Mh.Kagasheki: RPC Arusha awatorosha majangili

RPC Arusha kuchukuliwa hatua baada ya kuhusika kuwatorosha majangili raia wewenye asili ya kiarabu mapema baada ya kukamatwa wakihusika na ujangili.

Hii ni kwa mujibu wa Waziri Wa maliasilia na Utalii alipoongea na vyombo vya habari leo hii.

Mh. Kagasheki amesema kuwa RPC huyo alihusika moja kwa moja kuwatorosha majangili hao ambapo aliwarudihia passport na kusaidia kuwapa mbinu za namna ya kutoroka nchini baada ya yeye kuruhusu waachiwe baada ya kukamaatwa.

Source: Clouds F-Taarifa ya habari saa 12 jioni!
Vipi kinana alikuwepo katika dili hilo?
 
sasa mkuu hapo mulongo kaingiaje?
Mulongo si ndiye mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ambayo RPC ni lieutenant wake. Mbona alimtuma kumvamia Lema ucku wa manane? Kwa nini asione umuhimu wa nyra za taifa. Apigwe tu Mulongo maana tumechoka sie.
 
RPC Arusha kuchukuliwa hatua baada ya kuhusika kuwatorosha majangili raia wewenye asili ya kiarabu mapema baada ya kukamatwa wakihusika na ujangili.

Hii ni kwa mujibu wa Waziri Wa maliasilia na Utalii alipoongea na vyombo vya habari leo hii.

Mh. Kagasheki amesema kuwa RPC huyo alihusika moja kwa moja kuwatorosha majangili hao ambapo aliwarudihia passport na kusaidia kuwapa mbinu za namna ya kutoroka nchini baada ya yeye kuruhusu waachiwe baada ya kukamaatwa.

Source: Clouds F-Taarifa ya habari saa 12 jioni!

Haya yalikuwa maneno ya Ezekiel Maige, mara baada ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, na yeye kuwekwa kando. Aliandika hivi;

Ndugu zangu na rafiki zangu.

Kwanza niwape pole kwa mshituko mlioupata kwa haya yaliyojitokeza. Naomba msisikitike sana. Kila jambo alilopanga Mola hutokea kadiri ya mapenzi yake. Route ya maisha ya mwanadamu hupangwa na Mola mara tu anapompulizia pumzi ya uhai. Hili lilipangwa hata kabla sijatokea duniani miaka 42 iliyopita!

Mungu hakushindwa kumwokoa mwanawe Yesu asisulubiwe, tena kwa kuonewa! Hasha, tungeupataje ukombozi bila hilo kutokea? Wakati mwingine Mungu hutoa nafasi kwa mambomagumu kuwafika waja wake, si kwamba hawapendi,bali ili unabii utimie. Ilifika wakati hata Yesu akaona kama Mungu kamuacha! Hasa sisi kwa hili tunaweza kudhani Mungu katuacha! Hasha, ni njia ya kuufikia ukombozi wa kweli.

Pili, kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa, yaliyotokea ni ushahidi kwamba maliasili ni ngumu. Kukabiliala na wabaya ni kazi ngumu. Wapo waliojipanga ukiwavamia ovyoovyo unaondoka wewe. Ndivyo ilivyotokea.

Niwahakikishie, wazalendo wamepoteza mpambanaji. Nimepambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na vijijini ndani na nje ya nchi. Nilitumia kila aina ya uwezo wangu kulizawadia taifa langu utumishi uliotukuka. Sikubakisha chembe ya energy.

Waziri gani aliyesimamia sheria na kuwapa vitalu watanzania maskini wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza?

Waziri gani aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina Kamrani na wenzake? Watu wametumia records za matukio ya 2009/10 kuficha matendo na maamuzi ya kishujaa ya maige ya 2011. Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata. Tena si siku nyingi. Niliwaomba wenzangu wamwogope Mungu. Bado nasisisitza hivyo, si Mungu wangu kama ilivyodhaniwa, bali Mungu wetu wa haki.

