Serikali Lazima itishe isichezewechezewe; Naafiki maneno yako, hapa chini naweka nukuu kutoka kwenye Biblia
kitabu cha1 cha Wafalme sura ya 2;
the days of David drew nigh that he should die; and he charged Solomon his son, saying,
... I go the way of all the earth: be thou strong therefore, and shew thyself a man;
Wito kwa JK, ni wakati wa kutenda sasa, usitake kuwapendeza madaktari kwa kuwa wanaua watu na
kuuonesha uma kuwa wewe ni dhaifu, fuata maneno ya Mfalme Daudi aliyomwambia Mfalme Suleiman
wakati alipomtawaza... "be thou strong therefore, and shew thyself a man;"
Sheria zipo wazi wataalamu wetu wamevunja sheria, umewabembeleza vya kutosha, chukua hatua...muda wa kutafakari umepita.
Najua maneno haya yatawaudhi sana mashabiki wa mgomo lakini hata kama Dr. Slaa akiwa rais hawezi vumilia hali hii
Tatizo siyo Mponda wala Lucy Nkya, bali tatizo lipo Utumishi na Hazina.
Tulianza na Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa wizara tukadhani tumetatua
tatizo kumbe wapi? Sasa tutawafukuza Mponda na Lucy Nkya, kisha tutadhani
tatizo ni Pinda, tutamuondoa na yeye lakini bado tatizo litakuwa palepale na
hatutakuwa tumetatua tatizo kwa kuwa serikali haina hata senti Hazina.
Mishahara ya kuwalipa wafanyakazi wake inakopa kwenye taasisi binafsi,
balozi zetu hazina pesa, wanaishi kwa kuganga njaa kwa kuwa tulichopitisha
kwenye bajeti yetu kilikuwa ni kuchumia tumbo, tuna madini lukuki lakini
yote tunayagawa kwa mikataba isiyo na tija, mibovu kuliko ya enzi za kina
Karl peters, tunasamehe kodi wakati tunategemea misaada ya wahisani!
Waziri Mponda au Lucy Nkya watafanya nini endapo hazina imekataa
kutoa fedha? Watafanya nini wakati Hawa Ghasia (Utumishi) ni tatizo
katika utumishi wa umma? Tafakari, chukua hatua...
ndiye anayesababisha yote haya?
we unaona ni akili kama hutushiki na vifo vya waliokuweka madarakani?yetu machoSerikali inampango kabambe wa kuonyesha makucha yake kwa madoctor na kuwa haitishiki na vifo vya raia wake na nilazima ishinde kwenye timbwili hili no matter what!
Hii ndio tafsiri niliyoipata baada ya tamko la waziri mkuu baada ya madaktari kutoa tamko takribani mwezi mmoja tangu wasitishe mgomo wakwanza ambao ulisababisha maafa makubwa baada ya kuvutana na PM wakutanie wapi mwisho PM akakubali kwenda kwenye venue ya madaktari.
Habari nilizozipokea sasa hivi kwa njia ya SMS kutoka kwa doctor mmoja pale Mhimbili zinasema hivi,nanukuu,"Hii ya sasa ni bab kubwa responce ni 100% MPAKA EMERGENCY,intern ndio wamemaliza kikao chao cha kupeana moyo na specialist ndio wanaanza Russian culture nw..together we can make it" mwisho wa kunukuu sms niliyoipokea.
My take; hivi serikali ina shindana na madaktari kwa ajili ya maslahi ya kisiasa? au inatakiwa kulinda afya za wananchi wake?
Maana kama mawaziri wamelalamikiwa na ni kweli wameshindwa kuwajibika kwa nini waendelee kuwepo hapo?na je inawezekanaje kupokea malalamiko ambayo kimsingi wao ndio wanalalamikiwa na kisha wakayafanyia kazi?
Nawasilisha wadau
Mbona hata Mawaziri na wabunge wanakula viapo? what is ur point here?Hivi hawa madaktari wetu huwa wanakula viapo?
sidhani kama madaktari wanaweza kugoma mara hii napata mashaka wacha tuone ila ni ngumu sana
wengi mnaojadili humu mnajadili kwa upana mdogo sana, lamsingi madfaktari waangalie mipaka ya majukumu yao, wao ni wataalamu, hawawezi kumpangia Raisi nani wa kumpa wizara na nani wa kumtoa, na Raisi akiwakubalia matwakwa yao ya kuwaondoa mawaziri atakuwa hajatumia busara, nawasihi madaktari wasilegee kwenye kudai maslahi yao na waboreshewe mazingira yao ya kazi, lakini wasijiingize kwenye mambo ya kisiasa wawaachie wanasiasa mambo yao.
Huu mgomo ni batili kisheria. Serikali ina haki ya kuwashtaki au iwafukuze kazi wale watakaoendelea kukaidi rai ya kuwataka warudi kazini.
For Dr's info: ma-dr wa kutosha kutoa huduma za dharura wako stand-by toka nchi rafiki. Liwalo na liwe, watakuja kuokoa roho mnazotaka zipotee. In the meantime serikali inajipanga kushughulikia kiburi chenu na kuwarudisha kwenye saizi yenu halisi.
Kipindi hiki lazima jambo litafanyika, hata kama ni kwa gharama. Lazima kukomesha hii jeuri ya madaktari kuvunja katiba na kutaka kuingilia madaraka ya Rais ya kuteua wasaidizi wake.