Mh.Makonda umejikwaa kidogo kumshambulia Pierre!

Mh.Makonda umejikwaa kidogo kumshambulia Pierre!

Huyo kibwengo Pierre is a talent-less, unfunny, fake, alcoholic midget full of nonsense. Huwezi kumlinganisha na marehemu Mzee Majuto, mfano. Hapawsi kabisa kupewa promo kwenye jamii sababu ni mpuuzi.
Kila mtu na nafasi yake wewe... sasa aloekwambia umlinganishe na majuto nani....
Haya wacheza mpira wna style tofauti so kama hupendi style yake ya uchekeshaji sio kwamba hajui....
Au wivu tu mkuu
 
Una kipaji kikubwa sana cha kujenga hoja na kuzipanga kwa ustadi mkubwa na kuziwakilisha kwa msomaji katika mtiririko unaovutia kuendelea kusoma hadi mwisho. Hongera sana Abdul Nondo na nondo zako za uhakika.

Mh.Makonda @baba_keagan binafsi umejikwaa ,umeteleza kutamka maneno, wanafiki wanaokupigia makofi.

Wewe Mh.Makonda ni muumini mkubwa sana wa dini ya kikristo,unasoma biblia kutwa kucha ,najua unafahamu kuwa Riziki na neema kwa mtu hutolewa na Mungu,Mungu kwa wanadamu wake habagui hata kidogo,yeyote amuombaye humpa,humpa kwa namna tofauti haijalishi ni kupitia ulevi,au kupitia biashara,au kupitia usanii au kupitia uongozi vyote Mungu hujalia.

Ndio maana ukisoma Wakoritho2 9:8 inasema "Na Mungu anaweza kuwajaza kila neema kwa wingi,ili nanyi mkiwa na Riziki za kila namna siku zote ,impate kuzidisha sana katika kila tendo jema"

Kwa waislam kupitia Hadithi Qudsi Mungu anasema ,inasema (4.) Wewe hula riziki Yangu (kutoka Kwangu) na unaniasi, lakini unaponiomba Mimi hukuitikia.

Hivyo umejikwaa au kuteleza kumshambulia @officialpierre_liquid @officialpiere_liquid @pierre_konki_liquid ,Pierre amepaishwa na neema ya Mungu ,hao unaotaka wafahamike sio kwa matakwa yako au yao ni Mungu tuu. Mungu akitaka kukupaisha au kukuinua sio lazima vyombo vya habari.

vyombo vya habar hasa online bloggers wanafanya biashara wanatafuta viewers,Pierre sio mlevi namna hivyo ila ni mnywaji tuu akiambatanisha vituko,vichekesho na ucheshi watanzania wakatokea kumpenda hadi nje Kama Kenya,wakimuona wanacheka wanafurahi,media zinapata viewer,Wafanyabishara Kama @tullyswine wanamtumia kutangaza biashara,Mungu ana muinua ,Kuwa Brand Ambassador kila mtu anaweza kuwa ila hutegemea na potentiality yako kwa biashara hiyo,Pirre wana mtumia sababu ametokea kuwavutia umma.Watu wanapenda kumuona hivyo ni rahisi kupitia Pierre kuona kabisa na biashara anayoitangaza

Mfano,Dr.Shika walikuwa wanamtumia sababu watu hupenda kumuona anavyoongea hivyo kupitia hii watu wakawa wanamtumia ku brand biashara,waandishi katika kupata viewers,haya mambo ni uwezo wa Mungu,hao unaotaka wajulikane subiri hadi Mungu atakapo amua iwe hivyo,usilazimishi.Mbona ulitangaza nusu bei ya pombe?

@officialpierre_liquid usivunjike Moyo ,pambana kuna watu ni walevi wa kutupa ila ndio marafiki zetu ,mabosi zetu ,Ndugu zetu,viongozi wetu mbona hatuwasemi tumemuona Pierre tuu !
Piga kazi @officialpierre_liquid.Utabaki kuwa juuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana Nondo kwa maneno ya busara uliyomuusia mheshimiwa. Ni kweli ndg Makonda ni Mkristo anayejitambulisha kama mtumishi wa Mungu. Sasa katika hili amekosea sana kama sio kuteleza. Sisi wakristo tunafundishwa kuwa binadamu wote akiwemo Pierre tumeumbwa kwa sura ya Mungu. Hata mtu awe Rais,waziri,padre,Askofu,mchungaji, RC,DC,Dr, mkulima , mlevi au mwenye utapiamlo bado ni sura ya Mungu. Na kukiita kile alichokiumba Mungu kuwa ni cha hovyo, maanake ni kumdharau Mungu, na hili kosa huutwa kumkufuru Roho mtakatifu, dhambi ambayo n kubwa kuliko zote.
Ni kweli unaweza ukawa hupendezw na mafanikio ya konki, basi bora ungetumia lugha yenye staha kuliko iyo yenye viashiria vya dharau ya hali ya juu
Shukrani umeongea vyema sana Mkuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo kibwengo Pierre is a talent-less, unfunny, fake, alcoholic midget full of nonsense. Huwezi kumlinganisha na marehemu Mzee Majuto, mfano. Hapawsi kabisa kupewa promo kwenye jamii sababu ni mpuuzi.
Nani anafaa kupewa promo , Pierre hakupewa promo na media ! Watanzania walimpenda na kumfurahia maneno yake ,anavyo act na kunywa ! Hapo media ndio zikafuata yote haya ni majaliwa ya Mingu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku nlikuwa govorners napiga masanga kama kawaida yetu
Pembeni yetu alikaa dada mmoja na wenzake mmoja wao alikuwa kwenye mode mbaya,kama alikwazika na jambo fulani muda tu
Maraa dj ndani mule anatangaza leo govorners kinondoni imetembelewa na pierre mzee wa liquid yule dada alipokuja muona wachaa aanzee kucheka mbavu hana
Kwa hiyo upigaji tungi wake pierre muonekano,u fupi ule,maneno yke lazima watu watafurahi na kicheko juu!

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Yes ,watu wanampenda tuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una kipaji kikubwa sana cha kujenga hoja na kuzipanga kwa ustadi mkubwa na kuziwakilisha kwa msomaji katika mtiririko unaovutia kuendelea kusoma hadi mwisho. Hongera sana Abdul Nondo na nondo zako za uhakika.
Shukrani sana Kaka yangu BAK tupo pamoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom