Mfumuko wa Bei wa Taifa Washuka hadi Asilimia 3.4

SNAP J

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Messages
5,210
Points
2,000

SNAP J

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2013
5,210 2,000
Umesoma vilivyopungua au?

Akifafanua amesema kuwa baadhi ya bidhaa zilizopungua bei kwa mwezi Septemba ni mafuta ya taa asilimia 1.0, Petroli asilimia 3.3 ,majiko ya gesi asilimia 1.5, dawa za kuulia wadudu nyumbani asilimia 2.2 na mafuta ya nywele asilimia 1.3.

Kati ya hivyo wewe kipi kinakuhusu kama upo kijijini? Wangapi wanatumia mafuta ya nywele, majiko ya gas na dawa za kuulia wadudu majumbani?
Tikisema mambumbumbu ndio mtaji wa ccm tunaambiwa twatukana.
 
Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
47,561
Points
2,000

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
47,561 2,000
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi septemba, 2019 umepungua hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Hayo yamesemwa na Kaimu mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja wakati akitangaza mfumuko wa bei jana Jijini Dodoma.

“Kushuka kwa mfumuko wa bei kunatokana na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwezi Septemba 2019 ikilinganishwa na bei za kipindi cha Septemba,2018”. Alisisitiza Bi. Minja.

Akifafanua amesema kuwa baadhi ya bidhaa zilizopungua bei kwa mwezi Septemba ni mafuta ya taa asilimia 1.0, Petroli asilimia 3.3 ,majiko ya gesi asilimia 1.5, dawa za kuulia wadudu nyumbani asilimia 2.2 na mafuta ya nywele asilimia 1.3.

Aliongeza kuwa mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Akizungumzia nchi za Afrika Mashariki Bi. Minja amesema kuwa mfumuko wa Bei nchini Kenya kwa mwezi Septemba umepungua hadi asilimia 3.83 kutoka 5.00 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.
Kwa upande wa nchi ya Uganda, mfumuko wa Bei kwa mwaka unaoishia mwezi Septemba 2019 umepungua hadi asilimia 1.9 kutoka asilimia 2.1 kwa mwaka unaoishia mwezi Agosti, 2019.
Mbona nimenunua unga kilo moja kwa 1,500.

Jana tu.

Au mimi ndio sielewi kitu
 
SNAP J

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Messages
5,210
Points
2,000

SNAP J

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2013
5,210 2,000
Ukiangalia kwa makini taarifa hiyo itaonesha bidhaa muhimu za chakula na vinywaji (ambapo uma mkubwa unatumia) ziliongezeka bei. Kwa makusudi kuna watu wanakwepa kuzungumzia hili na badala yake kuzungumzia kupungua kwa mfumuko wa bei katika bidhaa za petroli (ambayo kimsingi inatokana na bei katika soko la dunia wakati importation ikifanyika), dawa kuulia wadudu na mafuta ya nywele.

Kwa hakika tunapima mfumuko wa bei katika mambo yasiyo na uhitaji mkubwa katika maisha ya umma mkubwa.
Hakuna mwenye ubavu wa kusoma "the other side of that report" ambayo itakuwa imeweka bayana kuhusu mfumuko wa bei ktk bidhaa muhimu za chakula na vinywaji.
 
niah

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Messages
6,191
Points
2,000

niah

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2015
6,191 2,000
Tikisema mambumbumbu ndio mtaji wa ccm tunaambiwa twatukana.
Tusubiri kalne nyingine au wazaliwe wengine waliokula vyakula tofauti na tunavyowapa hawa watoto. Nyerere anatuona! Alitusomesha bure, tukala ugali, wali, nyama, samaki, maharagwe na maziwa bure kila siku including mikate pale mwanza ililetwa na mgiriki mmoja nimesahau jina. Sasa hao hao tuliokula nao hivi vyakula, ni mawaziri na niwenzanga lakini wanadiriki kusema uchumi ni juu!! Tuligawiwa modes, toilet papers, chupi, kalamu, madaftari, kila kitu niseme bure leo hao hao wanakuja na kusema kila kitu bure wakati watoto wanatoka kilomita 20 wakati sisi tulikuwa boarding hata wa day schools walikuwa wanahifadhiwa na rafiki wa wazazi na walipata kila kitu. Uchumi upo wapi. Nyerere rudi utueleze ilikuwaje tukafikia hapa tulipo? Hukuwahi fukuza wala kemea mtu mikutanoni ingawa uliweka ndani watu . je ni sawa hiyo? Haaaaaata.
 
