Mh. Mbilinyi (Sugu) alipuka bungeni

Inawezekana ukawa bonge la mjinga kulko unavyofkiri,kwa mawazo yako uanadhani hata wapinzani wangekuwa na hoja gani nzuri hawateweza kubadili mawazo ya wendawazimu wengi ndani ya bunge kupitisha upuuz wao,jiulze hata wewe uliwahi kuskia wapi mtu akapanga bajet ya milioni moja wakati mkononi ana laki moja kama sio serkali ya ccm?

hivi huyu sindie mtuhumiwa wa hile kesi ya ugaidi pia au polisi wanabagua watu wakukamata kichama?
 
Hoja yake imesaidia vipi kuboresha bajeti ya Waziri Mkuu?

Bunge sio Rock Concert, mbunge akiongea akimaliza inabidi kuwe na input alizoweka. Ukiona mbunge kamaliza halafu kinachojadili ni kwamba "kamchana Mwigulu" ujue kuna walakini.

kuisema serikali kwa kukataa hoja za maana kama ya Mbatia kuhusu elimu na huku watoto wanafeli,hakuna input hapo?kuishauri serikali kusimamia hoja za maana na zenye maslahi kwetu wananchi na kuachana na ushabiki wa siasa bungeni sio input hiyo?na wewe pia nakuambia kama Sugu alivyowaambia "acheni upuuzi kwenye mambo ya maana yanayogusa mamilioni ya viumbe wa Mungu Tz".bungeni ni mahala patakatifu,hatujawachagua wabunge kwenda kupageuza pango la kufichia wanyang'anyi.
 
Akichangia
bungeni,mheshimiwa Joseph Mbilinyi 'sugu' amemchanachana Mwigulu kuwa ni
mpumbavu,anafanya dili alafu anatumia m-pesa,akaendelea na waziri wa
elimu Mulugo kuwa ana elimu ya kuungaunga na ni chenga tupu,akadai
usalama wapo badala ya kumueleza rais kuwa jamaa huyo ni chenga tupu,wao
wanakalia kuifuatilia Chadema na kung'oa watu kucha na meno. Pamoja na
kukalishwa mara mbili na spika ili atumie lugha ya staha bado aliendelea
na baada ya kumaliza kuna wabunge kadhaa walisikika wakitaka kutoa
taarifa ila spika kawapotezea akamwita mchg.Natse aendelee
kuchangia.

yawezekana bi.kiroboto kaona ukweli hapo,ila usalama wa taifa umepwaya sana.
 
Hoja yake imesaidia vipi kuboresha bajeti ya Waziri Mkuu?Bunge sio Rock Concert, mbunge akiongea akimaliza inabidi kuwe na input alizoweka. Ukiona mbunge kamaliza halafu kinachojadili ni kwamba "kamchana Mwigulu" ujue kuna walakini.
Pia ukiona mbunge kaacha kujadili bajeti na " kaanza kuwachana chadema" ujue kuna hitilafu katika mfumo wake wa common sense
 
Kwa hakika hawa wabunge wa ccm ni janga kubwa kwa taifa letu.na kwa hakika hawa wabunge wa ccm watatupeleka kubaya,tutakao kuwepo tutashuhudia tz ya kuhuzunisha huko mbele..
 
Sugu kaongea kistaarabu.nampongeza sana,pa1 na elimu yake ya 4m 4 anajua anachokiongea.hakika nawambieni "ni heri kufa moyo au macho kuliko kufa fikra.wana ccm wote wamekufa fikra.ukibsha fuatilia michango yao hapa jf.wote kama mwingu na nape.
 
CCM walivyowapumbavu hakuna lugha ya kutumia tofauti na kuwapasha ukweli na kwa maneno makali maana hii nchi inaendeshwa kisanii sana. Nimesoma ripoti ya kufeli kwa wanafunzi 2010 kidogo nitokwe na machozi.
 
Mwigulu amewashika pabaya ndio maana wanatukana. Mwigulu is the man

Wakati mwingine huwa najiuliza sana, " hivi kwanini Mungu Aliweka tofauti kubwa sana ya kimtazamo baina ya wanadamu? " hata hivyo, sijawahi pata jibu linalokidhi hamu yangu ya kutaka kufahamu. Binafsi, sijaona tatizo la mchango wa Mh. Mbilinyi, 'SUGU' ; hivi, kwa namna ambavyo serikali yetu inatenda, ni neno gani hasa linaistahili? Ulimtaka 'SUGU' awe mnafiki dhidi ya dhamiri yake kwa kupunguza ukali wa maneno? Hiyo ni kawaida ya wanafiki. Neno kali litatumika tu, ilimradi limtendee haki mtamkiwa.
 
Wakati akichangia bajeti ya PM, Mh Mbilinyi ametumia lugha kali sana dhini ya serikali na Mwigulu Nchemba akazua ubishi mkubwa kati yake na Speaker..

Ameanza kwa kusema kuwa "Mwanamke mpumbavu huvunja nyumba yake mwenyewe" na hivyo hivyo serikali pumbavu hubomoa nchi.

Akasema kuwa walimnyanyapaa Mbatia na hoja yake ya Elimu na kukumbatia wapumbavu kama akina Mwigulu; na sasa matokeo ya Form 4 2012 yamewaumbua.

Amelaumu usalama wa Taifa kwa kushindwa kumshauri Rais hadi akamteua waziri wa elimu mwenye elimu ya kuunga unga.

Alipotakiwa kufuta neno upumbavu alikataa kata kata...

Tatizo Sugu analeta mambo ya mipasho mpaka bungeni hawa ndiyo wanajitapa kuwa wanataka kumkomboa mtanzania.
 
PHP:
hugochaves
kumbe ni CCM,huyu ndo aliyerusha barua na video ya lwakatare,anasubiri nini kukamatwa?
 
Amemtukana mwiguru kuwa ni mpumbavu.
Hizi bange bwana.
Na kama spika asingemzuia nchemba kutoa taarifa tungeshuhudua senema ingine maana mwiguru si mchezo kwa maneno.

.....na alitoa msaada ya watu wapumbavu wasiojua maana ya stupidity......
 
Back
Top Bottom