UPDATE: Mgomo waendelea Kariakoo kwa Siku ya 3, Wafanyabiashara wataka Mkutano wa Wazi na Majaliwa

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,618
1684230750549.png
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kufanya Mkutano wa Wazi na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo, hivi punde katika Viwanja vya Mnazi Mmoja

Wafanyabiashara hao ambao awali walipaswa kutoa wawakilishi wao kwenye kikao na Waziri Mkuu walikataa pendekezo hilo huku wakishinikiza uwepo wao wote ili kuleta tija ya maamuzi ya Mkutano huo

..................................................

Licha ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzungumza na wafanyabiashara katika soko la Kariakoo jana Mei 15, 2023 na kuahidi kuzipatia ufumbuzi changamoto zao, bado wafanyabiashara hao wamegomea agizo hilo Licha ya wachache kuonekana kutii agizo.

Ambapo Mwananchi asubuhi ya leo hadi saa 4.30 imeshuhudia maduka yakiwa yamefungwa na wafanyabiashara wakiwa wamesimama katika vikundi wakijadili hatma yao.

Jana wafanyabiashara hao walifunga maduka yao kwa saa 12 wakishinikiza kuonana na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye wamemtaja kwamba ndiye mtatuzi wa kero zao.

Miongoni mwa kero walizotaja wafanyabiashara hao ni kamatakamata inayofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Sheria mpya ya usajili wa stoo pamoja na kero zinginezo.

Jana Amos Makalla aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alifika sokoni hapo na kuwaomba wafanyabiashara kusitisha mgomo na wangeonana na Waziri Mkuu Majaliwa siku ya Alhamis jijini Dodoma lakini wafanyabiashara hao walidai wamechoshwa na maagizo ya kisiasa.

Kauli hiyo ilipingwa na Wafanyabiashara hao wakimtaka Waziri Majaliwa afike sokoni hapo na awasikilize, hata hivyo Majaliwa alifika sokoni hapo na kuwaomba wafanyabiashara kusitisha mgomo huku akiondoa kikosi kazi cha TRA pamoja na kukemea watumishi wanaodharau matamko ya viongozi.

"Hakuna kiongozi wa serikali anatakiwa kumdharau kiongozi wa juu, Rais na Makamu wa Rais wanaposimama kutoa maagizo sisi wa chini tunatekeleza mbiombio

TRA Rais amesema kodi ya miaka mitano nyuma achaneni nayo anzia mitano kwenda mbele wewe unamdai mfanyabiashara wa Kariakoo barua hiyo ni dharau ya hali ya juu.Natamani nimjue nani huyo"emesema.

Kauli hiyo iliambatana na ombi la Waziri Mkuu kuwataka wafanyabiashara hao kusitisha mgomo na kuitikiwa lakini leo hali ni tofauti kwani bado wafanyabiashara hao wanaendelea na mgomo.

Chanzo: Mwananchi
 
Mbona hao Wafanya biashara Jana walimkubalia Mhe. Waziri Mkuu na kuhaidi kusitisha mgomo wao.

Au ndiyo kusema Jana waliogopa yale mabinduki hivyo kujikuta wamekubali.

Au kuna nguvu nyuma yao inayowashinikiza kuendelea na Mgomo. Maana 2025 ni mwaka Keshokutwa tu 🤔
 
Wanajikuta wakina nani hao nao, wamemtaka Rais kamuagiza Waziri Mkuu wake na waliambiwa jumatano (kesho) watakaa kikao na Waziri Mkuu bado wanakaidi, acha waendelee kufunga siku wakiamua watafungua.
 
Wanajikuta wakina nani hao nao, wamemtaka Rais kamuagiza Waziri Mkuu wake na waliambiwa jumatano (kesho) watakaa kikao na Waziri Mkuu bado wanakaidi, acha waendelee kufunga siku wakiamua watafungua.
Waachie frem hizo kama vipi
 
Serikali ikamate viongozi wa mgomo na mechi itaisha wanaona Rais ni mpole Wana mchezea
 
Mbona hao Wafanya biashara Jana walimkubalia Mhe. Waziri Mkuu na kuhaidi kusitisha mgomo wao.

Au ndiyo kusema Jana waliogopa yale mabinduki hivyo kujikuta wamekubali.

Au kuna nguvu nyuma yao inayowashinikiza kuendelea na Mgomo. Maana 2025 ni mwaka Keshokutwa tu 🤔
Jana wengi waliokua pale kumsikiliza waziri mkuu ni Machinga washika remote hawakuepo kwa sehem kubwa
 
Mbona hao Wafanya biashara Jana walimkubalia Mhe. Waziri Mkuu na kuhaidi kusitisha mgomo wao.