X-bar

Senior Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
127
Points
250

X-bar

Senior Member
Joined Mar 20, 2019
127 250
Mimi sielewi hizi data wanazipatia wapi. Maana kwa sasa Dar vyakula na bidhaa nyingine muhimu vimepanda bei. Mfano mahindi mwezi wa 8 kurudi chini yalikuwa yanauzwa 80,000 kwa gunia la kilo 100 inamaana 800 kilo Moja,lakini tangu Mwezi wa Tisa bei imepanda mpaka kilo moja ya mahindi kufikia 1300,maharage na mchele nayo vivyo hivyo.
Ukweli ni kwamba unachokifahamu wewe kuhusu kupanda kwa bei ya vitu ulivyovitaja (vyakula) kimetajwa kwenye ripoti. Rudia kusoma na utaona.

Kuna "tactic" imetumika "kuzuga" taarifa mbaya katika ripoti ambayo bilashaka imekubabaisha.

Wametanguliza taarifa ya kupungua kwa bei ya bidhaa zisizo za lazima katika maisha (petroli, gesi, mafuta ya nywele na dawa ya rungu), kisha wakamalizia na taarifa mbaya ya kupanda kwa bei za bidhaa za lazima (vyakula na vinywaji baridi).
 
X-bar

Senior Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
127
Points
250

X-bar

Senior Member
Joined Mar 20, 2019
127 250
Hakuna kitu kinapaisha mfumuko wa bei kama mafuta, kuanzia mafuta ya taa, petroli dizeli, mafuta ya kuendesha mashine viwandani mpaka mafuta ya uzalishaji umeme. Hayo yote yanamgusa hata akiyekuwa kijijini ambaye hajawai kukajaga mguu mjini. Ukitaka maisha yawe magumu kweli kweli, ongeza bei ya mafuta.

Cha msingi, ni kuangalia hiyo ripoti kwa kina na kuilinganisha na takwimu za mwaka jana, na pia ni kujua kwanini bei zinashuka. Uzalishaji wa umeme wa kutumia gesi asilia umeongezeka kuliko tulivyokuwa tunaagiza mafuta kutoka nje, ununuzi wa bidhaa kutoka nje kiholela umeshuka, ufanisi wa viwanda vya ndani unaimarika, na hata kupelekwa watu nje Kwa matibabu pia kumepungua. Bila kusahau tumepata uzalishaji wa chakula cha kutosha mpaka tunauza nje ya nchi.

Unajaribu kuonesha kuwa bei ya mafuta ya mitambo huathiri moja kwa moja bei za bidhaa zingine. Lakini taarifa iliyotolewa haisapoti madai yako kwa maana bei ya mafuta iko chini na bado bei za vyakula na vinyaji baridi ziko juu. Je, tupinge "fact" yako au ripoti hii?
 
Mwanzi1

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2016
Messages
5,246
Points
2,000

Mwanzi1

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2016
5,246 2,000

Unashidwaje kuelewa kama gharama za uzalishaji kwenye kiwanda cha Bakhresa au MO ikiongezeka kutokana na bei ya mafuta kupanda inaweza kuathiri bei ya bidhaa zao masokoni? hili ni gumu kuelewa?

Bei ya mafuta ikishuka leo, haimaanishi kesho bei ya mahindi au mchele nayo itashuka, inachukuwa muda kwa mlaji kupata unafuu wa bei. Na swala la vitu kama vinwaji badiri, vingine vinatengenezwa na malighafi ya kutoka nje, mfano sukari nzito ya viwandani nk.
 
Sijashindwa kuelewa kama unavyodhani. Nimejaribu kuoanisha ukweli uliousema kuhusu athari ya bei ya mafuta kwa bidhaa zingine na kile tunachokiona kwenye taarifa lakini nashangaa haviendani. Yaani taarifa hii ya hali ya mfuko wa bei inakinzana na fact uliyoisema.

Je, unajua sifa ya kitu "fact"? Fact ni ukweli na ukweli huwa haubadiliki kutegemea na mabadiliko ya wakati wala mahali. Mathalani , tukisema jua huchomoza mashariki na kuzama magharibi ni fact (ukweli/uhalisi) ambao haubadiliki kutegemea na mahali au wakati.

