Wanaendelea kumpiga chura teke, na pia ili CCM ianguke, ni lazima mambo na matendo kama haya yatokee na yaendelee kutokea.
No wonder wale wengine wamejidai kusitisha wito wa kumuita Lissu kwani ingekuwa ni too much kwa hizi taasisi zote kumsghulikia mtu mmoja, hivyo wakaona watuzuge eti aendelee na kampeni kumbe wameshamzuia.
Lissu hata angeitikia huo wito, sidhani kama maamuzi yangekuwa tofauti na haya waliyoyatoa.
Waendelee tu kufumbia macho matendo ya Mgombea yule huku wakishughulikia wengine wakidhani ndio wanambeba kumbe wanammaliza kwa kumuongezea Lissu kura za huruma plus kura za hasira kutoka kwa watu wasiopenda doublestand na uonevu.
Kumfungia Lissu kufanya kampeni, ni kumfanyia kampeni kubwa zaidi tena isiyo na gharama yoyote kwake ( it is a blessing in disguise).
Wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Tusubiri majibu/kauli ya Lissu.