Waziri gani aliyefunga biashara ya wanyamahai?

Waziri gani aliyeonyesha mfano wa kuchukua hatua kwa watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Maige hakusita kuchukua hatua.

Maamuzi haya ni magumu na yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa. Nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda. Nilisema Bungeni, watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini. Muda haukuruhusu, ila nitarudi Bungeni na nitasema.

Imesemwa issue ya nyumba. Nimefafanua na kutoa vielelezo. Kila mbunge aliyetaka amekopeshwa shs 290m, wengine wameanzisha biashara na wengine wamenununua magari na wengine majumba. Wapo walioficha, na tupo tuliojiweka wazi! Mkopo wangu huo umekuwa my contribution na balance kulipwa na benki na nyumba kuimortgage. Nimetoa nyaraka zote kwa wanahabari na vyombo vyote husika. Nimesema mwenye mashaka aende kwa Msajili wa hati wizara ya ardhi, au kwa kamishna wa maadili, au CRDB Azikiwe na Dodoma nilikokopa au amtafute muuzaji. Kote huko utapata rekodi ya bei na mode of payment. Wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei tofauti na niliyonunulia. Manasheria wangu anashughulikia hilo.

Niwahakikishie, vita nimepigana, imani na dhamana nimeilinda, muda wa kutuzwa na mwenye kumbukumbu sahihi, Mungu utafika. Naamini nimejiwekea akiba isyooza Mbiguni.

Yapo mengi yasiyo sahihi yaliyosemwa. Nitakuwa nafafanua kila nipatapo fursa na muda utazidi kutufunua. Kwa kifupi, kwa suala la vitalu, hakuna kampuni hata moja iliyopewa kitalu cha uwindaji bila kuomba, kukaguliwa na kamati ya ushauri na hatimaye kupewa alama. Kampuni zisizokuwa na sifa ni zile zilizopata chini ya alama 50. Na kwa kampuni zilizokuwa kwenye biashara, passmark ni alama 40 kwa mujibu wa kanuni ya 16(5) ya kanuni za uwindaji wa kitalii za mwaka 2010. Hakuna kampuni iliyopata chini ya alama 50 iliyopata kitalu. Hakuna kampuni ya kizalendo iliyopendekezwa na kamati ya ushauri ambayo haikupewa kitalu.

Kwa upande wa report ya CAG, haikunigusa binafsi kwani ilikuwa inaishia juni 2010 wakati mimi ilishika dhamana Novemba 2010.

Ka upande wa biasharaya wanyamahai, hakuna wanyama waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati wangu (2011), na matukio ya utoroshaji tulipoyabaini, tulifungua mashitaka kwa watuhumiwa nakufnug biashara hiyo.

Naanza kazi ya kuwawakilisha wananchi wa Msalala. Nitawawakilisha kwa mujibu wa katiba na ahadi zangu kwao hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo.

Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana. Ka wakristo, naomba msome Mwanzo 4:1-15.
 
One of my friends yupo kwenye hiyo operation,anasema waliwakamata broker (kuna mwindaji,broker,mnunuzi wa ndani na mnunuzi wa nje),yule broker aliwapa full information (alikuwa supportive) wakaenda kwa mnunuzi wa ndani ambaye aliwaeleza kuwa ni kweli anahusika na wanunuzi wa nje (waasia) washafika nchini na wapo hoteli fulani,akawaelezea namna hata ya kuwakuta na exhibit ,timu ikapanga ambush,wakati wakijiandaa kumkamata manyota akauza info kwa muasia,lakini kwa bahati nzuri timu ilikuwa na plan b ambayo ilimkamatisha/wakamatisha,manyota alipoona kashindwa kuzuia,akaona akachezee ngoma kituoni,maelezo yaliandikwa na mkubwa na yalionyesha walikamatwa kwa bahati mbaya kwani walikuwa vacation,akatumia nguvu aliyonayo kwamba ubalozi wa waasia unacomplain sana kwa wakubwa,so wacha wapewe dhamana wakati upelelezi unaendelea.
So timu ilibaki disappointed coz nasikia jamaa walikuwa na full vidhibiti ambavyo wangefikishwa kwa pilato wasingechomoza.(Am not sure about the truth of the story,lakini aliyenipa ni officer aliye kwenye hiyo timu ya kudhibiti majangili).Sasa my point ni kuwa kama waziri analalamika,nguvu na mamlaka ya kuchukua hatua tutegemee kutoka kwa nani?

