Mfumuko wa Bei wa Taifa Washuka hadi Asilimia 3.4

Halafu bado tunaimbiwa ngonjera na wana Pinga-Pinga Stars, maisha ni magumu. SMH
Umesoma vilivyopungua au?

Akifafanua amesema kuwa baadhi ya bidhaa zilizopungua bei kwa mwezi Septemba ni mafuta ya taa asilimia 1.0, Petroli asilimia 3.3 ,majiko ya gesi asilimia 1.5, dawa za kuulia wadudu nyumbani asilimia 2.2 na mafuta ya nywele asilimia 1.3.

Kati ya hivyo wewe kipi kinakuhusu kama upo kijijini? Wangapi wanatumia mafuta ya nywele, majiko ya gas na dawa za kuulia wadudu majumbani?
 
Haya mambo mimi huwa naona maruweruwe tu, huwa siyaelewi kabisa, sukari huku 2500, mfuko wa saruji 20000/=Mche wa sabuni 2600/= ...wengine mafuta ya nywele tunayasikia kwenye vyombo vya habri, pakiti ya chumvi 800/= lita ya mafuta ya kupika 5000/= sasa haya mambo yamekaaje wadau maana utaskia mara bei imeshukaaaa. Lakini mimi huu ni mwaka wa nne mfululizo nanunua mfuko wa saruji 20000/ ....Wakati mwingine naamini Tanzania ni ya wachache tu.
 
Unafikiri 1.7T kwa mwezi imetoka wapi?
 
Hii ni taarifa muhimu sana, uchumi wa Magufuli has started doing good, then better and finally best!.

P
Mkuu Pascal kilchopungua bei ni bidhaa zisizo za vyakula. Ukiangalia bidhaa za vyakula zimepanda bei sana na ndizo zenye athari ya moja kwa moja kwa mwananchi.
Kwa hiyo mimi mwanachi wa kawaida ukiniambia mfumuko wa bei umeshuka nashindwa hata kushangaa kwa sababu nikishangaa nitakuwa nimeelewa!!
 
Ukiangalia kwa makini taarifa hiyo itaonesha bidhaa muhimu za chakula na vinywaji (ambapo uma mkubwa unatumia) ziliongezeka bei. Kwa makusudi kuna watu wanakwepa kuzungumzia hili na badala yake kuzungumzia kupungua kwa mfumuko wa bei katika bidhaa za petroli (ambayo kimsingi inatokana na bei katika soko la dunia wakati importation ikifanyika), dawa kuulia wadudu na mafuta ya nywele.

Kwa hakika tunapima mfumuko wa bei katika mambo yasiyo na uhitaji mkubwa katika maisha ya umma mkubwa.
 
Mi hata sielewi mfumuko wa bei au mshonoko wa bei ndo nini

Maana sijawahi nunua soda 400 tangu nianze skia hayo ma msemo

sijawahi nunua kilo ya mchele 500 wala sukari kilo Buku

Bei za vitu navyonunua ni zile zile ila upande huu ntaskia mfumuko wa bei

sijui mteremko sijui nini..msemege hizo bei n za vitu gani basi
 
Kweli umeshuka, kg moja ya unga wa sembe kutoka efu moja na sasa ni tsh 1400,
 
Kuna watu hata wakisikia mfumuko wa bei ni 1% watashangilia bila kujua athari zake tuache siasa kwenye kwenye mambo muhimu kama haya.
 
Kuna watu hata wakisikia mfumuko wa bei ni 1% watashangilia bila kujua athari zake tuache siasa kwenye kwenye mambo muhimu kama haya.

Hebu fafanua sasa hiyo report inauhalisia wowote ndugu?

Toa mifano sahihi na maeneo
 


Hakuna kitu kinapaisha mfumuko wa bei kama mafuta, kuanzia mafuta ya taa, petroli dizeli, mafuta ya kuendesha mashine viwandani mpaka mafuta ya uzalishaji umeme. Hayo yote yanamgusa hata akiyekuwa kijijini ambaye hajawai kukajaga mguu mjini. Ukitaka maisha yawe magumu kweli kweli, ongeza bei ya mafuta.

Cha msingi, ni kuangalia hiyo ripoti kwa kina na kuilinganisha na takwimu za mwaka jana, na pia ni kujua kwanini bei zinashuka. Uzalishaji wa umeme wa kutumia gesi asilia umeongezeka kuliko tulivyokuwa tunaagiza mafuta kutoka nje, ununuzi wa bidhaa kutoka nje kiholela umeshuka, ufanisi wa viwanda vya ndani unaimarika, na hata kupelekwa watu nje Kwa matibabu pia kumepungua. Bila kusahau tumepata uzalishaji wa chakula cha kutosha mpaka tunauza nje ya nchi.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi maana wengine tunaishi porini kusikokuwa na radio wala tv hivyo hatujui kitokeacho makwetu.
 
Congrats kwa serikal, moja ya target ya mwaka wa fedha 2019/2020 ilikua kumaintain infation rate katika single digit kati ya 3.0 had 4.5 ..na wamefanikiwa
Rejea awamu iliyopita. Infration rate unajua ilichezea rate gani?
 
Mfumuko wa bei hata ukiwa 0. Kwa nchi ya TZ kiuchumi una negative impact. Hii ni sababu asilimia kubwa ya vyakula vinazalishwa humu humu. Wakulima ndyo wanaumia huku walaji wakifurahia. Ila kiuchumi maana yake ni mzunguko mdogo wa pesa sababu nchi yetu bado inategemea kilimo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…