Mfumuko wa Bei wa Taifa Washuka hadi Asilimia 3.4

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2019
Messages
381
Points
500

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined May 23, 2019
381 500
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi septemba, 2019 umepungua hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Hayo yamesemwa na Kaimu mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja wakati akitangaza mfumuko wa bei jana Jijini Dodoma.

“Kushuka kwa mfumuko wa bei kunatokana na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwezi Septemba 2019 ikilinganishwa na bei za kipindi cha Septemba,2018”. Alisisitiza Bi. Minja.

Akifafanua amesema kuwa baadhi ya bidhaa zilizopungua bei kwa mwezi Septemba ni mafuta ya taa asilimia 1.0, Petroli asilimia 3.3 ,majiko ya gesi asilimia 1.5, dawa za kuulia wadudu nyumbani asilimia 2.2 na mafuta ya nywele asilimia 1.3.

Aliongeza kuwa mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Akizungumzia nchi za Afrika Mashariki Bi. Minja amesema kuwa mfumuko wa Bei nchini Kenya kwa mwezi Septemba umepungua hadi asilimia 3.83 kutoka 5.00 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.
Kwa upande wa nchi ya Uganda, mfumuko wa Bei kwa mwaka unaoishia mwezi Septemba 2019 umepungua hadi asilimia 1.9 kutoka asilimia 2.1 kwa mwaka unaoishia mwezi Agosti, 2019.
 
RUSSESABAGINA

Senior Member
Joined
Dec 23, 2016
Messages
145
Points
250

RUSSESABAGINA

Senior Member
Joined Dec 23, 2016
145 250
Kwa taarifa yankuvunja rekod ya makusanyo ya kodi hivi juzi juzi tu, inatupa picha kiwa kiasi cha mzunguko wa fedha kwenye uchumi kimepungua, so technically thaman ya sarafu itakua maintained pamoja na inflation rate kupungua. Simple economics
Data za NBS sio za huku mtaani, hizo ni za ofisini lakini ukweli ni kuwa bidhaa zote zimepanda bei.
 
RUSSESABAGINA

Senior Member
Joined
Dec 23, 2016
Messages
145
Points
250

RUSSESABAGINA

Senior Member
Joined Dec 23, 2016
145 250
Congrats kwa serikal, moja ya target ya mwaka wa fedha 2019/2020 ilikua kumaintain infation rate katika single digit kati ya 3.0 had 4.5 ..na wamefanikiwa
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi septemba, 2019 umepungua hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Hayo yamesemwa na Kaimu mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja wakati akitangaza mfumuko wa bei jana Jijini Dodoma.

“Kushuka kwa mfumuko wa bei kunatokana na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwezi Septemba 2019 ikilinganishwa na bei za kipindi cha Septemba,2018”. Alisisitiza Bi. Minja.

Akifafanua amesema kuwa baadhi ya bidhaa zilizopungua bei kwa mwezi Septemba ni mafuta ya taa asilimia 1.0, Petroli asilimia 3.3 ,majiko ya gesi asilimia 1.5, dawa za kuulia wadudu nyumbani asilimia 2.2 na mafuta ya nywele asilimia 1.3.

Aliongeza kuwa mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Akizungumzia nchi za Afrika Mashariki Bi. Minja amesema kuwa mfumuko wa Bei nchini Kenya kwa mwezi Septemba umepungua hadi asilimia 3.83 kutoka 5.00 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.
Kwa upande wa nchi ya Uganda, mfumuko wa Bei kwa mwaka unaoishia mwezi Septemba 2019 umepungua hadi asilimia 1.9 kutoka asilimia 2.1 kwa mwaka unaoishia mwezi Agosti, 2019.
 
Mwanzi1

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2016
Messages
5,246
Points
2,000

Mwanzi1

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2016
5,246 2,000
Data za NBS sio za huku mtaani, hizo ni za ofisini lakini ukweli ni kuwa bidhaa zote zimepanda bei.
Lazima ukubali zama hizi sio za kukaa chini na hela ikufuate huko uliko, idadi ya watu imeongezea na inachingia hela kusogea mbali lakini haimaanishi kuwa maisha ni magumu. Baadhi ya Watanzania wanashindwa kwenda na kasi ya sasa hivi.
 
mwakijembe

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2017
Messages
892
Points
1,000

mwakijembe

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2017
892 1,000
Lazima ukubali zama hizi sio za kukaa chini na hela ikufuate huko uliko, idadi ya watu imeongezea na inachingia hela kusogea mbali lakini haimaanishi kuwa maisha ni magumu. Baadhi ya Watanzania wanashindwa kwenda na kasi ya sasa hivi.
Huyo mwenye hiyo kasi mwenyewe hajui hata bei ya mchele, kila kitu analipiwa kuanzia chakula, mavazi, malazi, maji, umeme mpaka airtime. Pale muongoza anapokuwa tegemezi unategemea nini?
 
1954

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Messages
6,331
Points
2,000

1954

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2006
6,331 2,000
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi septemba, 2019 umepungua hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Hayo yamesemwa na Kaimu mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja wakati akitangaza mfumuko wa bei jana Jijini Dodoma.

“Kushuka kwa mfumuko wa bei kunatokana na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwezi Septemba 2019 ikilinganishwa na bei za kipindi cha Septemba,2018”. Alisisitiza Bi. Minja.

Akifafanua amesema kuwa baadhi ya bidhaa zilizopungua bei kwa mwezi Septemba ni mafuta ya taa asilimia 1.0, Petroli asilimia 3.3 ,majiko ya gesi asilimia 1.5, dawa za kuulia wadudu nyumbani asilimia 2.2 na mafuta ya nywele asilimia 1.3.

Aliongeza kuwa mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Akizungumzia nchi za Afrika Mashariki Bi. Minja amesema kuwa mfumuko wa Bei nchini Kenya kwa mwezi Septemba umepungua hadi asilimia 3.83 kutoka 5.00 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.
Kwa upande wa nchi ya Uganda, mfumuko wa Bei kwa mwaka unaoishia mwezi Septemba 2019 umepungua hadi asilimia 1.9 kutoka asilimia 2.1 kwa mwaka unaoishia mwezi Agosti, 2019.
Zito anasemaje ???!!! Kesho kama siyo leo atakanusha habari hizi akiungwa mkono na wale ambao kila kitu cha awamu ya tano humu JF
 
Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
11,793
Points
2,000

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
11,793 2,000
Kuna kitu mnaficha Hapo, Bei haijapungua Bali imeongezeka, sema ongezeko la Bei ndio limepungua.

Mfano Kama bidhaa ilikuwa 1000 mwezi uliopita, mwezi huu itakuwa imeongezeka Hadi 1034 kwa ongezeko la asilimia 3.4
Mimi sielewi hizi data wanazipatia wapi. Maana kwa sasa Dar vyakula na bidhaa nyingine muhimu vimepanda bei. Mfano mahindi mwezi wa 8 kurudi chini yalikuwa yanauzwa 80,000 kwa gunia la kilo 100 inamaana 800 kilo Moja,lakini tangu Mwezi wa Tisa bei imepanda mpaka kilo moja ya mahindi kufikia 1300,maharage na mchele nayo vivyo hivyo.
 
Forum statistics

Threads 1,343,347
Members 515,021
Posts 32,781,651
Top