Mwanzi1
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 5,999
- 4,591
Napata picha hapo ulipo una aje ajenda binafsi. Anyway, acha tuende na mdindo uliyouzowea na kuuelewa kirahisi (swali kwa swali).Umejibu swali gani kati ya hayo mawili na nusu?
Nimekuuliza maswali hayo si kwa maana eti sijui au kwa lengo la kuwavunjia heshima NBS. Lakini mbona maswali hayo sijawauliza NBS! Nimekuuliza wewe uliyetoa hoja kwamba bei ya mafuta inaweza kuathiri mfumuko wa bei za bidhaa zingine ili tujiridhishe ukweli huo kutokana na ripoti ya NBS. Labda nikuongeze swali lingine.
Je, unaweza kuthibitisha ulichokisema kwa kutumia "holistic report" ya NBS? Haya twende kazi!
Je nyanya zikivunwa Lushoto au Mahenge, zinapelekwa sokoni kwa kubebwa kichwani au wanapakia kwenye malori mambayo yanatumia mafuta? Na je? mafuta yakipanda bei hayata athiri bei ya nyanya kwa mteja?
Mahindi ya Songea je? yakifika kiwandani ni mashine zinano tumia umeme na dizeli hutumika kuyakobia na kusaga au bado wanatumia kinu na mwichi Kwa mtazamo wako bei ya mafuta ya uzalishaji umeme haiwezi kuathiri kwenye bei ya unga?
Fikiria nguo za mitumba zilizo bandarini DSM, zitamfikiaje muuzaji aliyeko Bukoba mjini au vijijini? Unafikri gharama za usafirishaji zikipanda haziwezi kubadiki bei anayouza mitumba?
Uchumi wa dunia unategemea mafuta ili kujuendesha Kwa 40% hakuna nchini inaweza kuwa Sawa kama bei ya mafuta itatetereka
Posti mbili za nyuma, nimesema ukiona bei ya mafuta inapungua, inaweza kuchukuwa muda (mwezi moja au mmoja na nusu) kuanza kuona za vitu zinashuka au kubaki pale pale kutoka na wafanyabiasha wanavyojipangia faida.