Mgomo wa wafanyabiashara Mwanza: Maduka yafungwa kupinga mashine za TRA!

Ni aibu kwa nchi kulazimisha aina ya kifaa kuuzwa kwa bei kubwa ili kbariki ulaji wa baadhi ya vigogo wa serikali wenye hisa na biashara hiyo.
wananchi wakikubaliana na unyonyaji huo utakuwa ni UZOBA uliopitiliza. Wakomae tuu.
 
maduka yote yamefungwa, nilikuwepo leo asubuhi, star times walifungua vijana wakaanza kujisevia Tv na decoder zao, kuna jamaa mwingine alifungua kalibu na mataa, mwenyekiti wa wafanyabiasha akaagiza vijana zaidi ya 20., vijana hao wamekamatwa na polisi wako ndani.,
 
mkuu wa mkoa ametuma barua iliyoandikwa tarehe 27/12/2013 kuwa viongozi wamfuate ofisini kwake watu wamekataa wamesema yeye aje hapa.
na maazimio yametoka kuwa tutakaa hapa hadi muda wa kazi serekalini uishe na ujumbe umeenda kuwa tunamsubiria hapa na endapo hatakuja kesho asubuhi kila mtu aje na chai na lunchi tushinde hapa hadi kieleweke.
polisi wana randaranda hapa na magari yao ila hakuna anyetishika.
watu ni nyomi ya kutosha
 
Nchi ya rushwa inaendeshwa kirushwa rushwa tu,hawati slko huria ili wawaibie wafanya biashara.
 
hivi kwanini watu hatupendi kulipa kodi? then bavichwa wanakuja hapa jamvini wakisupport mgomo,sijui wanafikiria nn,tulipe kodi jamani maandeleo hayaji kutoka mbinguni
 
Mashine za EFD 800,000
leseni 200,000 kila mwaka
fire 100,000 kila mwaka
usafi 8,000 kila mwezi
Hizo ndio baadhi ya kero zinazolalamikiwa.
mwanasheria wa wafanyabiashara na uongozi wameenda kwa mkuu wa mkoa.
 
Nimepita mitaa ya Rwagasole hivi ndivyo maduka ya wafanyabiashara yalionekana yakiwa yamefungwa kupinga mashine ya TRA
 

Attachments

  • mwanza_n.jpg
    mwanza_n.jpg
    7.8 KB · Views: 467
Lakini mkuu mbona Laptop kila mtu ananunua anakojisikia mwenyewe kiroho safi, kwa nini EFD tukanunue kwenye maduka "Maalum"

Kuna sababu nyingi
  • Yawezekana system yenyewe ya TRA ina mashine zake special ambazo zinaweza kuwa intergrated nayo.
  • Yawezekana kwa ajili ya kucontrol uchakachuaji na kudhibiti standards za mashine.
  • Yawezekana zile mashine zina security ambayo inazuia kufuta local data ilizonazo ili kudhibiti ukwepaji wa kodi.
Na nyinginezo
 
Hata laptop kuna za laki nne mpya kabisa na za milioni tatu mpya kabisa na kwa sura zinafanana.

Lakini hakuna anayelazimishwa kununua laptop ya milioni tatu. Unaweza kuchagua upendayo. Kwa nini walazimishe kila mtu awe hiyo yao????!!! Hebu fikiria kila mtu alazimishwe kuwa na laptop ya milioni tatu!!!
 
Kuna sababu nyingi
  • Yawezekana system yenyewe ya TRA ina mashine zake special ambazo zinaweza kuwa intergrated nayo.
  • Yawezekana kwa ajili ya kucontrol uchakachuaji na kudhibiti standards za mashine.
  • Yawezekana zile mashine zina security ambayo inazuia kufuta local data ilizonazo ili kudhibiti ukwepaji wa kodi.
Na nyinginezo


Hakuna majibu ya jumla miaka hii,huwezi ingiza watu gharama kwa tofauti hiyo then useme kama hapo juu!!!!!!

Weka comparative advantage ya hizo na nyingine waweza eleweka kirahisi zaidi!!!!!
 
Back
Top Bottom