Mh.Kagasheki: RPC Arusha awatorosha majangili

Mh.Kagasheki: RPC Arusha awatorosha majangili

Nimemsikia Waziri kagasheki akilalamikia polisi wa vyeo vya juu kufifisha vita dhidi ya ujangili na kwamba baadhi yao wanashiriki kuwaachia/kuwatorosha watuhumiwa. Sijui kwa nini viongozi wetu wa serikali tena viongozi wa juu wanalalamika kwenye vyombo vya habari kuhusu udhaifu ndani ya serikali. Wanashindwa nini kuzungumza na kuchukua hatua stahiki kuliko kuja kutulalamikia sisi wananchi.

Hivi Waziri anapolalama hajui kuwa anaidhalilisha serikali yake. Kagasheki anawalalamikia polisi wakati yeye ni Waziri, na zaidi alishakuwa Waziri wa mambo ya ndani akiwasimamia polisi! Kama hawezi kuchukua hatua si amwendee Raisi wake ili achukue hatua. Inakera kusikia Waziri au Kiongozi coyote wa serikali akilalamika.

Hakuna la ajabu. Katika serikali ya awamu hii almost kila kiongozi analalamika.
 
Mhe Kagasheki amenukuliwa Na ITV akisema kuna mtu amemupigia simu akimuonya aache kumufatafata la sivyo atamshitaki kwa mhe rais
sasa swali la kujiuliza je ?rais analinda majangili ?

Heee hii nayo mpya!!..

Kweli Serikali ya kishkaji..
 
Magesa mulongo kumbe nae ni balaaaaaaa!
 
Ukisikia majanga ndiyo haya sasa polisi wamekuwaje tena wakibainika ni vema sheria itembee juu ya migongo yao.

Toka lini panya akamfitini panya mwenza! Bado mtayasema yote mlowafisadi wananchi magamba nyie.
 
Mhe Kagasheki amenukuliwa Na ITV akisema kuna mtu amemupigia simu akimuonya aache kumufatafata la sivyo atamshitaki kwa mhe rais
sasa swali la kujiuliza je ?rais analinda majangili ?

na wasiwasi atakuwa kinanananannaaaa
 
Leo nimefurahi sana angalau simiyu yetu naye ameonyesha uzalendo kwa kuchukizwa na jambo hili.Nina amini Mungu yupo na siku moja ukweli utashinda na nchi yetu itakombolewa
Hana uzalendo huyo.... Ni kwa vile tu katajwa na mwana CCM mwenzie... Si mnakumbuka walivyotoka povu kumtetea Kinana kwa vile alitajwa na Msigwa..??? Na watatajana sana mpaka kufika mwaka 2015
 
daaah hii hatari hivi huyo katibu mkuu wa MAGAMBA hausiki kweli?daaah polisiccm mtatumaliza.
 
Hakuna la ajabu. Katika serikali ya awamu hii almost kila kiongozi analalamika.
Siyo almost, ni wote... Uwaulize maandishi ya kwenye makaratasi sasa, utawasikia MEGAWATI, MFUMUKO WA BEI UMESHUKA KWA ASILIMI KADHAA, UMASIKINI UMESHUKA KWA ASILIMIA KADHAA, ELIMU IMEPANDA KWA ASILIMIA KADHAA, KIWANGO CHA UFAULU KIMEPANDA..... Yaani full maandishi yasiyoendana na ukweli aua hali halisi
 
RPC Arusha kuchukuliwa hatua baada ya kuhusika kuwatorosha majangili raia wewenye asili ya kiarabu mapema baada ya kukamatwa wakihusika na ujangili.

Hii ni kwa mujibu wa Waziri Wa maliasilia na Utalii alipoongea na vyombo vya habari leo hii.

Mh. Kagasheki amesema kuwa RPC huyo alihusika moja kwa moja kuwatorosha majangili hao ambapo aliwarudihia passport na kusaidia kuwapa mbinu za namna ya kutoroka nchini baada ya yeye kuruhusu waachiwe baada ya kukamaatwa.

Source: Clouds F-Taarifa ya habari saa 12 jioni!

Kova wapi? Majangili dentists wanazidi kuongezeka polisi na majeshi...ndio MAANA hakuna wa kumkamata Chief Dentists Msomali??
 
Haya maswala yametokea arusha ambako lema ndiyo mbunge na lema tabia yake iko wazi sasa mnategemea nini.
 
Back
Top Bottom