yero, kama watu wawili wanagombana, kila utakaemuuliza atakwambia yeye ndio mwenye haki. Kinachohitajika ni msuluhishaji asiependelea upande wowote ule awasaidia kutatua ugonvi wao.
Mimi naelewa sana msimamo wa CUF ambao ndio msimamo wako. Sasa Jecha mwenye mamlaka ya kutangaza katia ngumu, huoni ni muhimu tupate msuluhishi. Ukinikemea mimi kuwa CUF wako sahihi haisaidii, ni sawa na kuuchapa mzoga wa mnyama ukitegemea utaamka utembee.
Umesema vizuri kuwa Jecha ana mamlaka ya kutangaza, na Je anayo mamlaka ya kufuta uchaguzi?yero, kama watu wawili wanagombana, kila utakaemuuliza atakwambia yeye ndio mwenye haki. Kinachohitajika ni msuluhishaji asiependelea upande wowote ule awasaidia kutatua ugonvi wao.
Mimi naelewa sana msimamo wa CUF ambao ndio msimamo wako. Sasa Jecha mwenye mamlaka ya kutangaza katia ngumu, huoni ni muhimu tupate msuluhishi. Ukinikemea mimi kuwa CUF wako sahihi haisaidii, ni sawa na kuuchapa mzoga wa mnyama ukitegemea utaamka utembee.
Swali linaweza kuwa jibu la swali. Tafakari.Classic yero. Unajibu swali kwa swali. Well, nimekuuliza mimi kwanza - Jibu.
Ni kweli sijui mashitaka yao wale vijana.
Lakini kama takwimu walizozitoa au tamshi zilizosemwa zilikuwa na athari kwa mtu, watu, taasisi, au shirika, hii ni libel case, na kuna libel laws tayari vitabuni. Sidhani nahitaji kukueleza hiki kitu JD. Kwa hiyo kumkamata mtu kwa kutoa tamshi la uongo mtandaoni huhitaji hii sheria ya mtandao.
Mfano: Kama mimi nikiandika hapa JF kuwa JD ni mbilikimo ilhali JD ana urefu wa futi sita na zaidi, huhitaji sheria ya mtandao kunishughulikia. Ukiweza kuonesha kuwa tamko lango hilo limekuathiri kibiashara, kimaslahi au mapato unaweza kuniburuza mahakamani. Huhitaji sheria ya mtandao.
Hunielewi, naongelea mchakato mzima wa katiba mpya, sio tu kuleta mswada bungeni......Sasa mbona unanipiga maswali tu badala ya kunipa ilmu.
Nimependa hiyo metaphor ya walozi kurudi kuwanga kwenye bunge la 11. Lakini narudia palepale, hili ni jukumu la wabunge wa UKAWA. Wabunge ndio wanaoingia mjengoni, sisi wengine tutapiga kelele tu huku nje. Pia wabunge wa UKAWA wanaweza kuwashawishi wananchi wengi walishinikize bunge na nchi turudie mchakato wa katiba.
Unajua katiba huwa zinakuja kwa nadra sana. Tukipitisha katiba mpya sasa inaweza kuchukua hata miaka 100 kuweza kuirekebisha tena, hasa katika hali hii tete ya muungano wetu. Sioni sababu ya kuiharakisha ile katiba pendekezwa.
Turudie mchakato, lakini tuanze mapema ili katiba mpya iweze kutumika 2020. Lazima tuipe katiba mpya kipaumbele na chachu ya huu mchakato ni wabunge wa upinzani. Wabunge wasijipare tu ili waonekane kwenye runinga. Ningekuwa na uwezo wabunge wote wa kike wangevaa ma-burka (ficha uso wote), na wanaume wavae kininja (nadhani Mh. Kangi Lugora angefurahia sana) ili sura zao zisionekane kwenye runinga, wafanye kazi tu.
Sidhani kama umenielewa JD. Wabunge wa CCM hawana haja ya kurudia (sina uhakika) huu mchakato kwa sababu walikwisha ufanya. Waliokuwa hawakuridhika ni UKAWA, kwa hiyo wao ndio wawe chachu ya huu mchakato mpya.
Well, akili, busara na hekima sie wengine zimetupitia kushoto na ndio maana nawasubiri vizito wanaojadili.
Ni fedheha kwa mtu mzima kama ww kuwa mnafiki,vyama vyote kwenye uchaguzi havijapeleka malalamiko na wasimamizi wote wamekiri uchaguzi ni huru na wa haki,sasa wewe unapo sema kuna ugomvi ni nani na na nani wanaogombana?jecha mamlaka yake ni kutangaza matokeo na sio kufuta uchaguzi.
Umesema vizuri kuwa Jecha ana mamlaka ya kutangaza, na Je anayo mamlaka ya kufuta uchaguzi?
