwa nguvu zote tena hadharani mbele ya wananchi wote wawajue.Nimeongea na Kassimu Majaliwa anisaidie yeye alikuwa kule TAMISEMI anaelewa vizuri mianya huko kwenye halmashauri zetu na amekubali.Tumekubaliana hatuendi Ikulu kuchumbia hivyo hakutakuwepo mtu wa kufumbia macho.
KIATU 3:KUKANYAGA KWENDA MAKAO MAKUU DODOMA.
Baba,Dodoma imechukua muda mrefu tangu 1973 kwa sababu viongozi hawakuwa na dhamira ya kweli ya kuhamia Dodoma kwa sababu ya miradi yao Dar es salaam na kuona Dodoma kama eneo kavu sana.Ninakuahidi ndani ya miaka mitano ya mwanzo tutahamia Dodoma.Nitaanza na kupeleka serikali pale na hasa wizara.Kiongozi yeyote atakayesita kuhamia Dodoma tutaachania Da es salaam yeye anarudi kwao mimi ninakwenda Dodama.
KIATU 4.KUKANYAGA UZEMBE WA KUTOHUDUMIA WANANCHI.
Baba,kuhusu huduma kwa jamii nitahakikisha kuwa kila mtumishi wa serikali anatoa huduma kwa jamii na kuwaondolea wananchi kero zilizop.Hilo litafanyika kwa kuweka nidhamu kazini kwa watumishi wa umma.Kila mtumishi wa umma lazima ajue ofisi aliyonayo na mshahara anaopata ni kodi ya wananchi ili awahudumie.Kwangu mimi mwananchi atakuwa ndiye BOSI.Uzembe wowote utashughulikiwa hapo hapo bila kupoteza muda.
KIATU 5:VYOMBO VYA DOLA.
Baba,swala la vyombo vya dola vitaimarishwa kwa kupewa vitendea kazi vya kisasa ili kuendana na sayansi na teknolojia ya sasa.
Kwa upande wa polisi tutahakikisha kwamba hakuna malalamiko ya rushwa,uonevu na kubambikiwa kesi.Tutawapa mamlaka zaidi ili kuondoa aibu hii ya kusikia vituo vya polisi vinavamiwa na majambazi na wakati mwingine eti wananchi wenye hasira kali.Lazima sasa atakayevamia kituo cha polisi aage kabisa ndugu zake kwamba watakutana mbinguni.
KIATU 6:KUJENGA MIUNDO MBINU.
Baba,tutawekeza katika miundo mbinu ya barabara,reli,ndege na meli na kuhakikisha kwamba usafiri upo muda wote kwenda na kurudi nchi jirani ili kuwa na biashara katika nchi zetu na. pia kuhakikisha mikoa yote imeunganishwa na barabara za lami zinazopitika muda wote wa mwaka ili kuingia uchumi wa viwanda
KIATU 7:KUKANYAGA UBINAFSISHAJI HOLELA.
Baba,nimekuona unalia juu ya ubinafsishaji holela holela.Mfano wa benki ya NBC na ATC.Nakuahidi ndani tu ya mwaka wa kwanza tutakuwa na ndege zetu wenyewe za ATC ili kushindana na sekta binafsi.Pia mabenki yote yatadhibitiwa na Benki kuu ya Tanzania (BOT).
KIATU 8:KUKANYAGA TATIZO LA AJIRA.
Baba,wakati wako tatizo la ajira halikuwepo kwa sababu watu walikuwa wachache,shule zilikuwa chache,na vyuo vikuu vilikuwa viwili tu Dar es salaam na Sokoine University na ulisisitiza elmu ya kujitegemea ambayo ilimfanya mtu aweze kumudu mazingira ya kujiajiri mwenyewe anapomaliza darasa la saba au vyuo vya ufundi.Leo hii watanzania ni wengi,shule ni nyingi,vyuo vya kawaida ni vingi na vyuo vikuu vimetapakaa kila mahali hivyo tatizo la ajira za serikali litaendelea kuwepo.Ila mimi nitalishughulikia kwa:
KIATU 9:ELIMU YA KUJITEGEMEA.