Au ndiyo kusema Jana waliogopa yale mabinduki hivyo kujikuta wamekubali.

Au kuna nguvu nyuma yao inayowashinikiza kuendelea na Mgomo. Maana 2025 ni mwaka Keshokutwa tu
Jana wafanyabiashara hawakuwepo, bali wamachinga
 
Serikali ikamate viongozi wa mgomo na mechi itaisha wanaona Rais ni mpole Wana mchezea
Utawakamata wabunge wengi, mawaziri, wakuu wa idara, wahindi, wachina hawa ni fuata upepo, wachaga kidogo na wakinga wengi
 
Wanajikuta wakina nani hao nao, wamemtaka Rais kamuagiza Waziri Mkuu wake na waliambiwa jumatano (kesho) watakaa kikao na Waziri Mkuu bado wanakaidi, acha waendelee kufunga siku wakiamua watafungua.
Wanapo shusha mizigo bandarini wanalipa kodi wakija dukani wanalipa kodi mizigo yao ya sitoo ilipiwe kodi watu wa mkoani wakinunua wakija huku madukani kwao walipe kodi hapa hanae kamuliwa ni mlaji wa chini
Kibaya zaidi pesa hikisha kusanywa wajanja wachache wanakula kiulaini bora wasilipe kabisa
 
Q
Serikali ikamate viongozi wa mgomo na mechi itaisha wanaona Rais ni mpole Wana mchezea
Wangeanza kuwakamata wa kwenye ripoti ya CAG kwanza, watu wanalimbikiziwa marundo ya kodi kisha watu wachache wanaenda kuzitapanya
 
Jana wengi waliokua pale kumsikiliza waziri mkuu ni Machinga washika remote hawakuepo kwa sehem kubwa
Hili huenda ni sahihi, niliona sura zao wale jamaa nikahisi huenda PM alidanganywa ndiyo maana wakatoa Mkeka wa Kumhamisha Mkuu wa mKoa Usiku Mnene
 
Wananchi washajua porojo za wanasiHasa,kilichobaki Kuna mtu namuona(hasa kinara wa mgomo) anapelekwa mabwepande kung'olewa kuchraaa.
 
Serikali ikamate viongozi wa mgomo na mechi itaisha wanaona Rais ni mpole Wana mchezea
Ili iwalazimishe kuuza mali zao wenyewe? Au hizo bidhaa zinaozouzwa hapo Kariakoo ni mali ya seriakali kiasi kwamba inaweza kuwaamuru kuuza hata kama wao hawataki?
 
Waendeleze mgomo mpaka sheria za kukandamiza ndani ya ukusabyaji mapato zifanyiwe marekebisho bungeni. Huu uhuni wa kusajili stoo ni sheria mumiani mana mzigo unapita bandarini na unalipiwa ushuru wa foroza.

Sasa wanataka wanaonunua mizigo kwa waliotoa nje nao walipe kodi ya foroza?

Kwa viwanda vilivyopo nchini vyote vimesajiliwa na vinalipa kodi ya mauzo na vati kwa kila bidhaa. Wanataka na hao wanao nunua mizigo iliyokwisha lipiwa kodi ya mauzo nao walipe hiyo ya mauzo ilhali wanalipa kodi ya ushuru na vat pia?

Hii nchi ni ya ajabu sana, mzigo mmoja ule ule kulipiwa kodi zaidi ya tano wao wanaona ni kawaida tu maana hawana utu wa kuthamini mlaji ambae ni mtu wa mwisho.

Wengi wanaoathirika ni watu wa mwisho.

Mfano ukiangalia mafuta(petroli) kwa bei ya elfu 2800 kwa lita thani yake hadi yafike kwa muuzaji ni elfu 1 na mia nne hiyo nusu inayozidi ni kodi.

Hii ni sawa na kusema kodi za hii bidhaa ni kubwa kuliko thamani ya mzalishaji jumlisha na kusafirisha.
Tanzania kodi zipo juu kuliko thamani ya mzigo utokao kwa wazalishaji wa nje na ndani ya nchi.

Na kubwa kuliko yote ni hizi kodi kuhudumia kundi la watawala wachache maisha ya anasa na pia wizi wanaoufanya kuziiba hizi kodi kwa ubinafsi wa familia zao.

Angalia ripoti ya CAG jinsi hawa watawala walivyoziiba hizi kodi za walala hoi kuhalalisha maisha yao ya anasa.
 
Back
Top Bottom