Mh.Kagasheki: RPC Arusha awatorosha majangili

Mh.Kagasheki: RPC Arusha awatorosha majangili

Watu hamjamuelewa waziri! Askari alietorosha hao majangili sio RPC sabas, ni OCD ila hakumtaja jina wala kusema ni wa wilaya gan.

Sema sabas Arusha imemshinda bora alivyokuwa Manyara.

Kwa mujibu wa clouds fm, ni RPC wa Arusha lbd wewe pia utwambie OCD nae alifanya hili wakati mwingine au ndo mchezo wao!
 
Nimemsikia Waziri kagasheki akilalamikia polisi wa vyeo vya juu kufifisha vita dhidi ya ujangili na kwamba baadhi yao wanashiriki kuwaachia/kuwatorosha watuhumiwa. Sijui kwa nini viongozi wetu wa serikali tena viongozi wa juu wanalalamika kwenye vyombo vya habari kuhusu udhaifu ndani ya serikali. Wanashindwa nini kuzungumza na kuchukua hatua stahiki kuliko kuja kutulalamikia sisi wananchi.

Hivi Waziri anapolalama hajui kuwa anaidhalilisha serikali yake. Kagasheki anawalalamikia polisi wakati yeye ni Waziri, na zaidi alishakuwa Waziri wa mambo ya ndani akiwasimamia polisi! Kama hawezi kuchukua hatua si amwendee Raisi wake ili achukue hatua. Inakera kusikia Waziri au Kiongozi coyote wa serikali akilalamika.
 
Anasema anaamini Amiri jeshi mkuu ataendelea kumwamini inamaana anadoubt hata kazi yake kwa sababu system nzima ni ujangili kwa kwenda Mbele huyo RPC wa Arusha aanze na KInana akitua tu Arusha
 
Sasa utaona NCHIMBI na MWEMA watakavyokaa kimya wakisubiri kauli ya RAIS.Mizigo mingine bwana....!

Wanaweza wakaibuka kesho kujibu serikali ya Kikwete kusutana ndio mchezo wao hizo kagasheki kaja na la ujangili ili kupotezea kauli ya Zitto ya kwamba CCM haijapeleka mahesabu ya fedha za umma chezea CCM kwa ujangili wa maneno
 
Bei ya meno ndio sababu ya ujangili kuongezeka!
Kg 1 inauzwa dola1500-2000.
Kazi kwelikweli!
 
One of my friends yupo kwenye hiyo operation,anasema waliwakamata broker (kuna mwindaji,broker,mnunuzi wa ndani na mnunuzi wa nje),yule broker aliwapa full information (alikuwa supportive) wakaenda kwa mnunuzi wa ndani ambaye aliwaeleza kuwa ni kweli anahusika na wanunuzi wa nje (waasia) washafika nchini na wapo hoteli fulani,akawaelezea namna hata ya kuwakuta na exhibit ,timu ikapanga ambush,wakati wakijiandaa kumkamata manyota akauza info kwa muasia,lakini kwa bahati nzuri timu ilikuwa na plan b ambayo ilimkamatisha/wakamatisha,manyota alipoona kashindwa kuzuia,akaona akachezee ngoma kituoni,maelezo yaliandikwa na mkubwa na yalionyesha walikamatwa kwa bahati mbaya kwani walikuwa vacation,akatumia nguvu aliyonayo kwamba ubalozi wa waasia unacomplain sana kwa wakubwa,so wacha wapewe dhamana wakati upelelezi unaendelea.
So timu ilibaki disappointed coz nasikia jamaa walikuwa na full vidhibiti ambavyo wangefikishwa kwa pilato wasingechomoza.(Am not sure about the truth of the story,lakini aliyenipa ni officer aliye kwenye hiyo timu ya kudhibiti majangili).Sasa my point ni kuwa kama waziri analalamika,nguvu na mamlaka ya kuchukua hatua tutegemee kutoka kwa nani?
 
Labda hakuwa na muda kwani askari polisi si kikwazo kwa ujangili tu bali ktk mabo yote yanayopitia mezani/mikononi mwao.
 
Yaani Lebaretus Sabas huyu huyu niliyekaa naye meza moja akitupiga mikwara na vitisho majuzi?

Akamatwe haraka sana, tena kama ni arrest warrant nikabidhiwe mimi!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hayo maccm yenyewe yanaogopana,hakuna wa kumsimamisha mwingine kazi,eti kakosea,mbona yanasemaga live sijiuzuru ng'o.wanajuana jinsi kila mmoja kwa nafasi yake anavyoiba.hivyo hakuna wa kumwadhibu huyo Rpc,hakuna cha mwema,nchi bi,waziri mkuu wala rais wa kuthubutu kumchukulia hatua.
 
Akamatwe mara moja na kupelekwa mahakamani afungwe maisha au apigwe risasi kabisa.

Safi sana Simiyu yetu. Yaone mwenyewe ya utawara wa panya. Angalau Kagasheki amethubutu japo kwa matamshi yake sasa ni adui wa mfumo magamba. RPC amewekwa huko na Rais na kazi anayoifanya ametumwa na rais.
 
Huyu Kagasheki ni MNAFIKI MKUBWA kwani yeye alikuwa Waziri wa Mambo ya ndani na ameondoka hiyo wizara si siku nyingi na hao akina Liberatus amewalea yeye na ameshiriki kuwapandisha vyeo leo anataka kusema nini?

Anamfahamu Liberatus RPC wa arusha siku nyingi na kwa nini nisi amini wana ugomvi binafsi wa siku nyingi?
 
Kwa nini hakumtaja na aaliyemtishia NYAU?
 
Ila sana sana Kama Jk akijitutumua,basi utasikia kasimamishwa kazi ili uchunguzi ufanyike,na hutakuja kusikia Majibu ya uchunguzi huo ng'o.mwisho utasikia kapewa mkuu wa bodi Fulani ili andelee kupiga hela,
 
Wallahi kwa serikali hii ilivyo utasikia RPC huyu eti kapandishwa cheo!!
 
Back
Top Bottom