Baba,hata mimi nakubali nilisoma elimu ya kujitegemea na ilikidhi haja ya wahitimu wake.Leo hii utakuta mhitimu wa Mechanical Engineering hata injini ya gari lake ikipata hitilafu anampelekea mtu wa darasa la saba aliyehitimu Veta.Katika serikali yangu nitafanya yafuatayo:
JULIUS.K.NYERERE:Asante mwanangu kwa kukubali nimeona hutavua viatu.Usiogope chochote.Usiogipe auaye mwili bali ogopa tu Yule awezaye kuua mwili na Roho ambaye ni Mungu.Kumbuka neno la Mungu linasema watu wengine matendo yao huwatangulia mbinguni na wengine matendo yao huwafuata.Jitahidi matendo yako yatangulie maana ilipo hazina yako ndipo roho yako itakuwepo huko Mbinguni.
Sasa ndugu zangu watanzania mheshimiwa Magufuli ametimiza ahadi zake? Kuna wale wanaosema mheshimiwa Magufuli hajafanya chochote. Wengine wanasema hajakamilisha yale aliyoyaahidi. Wengine wanadai ni mkali mno watu wanamuogopa naomba tuangalie ukweli huu
Tunapokumbuka Nyerere lazima tumtazame si katika mauti yake bali katika uhai wake ndani ya mheshimiwa Magufuli. Maana hayo mazuri aliyofanya Nyerere na ambayo hakufanya sasa yanaishi tena ndani ya Magufuli. Ni unafiki kumuenzi Nyerere wakati unampiga Yule anayetimiza aliyoyataka Nyerere.Hii ina maana tunamuenzi Nyerere si kwa sura yake ya tabasamu bali kwa matendo yake ambayo yanaishi ndani ya Magufuli. MAGUFULI OYEEEEEEE!!!!! KANYAGA ACCELERATOR TWENDE BABA !!
JOSEPH.M. MATARE (SONGEA)
Mobile:0757282151
Jmmatare@yahoo.com/mmgwesso@gmail.com

- Ninadhibiti uporaji wa rasilimali zetu na wageni kwa kuwa na sera zenye manufaa kwa nchi yetu.
- Kudhibiti mianya ya rushwa na ufisadi kwa kufunga mianya yote inayotumika kuiba rasilimali zetu na kuanzisha mahakama za mafisadi na rushwa kubwa.
- Kusimamia makusanyo ya kodi ili kila mtanzania ashiriki kuchangia uchumi wetu kwa pamoja na kuwa na fedha zetu za ndani.
- Tutafanya biashara na mataifa yale yatakayotambua uchumi wetu na kuuheshimu na wale wenye nia njema na Tanzania.
- Kuthibitisha kwamba tunaweza, katika awamu ya kwanza ya uongozi wangu tutajenga miradi mingi kwa mapato yetu ya ndani.
KIATU 2:KUKANYAGA RUSHWA NA UFISADI.
Baba,nitafuata ahadi yako ya mwana- TANU na baadaye CCM kuwa”Rushwa ni adui wa haki sitapokea wala kutoa Rushwa”.Wala rushwa na mafisadi watashughulikiwa kwa nguvu zote tena hadharani mbele ya wananchi wote wawajue.Nimeongea na Kassimu Majaliwa anisaidie yeye alikuwa kule TAMISEMI anaelewa vizuri mianya huko kwenye halmashauri zetu na amekubali.Tumekubaliana hatuendi Ikulu kuchumbia hivyo hakutakuwepo mtu wa kufumbia macho.
KIATU 3:KUKANYAGA KWENDA MAKAO MAKUU DODOMA.
Baba,Dodoma imechukua muda mrefu tangu 1973 kwa sababu viongozi hawakuwa na dhamira ya kweli ya kuhamia Dodoma kwa sababu ya miradi yao Dar es salaam na kuona Dodoma kama eneo kavu sana.Ninakuahidi ndani ya miaka mitano ya mwanzo tutahamia Dodoma.Nitaanza na kupeleka serikali pale na hasa wizara.Kiongozi yeyote atakayesita kuhamia Dodoma tutaachania Da es salaam yeye anarudi kwao mimi ninakwenda Dodama.
KIATU 4.KUKANYAGA UZEMBE WA KUTOHUDUMIA WANANCHI.
