Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba leo Bungeni Dodoma amewasilisha Bungeni taarifa ya Hali ya Uchumi wa Kitaifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka 2023/2024 ambapo moja ya mambo aliyoyasema ni kwamba mfumuko wa bei nchini umeendelea kuwa ndani ya lengo la wigo wa kuwa chini ya asilimia 5.
“Mwaka 2022, mfumuko wa bei ulifikia wastani wa asilimia 4.3 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.7 mwaka 2021, aidha mfumuko wa bei hadi mwezi Mei, 2023 umebaki kama ilivyokuwa katika kipindi hicho hicho mwaka 2022 ikiwa ni wastani wa asilimia 4.0”
“Hali hii imesababishwa na kuongezeka kwa uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma na kuongezeka kwa upatikanaji wa mazao ya chakula katika baadhi ya maeneo nchini na Nchi jirani kulikosababishwa na upatikanaji wa mvua katika maeneo yanayotegemea mvua”