Sijakuuliza kuhusiana na Sheria ya Takwimu.....anyway maelezo mazuri...
Good. Nadhani pia unamaanisha imetumika vibaya kwenye uchaguzi wa mwaka huu......
Kinachonikera ni kesi kama ile ya yule kijana injinia wa DIT (Ngonyani, nadhani) aliezusha kuwa Generali Mwamunyange kalishwa sumu. Hawa watu wa umma (public fiigures) kama Jenerali, Rais wetu na wengineo ni mali yetu, amana yetu, tegemeo letu. Wasipoonekana kwa muda (kwa mfano Magufuli apotee kwa wiki moja) watu tunajiuliza. Jukumu la hawa watumishi wetu ni kutujuza kuwa mambo poa, huyu hapa. Wasipofanya hivyo katika muda muafaka, tetesi, uvumi, ushambenga unaanza kutokea vijiweni. Kuwatia hatiani hawa watu si haki. Kama viongozi hawataki tujue walipo basi waache nyadhifa zao nasi tutawaacha. Nani anaejua Dr. Kikwete yupo wapi leo - hakuna, na watu hawajali kwa kuwa yeye ni raia mwenzetu wa kawaida sasa.
Lakini kitu kibaya zaidi kuhusiana na hii sheria ya mtandao ni kuwa watu hawajui mipaka ni ipi. Unaweza kubarizi tu kijiweni na kubwabwaja uongo na utani, jioni yake unajikuta unanyea ndoo Segerea. Kwa hili watu wanaogopa kusema chochote kile. Hiki ni kitu kibaya sana kwa uhuru wa wananchi. Nilifikiri tulikwisha toka katika hali kama hizi. Siku za nyuma wengine sisi tuliogopa hata kuteta na marafiki zetu mambo yanayotukera tukihofia kukamatwa. Tusirudi tena huko jamani.
Sasa sijui wakati wa uchaguzi usalama wa taifa walikuwa na taarifa gani zilizoletea kuwakamata watu. Lakini sidhani walihitaji hii sheria ya mtandao kufanya kazi zao. Mahakama wanafuata tu sheria ilioko vitabuni lakini ni jukumu la bunge, ofisi ya raisi, na sisi wananchi kwa ujumla wetu kushinikiza sheria hii iangaliwe upya.
Nina wasiwasi kama ulifuatilia BMK...
Hivi huwa unafuatilia Bunge, maana kila mtu anajua kuwa wabunge wa Ukawa ndiyo wanaofanya kazi...hata Spika mstaafu A. Makinda anatambua hilo......
Kabla hujafikiria kuhusu matangazo ya bunge kutooneshwa kwenye TV, ungejiuliza ni kwanini yalianza kuoneshwa kwenye TV.......usiwe tu mropokaji.....
Nijuacho mimi ni kuwa UKAWA dropped the ball. Pick it up na mnyooshe mambo. Tusitafute mchawi katika bunge la 10 au BMK.
Kwahiyo wewe unatoa ushauri kwa wabunge wa upinzani tu....wabunge wa CCM huwezi kuwashauri?.....
Bunge zima linafanya kazi ya kushauri serikali, kutunga sheria na kuwakilisha wananchi.....sio wapinzani tu....
CCM wasipokuwa na nia ya dhati ya kuleta katiba mpya, jitihada za wapinzani haziwezi kufanikiwa maana hawafanyi hiyo kazi peke yao....mbona huelewi kitu rahisi hivi
Unajua kwanini 'katiba pendekezwa' ilipotelea njiani?......
Wabunge wa CCM wameridhika na katiba pendekezwa. Ninachokisikia toka kwako ni CCM hiki, CCM kile, CCM wanatufanya hivi au vile. JD man, stop whining. Fanyeni kazi. Upinzani sio lelemama.