Baba,kuhusu huduma kwa jamii nitahakikisha kuwa kila mtumishi wa serikali anatoa huduma kwa jamii na kuwaondolea wananchi kero zilizop.Hilo litafanyika kwa kuweka nidhamu kazini kwa watumishi wa umma.Kila mtumishi wa umma lazima ajue ofisi aliyonayo na mshahara anaopata ni kodi ya wananchi ili awahudumie.Kwangu mimi mwananchi atakuwa ndiye BOSI.Uzembe wowote utashughulikiwa hapo hapo bila kupoteza muda.
KIATU 5:VYOMBO VYA DOLA.
Baba,swala la vyombo vya dola vitaimarishwa kwa kupewa vitendea kazi vya kisasa ili kuendana na sayansi na teknolojia ya sasa.
Kwa upande wa polisi tutahakikisha kwamba hakuna malalamiko ya rushwa,uonevu na kubambikiwa kesi.Tutawapa mamlaka zaidi ili kuondoa aibu hii ya kusikia vituo vya polisi vinavamiwa na majambazi na wakati mwingine eti wananchi wenye hasira kali.Lazima sasa atakayevamia kituo cha polisi aage kabisa ndugu zake kwamba watakutana mbinguni.
KIATU 6:KUJENGA MIUNDO MBINU.
Baba,tutawekeza katika miundo mbinu ya barabara,reli,ndege na meli na kuhakikisha kwamba usafiri upo muda wote kwenda na kurudi nchi jirani ili kuwa na biashara katika nchi zetu na. pia kuhakikisha mikoa yote imeunganishwa na barabara za lami zinazopitika muda wote wa mwaka ili kuingia uchumi wa viwanda
KIATU 7:KUKANYAGA UBINAFSISHAJI HOLELA.
Baba,nimekuona unalia juu ya ubinafsishaji holela holela.Mfano wa benki ya NBC na ATC.Nakuahidi ndani tu ya mwaka wa kwanza tutakuwa na ndege zetu wenyewe za ATC ili kushindana na sekta binafsi.Pia mabenki yote yatadhibitiwa na Benki kuu ya Tanzania (BOT).
KIATU 8:KUKANYAGA TATIZO LA AJIRA.
Baba,wakati wako tatizo la ajira halikuwepo kwa sababu watu walikuwa wachache,shule zilikuwa chache,na vyuo vikuu vilikuwa viwili tu Dar es salaam na Sokoine University na ulisisitiza elmu ya kujitegemea ambayo ilimfanya mtu aweze kumudu mazingira ya kujiajiri mwenyewe anapomaliza darasa la saba au vyuo vya ufundi.Leo hii watanzania ni wengi,shule ni nyingi,vyuo vya kawaida ni vingi na vyuo vikuu vimetapakaa kila mahali hivyo tatizo la ajira za serikali litaendelea kuwepo.Ila mimi nitalishughulikia kwa:
- Kujenga uchumi wa viwanda vya serikali na vya watu binafsi vinavyoweza kutoa ajira kwa vijana wetu.
- Kutoa fedha kwa ajili ya watu watakaojiunga katika vikundi vya SACCOS ili wapate mtaji wa kuanzisha miradi itakayowawezesha vijana kujiajiri.
- Kuboresha kilimo kwa kufanya kilimo kuwa cha kisasa kwa kutoa pembejeo za kilimo.Kwa kufanya hivyo vijana wetu watavutiwa kuwa na miradi ya kilimo,uvuvi na ufugaji na kuacha kuona kilimo kama adhabu waliyopewa Adamu na Hawa.
- Kubadili mfumo wa elimu kutoka elimu ya nadharia kuwa ya vitendo zaidi.Na hapa msisitizo utakuwa juu ya masomo ya sayansi na baadaye kujifunza ufundi wa aina mbalimbali utakaowezesha ajira binafsi.
KIATU 9:ELIMU YA KUJITEGEMEA.
Baba,hata mimi nakubali nilisoma elimu ya kujitegemea na ilikidhi haja ya wahitimu wake.Leo hii utakuta mhitimu wa Mechanical Engineering hata injini ya gari lake ikipata hitilafu anampelekea mtu wa darasa la saba aliyehitimu Veta.Katika serikali yangu nitafanya yafuatayo:
- Tatizo la wanafunzi kukosa madawati linaondolewa kabisa.