nchi ikisha vurugwa na rushwa ni shida sana kufanya operesheni yoyote ukafanikiwa!
 
Haya yalikuwa maneno ya Ezekiel Maige, mara baada ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, na yeye kuwekwa kando. Aliandika hivi;

Ndugu zangu na rafiki zangu.

Kwanza niwape pole kwa mshituko mlioupata kwa haya yaliyojitokeza. Naomba msisikitike sana. Kila jambo alilopanga Mola hutokea kadiri ya mapenzi yake. Route ya maisha ya mwanadamu hupangwa na Mola mara tu anapompulizia pumzi ya uhai. Hili lilipangwa hata kabla sijatokea duniani miaka 42 iliyopita!

Mungu hakushindwa kumwokoa mwanawe Yesu asisulubiwe, tena kwa kuonewa! Hasha, tungeupataje ukombozi bila hilo kutokea? Wakati mwingine Mungu hutoa nafasi kwa mambomagumu kuwafika waja wake, si kwamba hawapendi,bali ili unabii utimie. Ilifika wakati hata Yesu akaona kama Mungu kamuacha! Hasa sisi kwa hili tunaweza kudhani Mungu katuacha! Hasha, ni njia ya kuufikia ukombozi wa kweli.

Pili, kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa, yaliyotokea ni ushahidi kwamba maliasili ni ngumu. Kukabiliala na wabaya ni kazi ngumu. Wapo waliojipanga ukiwavamia ovyoovyo unaondoka wewe. Ndivyo ilivyotokea.

Niwahakikishie, wazalendo wamepoteza mpambanaji. Nimepambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na vijijini ndani na nje ya nchi. Nilitumia kila aina ya uwezo wangu kulizawadia taifa langu utumishi uliotukuka. Sikubakisha chembe ya energy.

Waziri gani aliyesimamia sheria na kuwapa vitalu watanzania maskini wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza?

Waziri gani aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina Kamrani na wenzake? Watu wametumia records za matukio ya 2009/10 kuficha matendo na maamuzi ya kishujaa ya maige ya 2011. Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata. Tena si siku nyingi. Niliwaomba wenzangu wamwogope Mungu. Bado nasisisitza hivyo, si Mungu wangu kama ilivyodhaniwa, bali Mungu wetu wa haki.

Waziri gani aliyefunga biashara ya wanyamahai?

Waziri gani aliyeonyesha mfano wa kuchukua hatua kwa watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Maige hakusita kuchukua hatua.

Maamuzi haya ni magumu na yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa. Nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda. Nilisema Bungeni, watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini. Muda haukuruhusu, ila nitarudi Bungeni na nitasema.

Imesemwa issue ya nyumba. Nimefafanua na kutoa vielelezo. Kila mbunge aliyetaka amekopeshwa shs 290m, wengine wameanzisha biashara na wengine wamenununua magari na wengine majumba. Wapo walioficha, na tupo tuliojiweka wazi! Mkopo wangu huo umekuwa my contribution na balance kulipwa na benki na nyumba kuimortgage. Nimetoa nyaraka zote kwa wanahabari na vyombo vyote husika. Nimesema mwenye mashaka aende kwa Msajili wa hati wizara ya ardhi, au kwa kamishna wa maadili, au CRDB Azikiwe na Dodoma nilikokopa au amtafute muuzaji. Kote huko utapata rekodi ya bei na mode of payment. Wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei tofauti na niliyonunulia. Manasheria wangu anashughulikia hilo.

