Tabora: Mgomo wa Wafanyabiashara waondoka na Watumishi 3 wa TRA, DC awaripoti Makao Makuu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
1688409342981.png

Watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Tabora sasa kuondolewa mkoani humo kwa madai ya kulalamikiwa na wafanyabiashara wa Soko Kuu Tabora.

Wafanyabiashara hao wamefanya mgomo kutokana na madai ya mwenzao kuchukuliwa mali zake na watumishi wa TRA usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Julai 3, 2023 na kusababisha mgomo uliodumu siku nzima.

Akizungumza na wafanyabiashara hao, Mwakilishi wa mkuu wa Mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Dk Rashid Chuachua amewahakikishia wafanyabiashara kuwa watumishi waliowalalamikia hawatawaona tena mkoani hapo.

"Nawaomba kesho mfungue biashara zenu na watumishi hao hamtawaona tena mkoani kwetu hivyo msiwe na mashaka," amesema

Hata hivyo, Dk Chuachua amesema mfanyabiashara ambaye bidhaa zake zilichukuliwa usiku, hazikuwa zimelipiwa kodi kutoka nje ya nchi zilipoagizwa na kuagiza naye aendelee na biashara wakati taratibu zingine zikiendelea kuhusiana na mali zake.

Wakitoa malalamiko yao mbele ya Dk Chuachua, wafanyabiashara walielekeza kilio chao kwa watumishi wa TRA hususani hao watatu waliokuwa wakitajwa kwa jina moja moja.

Walimweleza, watumishi hao wamekuwa kero kwao wakidai walikuwa wakiomba rushwa na vitisho kwao.

Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Tabora, Ramadhan Kapela ametoa lawama kwa kitendo hicho na kuwa baadhi ya watumishi wachache wanaharibu sifa nzuri ya TRA.

Kutokana na uamuzi huo wa kuondokana na watumishi waliotuhumiwa, wafanyabiashara wameahidi kuendelea na biashara kesho kama kawaida.
 
Wametajwa kwa jina moja moja wakati ww mtoa habari umeshindwa kutaja hata jina moja lililotajwa? Hapo
 
Back
Top Bottom