- Elimu Msingi(Basic Education)kuanzia darasa la kwanza hadi la kumi na mbili inatolewa kwa gharama za serikali ili kila mtoto wa Tanzania apate fursa ya kwenda shule bila kujali kipato.
- Walimu wanapatikana katika shule zote za serikali kuanzia msingi hadi vyuo vya kawaida(Tertiary Colleges).
- Masomo ya sayansi yanahimizwa na kuwekewa motisha kwa kutoa mikopo kamili (100%) kwa wale watakaosoma masomo ya sayansi elimu ya juu.
- Kuiweka elimu yetu iwe ya vitendo zaidi ili watu waweze kuitumia kumudu maisha yao kwa kujiajiri.
JULIUS.K.NYERERE:Asante mwanangu kwa kukubali nimeona hutavua viatu.Usiogope chochote.Usiogipe auaye mwili bali ogopa tu Yule awezaye kuua mwili na Roho ambaye ni Mungu.Kumbuka neno la Mungu linasema watu wengine matendo yao huwatangulia mbinguni na wengine matendo yao huwafuata.Jitahidi matendo yako yatangulie maana ilipo hazina yako ndipo roho yako itakuwepo huko Mbinguni.
Sasa ndugu zangu watanzania mheshimiwa Magufuli ametimiza ahadi zake? Kuna wale wanaosema mheshimiwa Magufuli hajafanya chochote. Wengine wanasema hajakamilisha yale aliyoyaahidi. Wengine wanadai ni mkali mno watu wanamuogopa naomba tuangalie ukweli huu
- Hoja ya kwamba hajafanya chochote kwani alichofanya kinaonekana hata kipofu ameona.
- Wanadai kwamba hajakamilisha ahadi zake nyingine. Wanaweza kueleza umma wa mtanzania kwamba aliwahi kumaliza shida zao tarehe ngapi? Muda wake bado unaendelea na si lazima iwe ndani ya miaka mitano ya mwanzo.
- Tukumbuke kwamba hatuzungumzii Magufuli kama mtu bali kama taasisi na taasisi ina mambo mengi na ina watu wengine wanaofanya kazi humo na wengine wanaweza kuwa hawataki na ushahidi unaonekana kwa wale wanaotumbuliwa. Hawa wanaweza kuchelewesha malengo yasitimie na wengine wamo ambao hawajatumbuliwa. Wanaodai Nyerere alikuwa ni mpole sana kiasi kwamba hakuogopwa na watu. Hivi? Haya yaliyokuwa yameshindikana yangefanyika kwa kuchekacheka na kugongeana tano za vidole?
- Kutokufikia lengo hakuna maana kuwa mtu ameshindwa bali ni kwamba mtu huyo hajafanikiwa bado.
- Kutofikia lengo hakuna maana kuwa mtu hajafanya chochote bali kwamba ana kitu cha kujifunza kwa nini hakufanikiwa.
- Kutofikia lengo hakuna maana mtu ni mjinga bali kwamba mtu huyo alikuwa na imani kubwa sana ya kufanya kuliko mazingira halisi.
- Kutofikia lengo hakuna maana mtu ameacha kufanya bali kuwa bado ana nia ya kujaribu tena kwa njia bora zaidi.
- Kutofikia lengo hakuna maana mtu ni dhaifu bali kuwa si mkamilifu kwa kila jambo.
- Kutofikia lengo hakuna maana kuwa mtu alipoteza wakati bali kuna maana aanze kitu kipya kingine.
- Kutofikia lengo hakuna maana kuwa mtu hatafanikiwa bali kuwa itachukua muda mrefu zaidi kukamilisha.
- Kutofikia lengo hakuna maana kuwa mtu hakuthubutu bali kwamba alikuwa anatafuta kipi kingefanyika, wakati gani, wapi, Kwa namna gani na nani angefanya.
- Kutofikia lengo hakuna maana mtu ameachwa na mungu bali kuwa mungu ana mpango mzuri kwake, amche yeye ili ampe maarifa ya kupambanua magumu asiyoyajua.(Yeremia 33:3)