Mh.Makonda umejikwaa kidogo kumshambulia Pierre!

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Mh.Makonda @baba_keagan binafsi umejikwaa ,umeteleza kutamka maneno, wanafiki wanaokupigia makofi.

Wewe Mh.Makonda ni muumini mkubwa sana wa dini ya kikristo,unasoma biblia kutwa kucha ,najua unafahamu kuwa Riziki na neema kwa mtu hutolewa na Mungu,Mungu kwa wanadamu wake habagui hata kidogo,yeyote amuombaye humpa,humpa kwa namna tofauti haijalishi ni kupitia ulevi,au kupitia biashara,au kupitia usanii au kupitia uongozi vyote Mungu hujalia.

Ndio maana ukisoma Wakoritho2 9:8 inasema "Na Mungu anaweza kuwajaza kila neema kwa wingi,ili nanyi mkiwa na Riziki za kila namna siku zote ,impate kuzidisha sana katika kila tendo jema"

Kwa waislam kupitia Hadithi Qudsi Mungu anasema ,inasema (4.) Wewe hula riziki Yangu (kutoka Kwangu) na unaniasi, lakini unaponiomba Mimi hukuitikia.

Hivyo umejikwaa au kuteleza kumshambulia @officialpierre_liquid @officialpiere_liquid @pierre_konki_liquid ,Pierre amepaishwa na neema ya Mungu ,hao unaotaka wafahamike sio kwa matakwa yako au yao ni Mungu tuu. Mungu akitaka kukupaisha au kukuinua sio lazima vyombo vya habari.

vyombo vya habar hasa online bloggers wanafanya biashara wanatafuta viewers,Pierre sio mlevi namna hivyo ila ni mnywaji tuu akiambatanisha vituko,vichekesho na ucheshi watanzania wakatokea kumpenda hadi nje Kama Kenya,wakimuona wanacheka wanafurahi,media zinapata viewer,Wafanyabishara Kama @tullyswine wanamtumia kutangaza biashara,Mungu ana muinua ,Kuwa Brand Ambassador kila mtu anaweza kuwa ila hutegemea na potentiality yako kwa biashara hiyo,Pirre wana mtumia sababu ametokea kuwavutia umma.Watu wanapenda kumuona hivyo ni rahisi kupitia Pierre kuona kabisa na biashara anayoitangaza

Mfano,Dr.Shika walikuwa wanamtumia sababu watu hupenda kumuona anavyoongea hivyo kupitia hii watu wakawa wanamtumia ku brand biashara,waandishi katika kupata viewers,haya mambo ni uwezo wa Mungu,hao unaotaka wajulikane subiri hadi Mungu atakapo amua iwe hivyo,usilazimishi.Mbona ulitangaza nusu bei ya pombe?

@officialpierre_liquid usivunjike Moyo ,pambana kuna watu ni walevi wa kutupa ila ndio marafiki zetu ,mabosi zetu ,Ndugu zetu,viongozi wetu mbona hatuwasemi tumemuona Pierre tuu !
Piga kazi @officialpierre_liquid.Utabaki kuwa juuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana Nondo kwa maneno ya busara uliyomuusia mheshimiwa. Ni kweli ndg Makonda ni Mkristo anayejitambulisha kama mtumishi wa Mungu. Sasa katika hili amekosea sana kama sio kuteleza. Sisi wakristo tunafundishwa kuwa binadamu wote akiwemo Pierre tumeumbwa kwa sura ya Mungu. Hata mtu awe Rais,waziri,padre,Askofu,mchungaji, RC,DC,Dr, mkulima , mlevi au mwenye utapiamlo bado ni sura ya Mungu. Na kukiita kile alichokiumba Mungu kuwa ni cha hovyo, maanake ni kumdharau Mungu, na hili kosa huutwa kumkufuru Roho mtakatifu, dhambi ambayo n kubwa kuliko zote.
Ni kweli unaweza ukawa hupendezw na mafanikio ya konki, basi bora ungetumia lugha yenye staha kuliko iyo yenye viashiria vya dharau ya hali ya juu
 
Mh.Makonda @baba_keagan binafsi umejikwaa ,umeteleza kutamka maneno, wanafiki wanaokupigia makofi.

