Mfumo wa Matumizi ya Tarakilishi (Operating System) kwa Lugha ya Kiswahili

authjeremmy

authjeremmy

Member
8
45
Salamu kwenu wote.

Jina langu ni Jeremiah Rotich, kutoka nchi ya Kenya. Ningependa kuchukua fursa hii kuwatangazia kuwa nimeanzisha shirika/ mradi linalowania kutengeneza Mfumo wa Matumizi (Operating System) kwa lugha ya Kiswahili. Wengine wenu mnaweza kuwa mnafahamu uwepo wa kilinux iliyoanzishwa mwakani 2003. Ila kwa maoni yangu, sioni ikiwa mradi huo ulitufikia sisi sote kwa maana hamna mfumo hadi sasa unaotumia lugha ya Kiswahili kwa hali msingi.

Jina la mradi ni Swahilinux na unapatikana katika wavuti hii ya Swahilinux. Tunawaomba nyote kujiunga na kundi letu kwenye Twitter, Telegram au kuchangia kwa tafsiri kwa kujiunga na jukwaa letu la Tafsiri

Mfumo utakaotokana na mradi huu utajengwa kwa msingi wa Linux (Linux Kernel) na toleo la kwanza la majaribio litatoka Desemba mwaka huu (2019).

Asanteni.
 
Root

Root

JF-Expert Member
36,159
2,000
Ila tafadhari Usitumie Kiswahili chenu maana si sahihi
 
Stefano Mtangoo

Stefano Mtangoo

Verified Member
3,964

Ni Distro tofauti, au customized kwa kiswahili kwenye lugha tu? Desktop Environment? Ungeweka Tech summary ya mradi ingekuwa vyema!
 
authjeremmy

authjeremmy

Member
8
45
Ila tafadhari Usitumie Kiswahili chenu maana si sahihi
Kiswahili ni kimoja, Kiswahili chetu si kibaya, watu ndio wenye kupenda utohozi, ila ukienda pwani utapata kuwa Kiswahili cha Kenya na Tanzania ni sawia. Na ni kwa ajili ya hili ndiyo maana nawaomba muweze kuchangia ili kuhakikisha kuwa tunatumia lugha sanifu.
 
authjeremmy

authjeremmy

Member
8
45
Ni Distro tofauti, au customized kwa kiswahili kwenye lugha tu? Desktop Environment? Ungeweka Tech summary ya mradi ingekuwa vyema!
Kwa sasa, Swahilinux ipo kwenye hatua yake ya kwanza kati ya hatua nyingine nyinge, hatua hii, ni tafsiri. Baada ya kuwa na programu za kutosha katika lugha ya Kiswahili, basi tutaweza kuendelea na hatua zingine ambazo kwa sasa tunazifanya ila kwa mchango mdogo. Swahilinux itakuja kama distro tofauti, ila mtu unayetumia distro nyingine anaweza kuweka distro hiyo kuwa katika lugha ya Kiswahili, kwa maana mradi huu ni wa mfumo wazi (Open Source). Tunatumia leseni ya Umma ya GNU GPL2 na tayari tumewasiliana na shirikisho la FSF - Free Software Foundation ili kupata ruhusa ya kutafsiri Distro zote kwa lugha ya Kiswahili.
 
Hapo ipo clear. Kuna vitu vichache hata hivyo. Swahili haijakaa poa. Lugha inaitwa Kiswahili na wazungu ndio huiita Swahili. Samahani lakini nadhani si sawa kuiita swahili.

Kitu cha pili hauhitaji kibali cha FSF kwa sababu GPL2 ipo na inaruhusu software yoyote kutumia GPL software bila kutafuta kibali. Alimradi tu kama unatumia GPL lazima product yako iwe pia kwenye GPL. Pili hata ingekuwa unahitaji leseni, FSF sio mahali sahihi. Mahali sahihi ingekuwa ni kwenye base distro mnayotumia iwe ni Ubuntu/Debian, Fedora et al.

Mwisho jina la mradi litapendeza kama likiwa na maana pana zaidi. Mfano unaweza kutumia jina la Mnyama kama SimbaOS au hata kitu maarufu.kama Afrinux or anything but a language

Wishing you success. God blessings!
 
Asante kwa maoni yako ila sijasema kuwa jina la OS lenyewe litakua Swahilinux, Jina la Mradi ndio Swahilinux (Labda sikueleweka) kuna njia mingi za kuafikia jina litakalotumika na ifikapo wakati huo tutakua na jibu sahihi. Natumai kuwa watu wote watatuunga mkono na kuisherekea lugha yetu ya Kiswahili. FSF wametupa nafasi ya kufanya tafsiri kwenye mfumo wa GNU/Linux (Ila sio kama kibali, ina maana tutasimamia tafsiri kweye distro ya GNU/Linux na nyinginezo kama Ubuntu/Debian). Mfumo wenyewe utatolewa kwa Debian ili kuifanya kuwa rahisi kwa mtumizi wa kawaida. Asante.
 
Forum statistics

Threads
1,424,796

Messages
35,072,786

Members
538,098
Top Bottom