Sasa inapotokea tunachoambiwa, kwa mfano, hii taarifa ya mfumuko wa bei, haiendani na ukweli/uhalisia (fact) tunayoijua, maana yake hiyo taarifa ni ya uwongo! Kwahiyo jibu la swali nililokuuliza kwamba tupinge hoja yako au taarifa, chakupingwa hapo ni taarifa na wewe uko sahihi kwamaana fact haipingwi. Umeelewa?
 
Sasa fact unayonifundusha hapa, mbona hukuuweka kutuonyesha kama bei ya mafuta haihusiani moja Kwa moja na bei ya nyaya sokoni? Kama mafuta bei ukiwa chini, nyanya pia bei itakuwa chini lakini inategemea na bei ya mafuta imekuwa chini Kwa kipindi cha muda gani. Huwezi kushusha bei ya mafuta leo na nyanya ikashuka bei kesho. Hiyo ndio FACT.
 
X-bar

Senior Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
127
Points
250

X-bar

Senior Member
Joined Mar 20, 2019
127 250
Sasa fact unayonifundusha hapa, mbona hukuuweka kutuonyesha kama bei ya mafuta haihusiani moja Kwa moja na bei ya nyaya sokoni? Kama mafuta bei ukiwa chini, nyanya pia bei itakuwa chini lakini inategemea na bei ya mafuta imekuwa chini Kwa kipindi cha muda gani. Huwezi kushusha bei ya mafuta leo na nyanya ikashuka bei kesho. Hiyo ndio FACT.
Unaleta ligi sasa. Labda nikuulize maswali ndo utanielewa.

1. Je, unadhani NBS wanatambua uhusiano kati ya bei ya mafuta na bei za bidhaa zingine?
2. Je, ripoti hii ya NBS inataja ni kitu/vitu gani vimechangia kushuka kwa bei ya mafuta na kupanda kwa bei ya vyakula na vinywaji baridi? Je, kwa akili yako, walipasa watuambie au la?

Ukiweza kunibu utakuwa umenielewa. Haya twende kazi!
 
Mwanzi1

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2016
Messages
5,246
Points
2,000

Mwanzi1

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2016
5,246 2,000
Unaleta ligi sasa. Labda nikuulize maswali ndo utanielewa.

1. Je, unadhani NBS wanatambua uhusiano kati ya bei ya mafuta na bei za bidhaa zingine?
2. Je, ripoti hii ya NBS inataja ni kitu/vitu gani vimechangia kushuka kwa bei ya mafuta na kupanda kwa bei ya vyakula na vinywaji baridi? Je, kwa akili yako, walipasa watuambie au la?

Ukiweza kunibu utakuwa umenielewa. Haya twende kazi!
Haya ndio matatizo ya kujiingiza kwenye mada bila ya kuwa na ueleo wa kutosha.

NBS inamawakala nchi nzima na wao ndio wenye mamlaka "Kisheria" kukusanya taarifa zinazo husu idadi ya watu na matumizi yao kwa niaba ya serikali. Wewe unaamua kuwavunjia sheshima na kuuliza eti wanajuwa mahusiano ya bei ya mafuta na bei ya vyakula. Na waalamu wote walio nao hilo ndio swali la kuuliza, Don't be that naïve.

NBS wakitoa taarifa, wanaitoa Kwa ufupi na kwa lugha nyepesi ambayo mtu yoyote anaweza kuelewa. Ripoti kamili ni ndefu na imejaa mambo mbayo sio rahisi Kwa mwananchi wa kawaida kuelewa. Kwahiyo kama ulitegemea kupata ripoti yote kupitia magazeti hiyo sahau, hiyo ripoti ni ya serikali na wataalamu wa mambo ya kifedha.
 
Umejibu swali gani kati ya hayo mawili na nusu?

Nimekuuliza maswali hayo si kwa maana eti sijui au kwa lengo la kuwavunjia heshima NBS. Lakini mbona maswali hayo sijawauliza NBS! Nimekuuliza wewe uliyetoa hoja kwamba bei ya mafuta inaweza kuathiri mfumuko wa bei za bidhaa zingine ili tujiridhishe ukweli huo kutokana na ripoti ya NBS. Labda nikuongeze swali lingine.

Je, unaweza kuthibitisha ulichokisema kwa kutumia "holistic report" ya NBS? Haya twende kazi!
 
Forum statistics

Threads 1,343,339
Members 515,022
Posts 32,781,310
Top