msindikizaji
JF-Expert Member
- Aug 29, 2010
- 1,763
- 2,883
Unga wa sembe unauzwa kati ya tshs 1500-1800 miezi ya nyuma ulikua buku. Hapa mfumuko umepungiaje...hebu tuelimishe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata mje na id 100 hakuna uteuzi kwenu nyambafni wivu tu
wacha kujimwambafai
Umesoma vilivyopungua au?Halafu bado tunaimbiwa ngonjera na wana Pinga-Pinga Stars, maisha ni magumu. SMH
Unafikiri 1.7T kwa mwezi imetoka wapi?Haya mambo mimi huwa naona maruweruwe tu, huwa siyaelewi kabisa, sukari huku 2500, mfuko wa saruji 20000/=Mche wa sabuni 2600/= ...wengine mafuta ya nywele tunayasikia kwenye vyombo vya habri, pakiti ya chumvi 800/= lita ya mafuta ya kupika 5000/= sasa haya mambo yamekaaje wadau maana utaskia mara bei imeshukaaaa. Lakini mimi huu ni mwaka wa nne mfululizo nanunua mfuko wa saruji 20000/ ....Wakati mwingine naamini Tanzania ni ya wachache tu.
Mkuu Pascal kilchopungua bei ni bidhaa zisizo za vyakula. Ukiangalia bidhaa za vyakula zimepanda bei sana na ndizo zenye athari ya moja kwa moja kwa mwananchi.Hii ni taarifa muhimu sana, uchumi wa Magufuli has started doing good, then better and finally best!.
P
Kweli umeshuka, kg moja ya unga wa sembe kutoka efu moja na sasa ni tsh 1400,Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi septemba, 2019 umepungua hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.
Hayo yamesemwa na Kaimu mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja wakati akitangaza mfumuko wa bei jana Jijini Dodoma.
“Kushuka kwa mfumuko wa bei kunatokana na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwezi Septemba 2019 ikilinganishwa na bei za kipindi cha Septemba,2018”. Alisisitiza Bi. Minja.
Akifafanua amesema kuwa baadhi ya bidhaa zilizopungua bei kwa mwezi Septemba ni mafuta ya taa asilimia 1.0, Petroli asilimia 3.3 ,majiko ya gesi asilimia 1.5, dawa za kuulia wadudu nyumbani asilimia 2.2 na mafuta ya nywele asilimia 1.3.
Aliongeza kuwa mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.
Akizungumzia nchi za Afrika Mashariki Bi. Minja amesema kuwa mfumuko wa Bei nchini Kenya kwa mwezi Septemba umepungua hadi asilimia 3.83 kutoka 5.00 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.
Kwa upande wa nchi ya Uganda, mfumuko wa Bei kwa mwaka unaoishia mwezi Septemba 2019 umepungua hadi asilimia 1.9 kutoka asilimia 2.1 kwa mwaka unaoishia mwezi Agosti, 2019.
Kuna watu hata wakisikia mfumuko wa bei ni 1% watashangilia bila kujua athari zake tuache siasa kwenye kwenye mambo muhimu kama haya.
Umesoma vilivyopungua au?
Akifafanua amesema kuwa baadhi ya bidhaa zilizopungua bei kwa mwezi Septemba ni mafuta ya taa asilimia 1.0, Petroli asilimia 3.3 ,majiko ya gesi asilimia 1.5, dawa za kuulia wadudu nyumbani asilimia 2.2 na mafuta ya nywele asilimia 1.3.
Kati ya hivyo wewe kipi kinakuhusu kama upo kijijini? Wangapi wanatumia mafuta ya nywele, majiko ya gas na dawa za kuulia wadudu majumbani?
Nashukuru kwa ufafanuzi maana wengine tunaishi porini kusikokuwa na radio wala tv hivyo hatujui kitokeacho makwetu.Hakuna kitu kinapaisha mfumuko wa bei kama mafuta, kuanzia mafuta ya taa, petroli dizeli, mafuta ya kuendesha mashine viwandani mpaka mafuta ya uzalishaji umeme. Hayo yote yanamgusa hata akiyekuwa kijijini ambaye hajawai kukajaga mguu mjini. Ukitaka maisha yawe magumu kweli kweli, ongeza bei ya mafuta.
Cha msingi, ni kuangalia hiyo ripoti kwa kina na kuilinganisha na takwimu za mwaka jana, na pia ni kujua kwanini bei zinashuka. Uzalishaji wa umeme wa kutumia gesi asilia umwongezeka kuliko tulivyojuwa tunaagiza mafuta kutoka nje, ununuzi wa bidhaa kutoka nje kiholela umeshuka, ufanisi wa viwanda vya ndani unauimarika, na hata kupelekwa watu nje Kwa matibabu pia pungua. Bila kusahau tumepata uzalishaji wa chakula cha kutosha mpaka tunauza nje ya nchi.
Rejea awamu iliyopita. Infration rate unajua ilichezea rate gani?Congrats kwa serikal, moja ya target ya mwaka wa fedha 2019/2020 ilikua kumaintain infation rate katika single digit kati ya 3.0 had 4.5 ..na wamefanikiwa