Kwa kuwa Jecha mamlaka yake ni kutangaza matokeo na yeye amesema hawezi kutangaza kwa ajili ya madudu yaliyotokea basi ni dhahiri pana mgogoro hapo. Hakuna mtu mwengine wa kutangaza bali ZEC (Jecha). Unakumbuka Maalim alitangaza matokeo lakini ikashindikana kumuapisha? Ndio maana nasema tusubiri matokeo ya haya majadiliano.
Tamko langu mimi, pamoja na utu uzima wangu, halitaleta suluhisho hapa - na wala sio unafiki. Kwa hili Bobwe sina fedheha nalo.
We kila kitu hujui, kama hujui usiwe unabwabwaja ovyo,Sijui sheria inasemaje kuhusu kufuta uchaguzi lakini kama hatangazi matokeo huoni tunahitaji njia ya kupata maafikiano hapo?
Au tupate mamlaka/msuluhishi atakaesema kuwa Jecha amechemsha ili matokeo yatangazwe, au waseme ni haki Jecha ulichoamua ili uchaguzi urudiwe.
Ushasema hujui mashtaka ya watu hao. Hayo maelezo mengine ni irrelevant.......
Hunielewi, naongelea mchakato mzima wa katiba mpya, sio tu kuleta mswada bungeni......
RED: Wabunge wa CCM walio wengi wanahusika katika upitishwaji wake, maana hiyo sio Katiba ya UKAWA
BLUE: Tatizo sio kushawishi wananchi maana hiyo ni hatua ya mwisho....wabunge wa CCM watakubali kupitisha katiba isiyobeba maslahi ya chama chao?
LIME: Zinakuja kutoka wapi?
VIOLET: Unafaham historia ya Katiba ya JMT? imerekebishwa mara ngapi ndani ya miaka mingapi?
GOLD: Mchakato wa katiba hautakiwi kuwa mchakato wa kichama......tukiendekeza hilo basi tutapitisha katiba inayobeba maslahi ya CCM wala sio ya Taifa......Nataka nione wabunge wa CCM wanatema point sio wanamwaga mapovu bungeni......
TEAL: Wabunge wote hawatakiwi kuvaa mavazi yao kwa ajili ya kumfurahisha mtu moja
VIOLET: Siku nyingine uwe na uhakika kwanza.....
RED: Tatizo hujui kwanini UKAWA hawakuridhika na huo mchakato......
BLUE: Tatizo sio kuwa chachu tatizo lipo kwenye upitishwaji wa katiba yenye maslahi ya Taifa....wabunge wengi wa CCM hawaelewi chochote kuhusu maslahi ya Taifa......maslahi ya chama ndio kila kitu kwao.....sheria ya makosa ya mtandao, takwimu, gesi na mafuta ni mifano ya karibuni ya umbumbumbu wao......ndio maana nasisitiza wabadilike.....
We kila kitu hujui, kama hujui usiwe unabwabwaja ovyo,
Hujui kama Jecha kakosea au hajakosea, hilo mpaka msuluhishi ndo akwambie, we kweli kilaza wa mwisho
Hao unawawaita vizito wakikubalina kwamba ZEC iendelee kutangaza matokeo ya majimbo 21 yaliyobaki ili kuheshimu sauti ya wapiga kura.....utakubali kwamba wapo Fair? YES or NO
Nikikuelewa vizuri, ina maana sasa hivi huelewi kama kuna kosa limetokea kwenye uchaguzi wa ZNZ?.......na kwamba hayo unayoita majadiliano yakiisha ndipo utaelewa kama kuna makosa ama la?.....I don't know about fairness lakini kama kutokana na haya majadiliano wakiamua watangaze matokeo yote mimi nitaridhika.
Nikikuelewa vizuri, ina maana sasa hivi huelewi kama kuna kosa limetokea kwenye uchaguzi wa ZNZ?.......na kwamba hayo unayoita majadiliano yakiisha ndipo utaelewa kama kuna makosa ama la?.....
I am not going to let you take me through these childish circular arguments with you again JD. Sina muda wa kucheezea. When you grow up, come back for a sober discourse.
JD, mimi sio mwana sheria, sijabobea katika katiba ya Zanzibar. Mimi ni mwananchi mwengine wa kawaida tu nikifuatilia hili sakata. Ukiniuliza nani amekosa na nani yuko sahihi unanionea.
YES, majadiliano yakiisha ndio nitajua ukweli uko wapi.
"Ignorantia juris non excusat" (ignorance of the law is no excuse).......
Haimaanishi wote tuwe tumebobea kwenye sheria, ni ngumu kukariri sheria zote kichwani hata wanasheria hawawezi.....ila huwezi kusema unaonewa kwa sababu hujui sheria.....
Ingekuwa rahisi sana kwa watu kuvunja mikataba, kubaka, kuuza madawa ya kulevya n.k.......Pengine inaweza kuwa rahisi kwa Jecha kutoa kisingizio kuwa hakujua sheria inasemaje kuhusiana na yeye kufuta uchaguzi....
Kama ukweli wako unategemea matokeo ya majadiliano kumbuka tu kwamba pale hawapo mahakamani......
team gavana.naona mnashindwa tetea haki yenu-u wapi umoja wenu?