Ni vyema ukasahihisha kauli yako.
Siyo Tume ya uchaguzi ZEC iliyofuta uchaguzi, bali ni mtu mmoja anayeitwa Jecha 'alijikurupukia' na kurikodiwa kwenye mkanda ambao ulisomwa ZBC akidai kuufuta uchaguzi huo, akisema ni kutokana na mamlaka aliyonayo, bila kuquote Ibara yoyote ndani ya Katiba ya Zsnzibar ya mwaka 1984 inayompa mamlaka hayo. Vile vile alishindwa kuquote kifungu chochote cha sheria ndani ya Zanzibar Electoral Commission Act, kinachompa mamlaka hayo ya kuufuta uchaguzi huo.
Nimesema siyo ZEC iliyofuta uchaguzi huo kwa kuwa tunapotamka chombo kinachoitwa ZEC tunamaanisha composition ya wajumbe wanaounda Tume hiyo ya uchaguzi ambao ni Mwenyekiti wa Tume na Makamu wake pamoja na wajumbe wengine ambao ni makamishina wa Tume hiyo.
Kutokana na watawala wa Zanzibar kutambua kuwa tamko la Jecha ambalo lilitokana na shinikizo lao kujua ni batili, ndiyo maana tokea atamke tamko lake hilo 'wamemficha' mahali pasipojulikana ili wamwepushe na hasira za wananchi ambao walitumia haki yao ya kidemokrasia ya kumchagua kiongozi wanayemtaka halafu akajitokeza mtu huyo anayeitwa Jecha na kuwapora haki yao hiyo!
I stand corrected. Asante kwa sahihisho lako.
Kwani unafikiri mimi namtetea Jecha? La.
Sasa hivi Maalim, Dr. Shein, maraisi wa zamani (wote CCM) wanakutana au walishakutana chini ya ushauri wa UN, EU, AU, kutatua hili tatizo.
Ningefurahi kama katika hii timu ya usuluhishi kungekuwa na wataalam wachache wa sheria wa CUF (kama wapambe wa Maalim).
Basi tuwe na subira. Tuwape muda tuone kama watakuja na suluhisho. Tusikimbilie ikulu ya Marekani kwanza.