Niwahakikishie, vita nimepigana, imani na dhamana nimeilinda, muda wa kutuzwa na mwenye kumbukumbu sahihi, Mungu utafika. Naamini nimejiwekea akiba isyooza Mbiguni.

Yapo mengi yasiyo sahihi yaliyosemwa. Nitakuwa nafafanua kila nipatapo fursa na muda utazidi kutufunua. Kwa kifupi, kwa suala la vitalu, hakuna kampuni hata moja iliyopewa kitalu cha uwindaji bila kuomba, kukaguliwa na kamati ya ushauri na hatimaye kupewa alama. Kampuni zisizokuwa na sifa ni zile zilizopata chini ya alama 50. Na kwa kampuni zilizokuwa kwenye biashara, passmark ni alama 40 kwa mujibu wa kanuni ya 16(5) ya kanuni za uwindaji wa kitalii za mwaka 2010. Hakuna kampuni iliyopata chini ya alama 50 iliyopata kitalu. Hakuna kampuni ya kizalendo iliyopendekezwa na kamati ya ushauri ambayo haikupewa kitalu.

Kwa upande wa report ya CAG, haikunigusa binafsi kwani ilikuwa inaishia juni 2010 wakati mimi ilishika dhamana Novemba 2010.

Ka upande wa biasharaya wanyamahai, hakuna wanyama waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati wangu (2011), na matukio ya utoroshaji tulipoyabaini, tulifungua mashitaka kwa watuhumiwa nakufnug biashara hiyo.

Naanza kazi ya kuwawakilisha wananchi wa Msalala. Nitawawakilisha kwa mujibu wa katiba na ahadi zangu kwao hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo.

Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana. Ka wakristo, naomba msome Mwanzo 4:1-15.

Ukweli una tabia ya kuchelewa kujitokeza... Naanza kuamini kuna wabunge walijitokeza kuchangia wakionyesha wana uchungu sana maliasili zetu kumbe walikua ni chui waliovaa ngozi ya kondoo!
 
Siamini kama Kagasheki amegundua uhalifu wa wanyamapori sasa hivi.Tatizo la ujangili liliwekwa wazi na Msigwa kitambo na bado hakulifanyia kazi. Serikali ya marekani nayo ililiongelea wakati wa ziara ya Obama.Jambo la kujiuliza kwa nini sasa.Labda jambo hili limechangiwa na mgogoro wa Kagera. Isije ikawa waliomtetea adui yake mkubwa,Meya wa Kagera,wanahusika na huu ujangili.Mtu mwenye ujasili wa kumtishia waziri na waziri akaishia kulalamika kwenye vyombo vya habari,lazima awe mtu mwenye sauti kubwa sana.Isije ikawa Kinana alikuwa upande wa Meya hivyo Kagasheki kaamua kuharibu biashara yake ya ujangili.Kama ni hivyo basi Kagasheki haiwezi vita hiyo maana msomali huyo kamshika vilivyo JK,anatwanga maji kwenye kinu.Vita dhidi ya ujangili itafanikiwa tu CCM ikiondoka.
 
Akamatwe mara moja na kupelekwa mahakamani afungwe maisha au apigwe risasi kabisa.

Ni kweli kabisa kwani ana makosa manne makubwa aliyoyafanya katika utumishi wake
1. Alisaidia na kupanga shambulizi la Bomu pale kwenye mkutano wa CDM Soweto
2. Alisaidia kuwatorosha wale waarabu waliohusishwa na Mlipuko wa Bomu pale kanisani Olasiti
3. Alifanikisha kutoroka kwa wale waharifu waliomchinja Mwenyekiti wa CDM pale Usariver
4. Amehusika kuwatorosha waarabu ambao walikamatwa kwa ujangiri wa wanyama Poli

Huyu nina wasiwasi atakuwa ni mjumbe katika kikosi kazi cha Kinana cha Tokomeza Tembo Tanzania (TTT) sidhani kama atashughulikiwa .
 
