Maundumula
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 7,553
- 3,070
Poleni sana mlitumiwa.
Sasa nendeni kwenye nyumba za ibada mkatubu dhambi maana maisha yamepotea.
Sasa nendeni kwenye nyumba za ibada mkatubu dhambi maana maisha yamepotea.
Jamani madaktari kugoma ni haki yao. Ila cha maana wanatakiwa wawe na utu. Kusomea somo lolote kwa mtu mwenye akili anajua anafanya nini. Yafuatayo ni mambo yanaowakuta watu kwa kadri ya kazi yake.
1. Walimu, wanaishi katika mazingira magumu, hawana mishaara mizuri, wanaona kwamba hawathaminiwi, wameanza migomo siku nyingi kabla sijazaliwa
2. Wanasiasa, wanaishi mazingira mazuri, mishaara minono, wanaamini wanaeshimiwa, si wakweli hata kidogo. Sikuzote wanajiangalia wao tu
3. Wanajeshi, magereza, polisi, wanaishi mazingira mabaya kuliko wote, watiifu kwa yeyote aliyepo madarakani, mishaara sio mizuri, hawaheshimiki na wengi
4. Madaktari, mishahara sio mizuri, mazingira mabaya, wahaheshimika unapoumwa tu au ukiwa na mgonjwa, wanataka kuonekana wa maana kuliko mtu yeyote duniani kisa tu eti ukiugua yeye atakuokoa, wanatabia ya kugoma mara kwa mara
sasa wewe una mtoto wako anataka kusomea udktari unamruhusu vipi kwa historia hii. Kwanini asisomee wanasheria, biashara, uhasibu, sijawahi kusikia wamegoma.
kweli mama toto walikuwa wanatishia nyau, warudi tu wakaendelee kupokea vi rushwa vya 5000/- waasije kufa njaa!!
Kamati nyingine hii..."kamati kivuli"..hii ni kamati inayohitaji msamaha wa Rais mkuu.
Acha waombe msamaha maana hata Ulimboka alishaomba na akasamehewa.....
wamejiharibia sana hawa ndugu zetu, kosa namba moja ni pale mlipoamua kugawanyika wakati wa kugoma. Kosa namba mbili ni sasa mnapowageuka MAT na kuwatupia mpira wa lawama wakati utashi wa kugoma ulikua juu yenu.
Mwisho kabisa nasikitika kusema ya kwamba JK au serikali yake haitawasemehe kwa kuwa imeshagundua wapi mna kasoro, tafadhali jaribuni tu kutafuta career nyinginezo maana inaonesha hamkuwa na plan B.
Suala na ninyi kugoma ama kutokugoma ilipaswa mliongee vizuri hapo awali kwenye vikao vyenu vya ndani huku mkishauri na kushauriwa kutoka MAT.
sijawai kusiki... aliomba msamaha wa nini.??
Hili ni pigo kubwa sana kwa CHADEMA waliokuwa wanashadidia hii migomo.