Mh. Mbilinyi (Sugu) alipuka bungeni

Mh. Mbilinyi (Sugu) alipuka bungeni

Dark City

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2008
Posts
16,252
Reaction score
11,648
Wakati akichangia bajeti ya PM, Mh Mbilinyi ametumia lugha kali sana dhini ya serikali na Mwigulu Nchemba akazua ubishi mkubwa kati yake na Speaker..

Ameanza kwa kusema kuwa "Mwanamke mpumbavu huvunja nyumba yake mwenyewe" na hivyo hivyo serikali pumbavu hubomoa nchi.

Akasema kuwa walimnyanyapaa Mbatia na hoja yake ya Elimu na kukumbatia wapumbavu kama akina Mwigulu; na sasa matokeo ya Form 4 2012 yamewaumbua.

Amelaumu usalama wa Taifa kwa kushindwa kumshauri Rais hadi akamteua waziri wa elimu mwenye elimu ya kuunga unga.

Alipotakiwa kufuta neno upumbavu alikataa kata kata...
 
Amemtukana mwiguru kuwa ni mpumbavu.
Hizi bange bwana.
Na kama spika asingemzuia Nchemba kutoa taarifa tungeshuhudua senema ingine maana Mwiguru si mchezo kwa maneno.
 
Ndo wakome! Nyoka alikuwa katika harakati ya kummeza chura, chura akakamata koo la nyoka na kuliminya kwa nguvu..Nyoka akashindwa kummeza! ngoma droo!
 
amesema Serikali hii ni sawa na mwanamke mpumbavu anaeiharibu nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.

hatuwezi kuwa na waziri mwenye elimu ya kuungaunga tutegemee elimu bora.!!
 
Hoja yake imesaidia vipi kuboresha bajeti ya Waziri Mkuu?

Bunge sio Rock Concert, mbunge akiongea akimaliza inabidi kuwe na input alizoweka. Ukiona mbunge kamaliza halafu kinachojadili ni kwamba "kamchana Mwigulu" ujue kuna walakini.
 
Kigwangala naye anachemka kishenzi...anasema kuwa serikali ispoacha upuuzi atachukua hatua mwenyewe...

Kwamba wanaandamana, wanaua watu na kung'oa kucha na meno...

Kama wataachwa yeye atahamasisha watu wa Nzega wawakamate na yeye atawashughulikia...

Amesema kuwa viongozi wote wa CHADEMA ni wapuuzi...

Na speaker hajaingilia kati...
 
Wa
Mwigulu amewashika pabaya ndio maana wanatukana. Mwigulu is the man
wana hasira kwa Mwigulu kumsema Mbowe,hadi wamechanganyikiwa.

Kigwa naye kawachana live kwamba ni wapuuzi,huh?
 
Back
Top Bottom