Yaani Lebaretus Sabas huyu huyu niliyekaa naye meza moja akitupiga mikwara na vitisho majuzi?

Akamatwe haraka sana, tena kama ni arrest warrant nikabidhiwe mimi!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
huyo anatakia ale kitanzi au risasi ya kichwa,hafai kabisa.
 
Kagasheki andaa ushahidi, weka hata number ya simu iliyokupigia kwa mwanzo tu
 
hii habari nimeiona itv usiku huu...nimesikiliza kaga..nimeogopa

Yeye mwenyewe Kaga alikuwa anaongea huku anatetema akionyesha dhahiri vita iliyo mbele yake imemshinda kabla hajaianza."mahewa".
 
Kwa mujibu wa clouds fm, ni RPC wa Arusha lbd wewe pia utwambie OCD nae alifanya hili wakati mwingine au ndo mchezo wao!

Waziri alisema ni askari mwenye nyota begani na kavaa nguo za serikali. Hakutaja cheo wala jina la askari huyo.

Sasa na me nakwambia alietorosha hao majangili ni OCD na sio RPC. Umem quote vibaya waziri.

Ila bado narudia hii movie ni kubwa hiyo ya ujangili ni cover up manake RPC WA KILIMANJARO NA ARUSHA WALIKUWA WAMEKALIA KUTI KAVU TOKA ILI ISHU YA DEFENDER YA RCO ARUSHA KUKAMATWA NA BANGE MOSHI. KIMSINGI WALITAKIWA WAMALIZANE BILA KWENDA KWENYE PRESS NA MATOKEO YAKE WAKACHAFUA JESHI NA KULIPAKA MATOPE WAKATI NI ISHU WANGEWEZA KUSOLVE NDAN YA JESHI. AIBU WALIMPA HAD IGP IKABIDI AFUKUZE ASKARI KAZI.

SASA WAMEMUINGIZA KWENYE KUMI NA NANE NA KAJAA! NGOMA KACHEZA OCD YEYE ANABWAGIWA MZIGO. TUSUBIRI RPC WA MOSHI WATAMTEGA VIP THEN UTA CONNECT MATUKIO VIZURI. NADHAN KABLA MKUBWA WAO HAJAACHIA KITU LAZMA ATAKUWA AMESHAWACHEZESHA GWARIDE KALI NA KUBANDUA MAWE YAO MABEGANI.
 
RPC Arusha kuchukuliwa hatua baada ya kuhusika kuwatorosha majangili raia wewenye asili ya kiarabu mapema baada ya kukamatwa wakihusika na ujangili.

Hii ni kwa mujibu wa Waziri Wa maliasilia na Utalii alipoongea na vyombo vya habari leo hii.

Mh. Kagasheki amesema kuwa RPC huyo alihusika moja kwa moja kuwatorosha majangili hao ambapo aliwarudihia passport na kusaidia kuwapa mbinu za namna ya kutoroka nchini baada ya yeye kuruhusu waachiwe baada ya kukamaatwa.

Source: Clouds F-Taarifa ya habari saa 12 jioni!
Kwa mtaji huu mheshimiwa Kagasheki kazi unayo. No wonder ulitaka majangili wakikamatwa watwangwe risasi. Nakubaliana na hoja yako ingawa wengi hawaitaki. Hata huyo RPC alitakiwa apigwe risasi hadharani na hapo ndio nchi itakuwa na maadili
 
Hakuna la ajabu. Katika serikali ya awamu hii almost kila kiongozi analalamika.

sisi wenyewe tupo nyuma ya key board hapa tunalalamika,nchi hii kila mahali ni malalamiko na vilio km wakina mama wa galilaya.
 
Back
Top Bottom