Sifa moja ya magaidi ni kutishia na ikiwezekana kutoa roho za binadamu wasio na hatia ili kutimiziwa malengo yao. Madaktari kuamua kugoma na roho za watu zipotee ili matakwa yao yatimizwe ni ugaidi. Kwa mfano, Magaidi wanaua mamia ya watu ili mwenzao mmoja atolewe gerezani na madaktari wetu wanataka kufanya hivyo hivyo kupoteza mamia ya maisha ya wagonjwa eti watu wawili tu waondolewe madarakani, hii inaingia akilini kweli?
Hao watu wataendelea kuwepo hapo wizarani milele? Kwani wameona hakuna njia nyingine zaidi ya mgomo? Haki inaweza kupiganiwa kwa muda mrefu sio lazima anufaike yule anayedai na kutaka mabadiliko ya papo kwa hapo.
Sasa hivi napata picha kila nikimuona daktari namuona kama gaidi, watadharauliwa na jamii kwani ni wananchi wachache sana ambao hawataathirika kama mgomo kama ukitokea.
Nawasilisha.