Wewe Mh.Makonda ni muumini mkubwa sana wa dini ya kikristo,unasoma biblia kutwa kucha ,najua unafahamu kuwa Riziki na neema kwa mtu hutolewa na Mungu,Mungu kwa wanadamu wake habagui hata kidogo,yeyote amuombaye humpa,humpa kwa namna tofauti haijalishi ni kupitia ulevi,au kupitia biashara,au kupitia usanii au kupitia uongozi vyote Mungu hujalia.

Ndio maana ukisoma Wakoritho2 9:8 inasema "Na Mungu anaweza kuwajaza kila neema kwa wingi,ili nanyi mkiwa na Riziki za kila namna siku zote ,impate kuzidisha sana katika kila tendo jema"

Kwa waislam kupitia Hadithi Qudsi Mungu anasema ,inasema (4.) Wewe hula riziki Yangu (kutoka Kwangu) na unaniasi, lakini unaponiomba Mimi hukuitikia.

Hivyo umejikwaa au kuteleza kumshambulia @officialpierre_liquid @officialpiere_liquid @pierre_konki_liquid ,Pierre amepaishwa na neema ya Mungu ,hao unaotaka wafahamike sio kwa matakwa yako au yao ni Mungu tuu. Mungu akitaka kukupaisha au kukuinua sio lazima vyombo vya habari.

vyombo vya habar hasa online bloggers wanafanya biashara wanatafuta viewers,Pierre sio mlevi namna hivyo ila ni mnywaji tuu akiambatanisha vituko,vichekesho na ucheshi watanzania wakatokea kumpenda hadi nje Kama Kenya,wakimuona wanacheka wanafurahi,media zinapata viewer,Wafanyabishara Kama @tullyswine wanamtumia kutangaza biashara,Mungu ana muinua ,Kuwa Brand Ambassador kila mtu anaweza kuwa ila hutegemea na potentiality yako kwa biashara hiyo,Pirre wana mtumia sababu ametokea kuwavutia umma.Watu wanapenda kumuona hivyo ni rahisi kupitia Pierre kuona kabisa na biashara anayoitangaza

Mfano,Dr.Shika walikuwa wanamtumia sababu watu hupenda kumuona anavyoongea hivyo kupitia hii watu wakawa wanamtumia ku brand biashara,waandishi katika kupata viewers,haya mambo ni uwezo wa Mungu,hao unaotaka wajulikane subiri hadi Mungu atakapo amua iwe hivyo,usilazimishi.Mbona ulitangaza nusu bei ya pombe?

@officialpierre_liquid usivunjike Moyo ,pambana kuna watu ni walevi wa kutupa ila ndio marafiki zetu ,mabosi zetu ,Ndugu zetu,viongozi wetu mbona hatuwasemi tumemuona Pierre tuu !
Piga kazi @officialpierre_liquid.Utabaki kuwa juuu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Pale unapoalikwa halafu unaombwa uzunguze nawe hukujipanga kuzungumza, kinafuata ni."...........”
 
Nondo unapiga nondo unatisha.
P
Kuna siku nlikuwa govorners napiga masanga kama kawaida yetu
Pembeni yetu alikaa dada mmoja na wenzake mmoja wao alikuwa kwenye mode mbaya,kama alikwazika na jambo fulani muda tu
Maraa dj ndani mule anatangaza leo govorners kinondoni imetembelewa na pierre mzee wa liquid yule dada alipokuja muona wachaa aanzee kucheka mbavu hana
Kwa hiyo upigaji tungi wake pierre muonekano,u fupi ule,maneno yke lazima watu watafurahi na kicheko juu!

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom