Naomba Bakita iingilie Kati kwani tafsiri ya John 1:18 kwenda lugha ya kiswahili imepotoshwa kwa makusudi maalumu

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,209
4,706
Wadau wote wa JF nawasalimu kwa jina la Bwana

Niseme wazi kuwa tafsiri ya Yohana ( John) 1:18 kwenda lugha ya kiswahili imepotoshwa kwa makusudi kukidhi Imani za watu wanaoamini kwenye fundisho la Utatu

Neno "the only begotten Son" tafsiri yake sahihi Kwa lugha ya kiswahili ni "Mwana Pekee wa Mungu" na siyo MunguMwana.

Nimeweka fungu hilo kwa lugha zote mbili kwa rejea yenu.

Baraza la Kiswahili Tanzania naomba msaada wenu tafadhali
Niwatakie sabato njema

•No man hath seen God at any time; the only begotten Son, which is in the bosom of the Father, he hath declared him•

•Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua. Ushuhuda wa Yohana Mbatizaji•
 
Kwani tofauti ya Mungu Mwana na Mwana Pekee wa Mungu ni nini?
Fahamu kwa asili Mwana wa Mungu ni Mungu! Yaani amezaliwa au ametokana na Mungu mwenyewe! Kwa hiyo ni sahihi kusema Yesu Kristo ni Mungu Mwana.
Kama hukubaliani na hilo, soma, Yohana5:17-18, Yohana10:30-36
Katika maandiko haya Wayahudi walitaka kumpiga mawe Yesu kwa kumwita Mungu ni Baba yake! Walijua Mwana wa Mungu ni Mungu sawa na Mungu Baba.
Kwa hiyo waliamini Yesu Kristo ni binadamu tu wa kawaida! Kwa kumwita Mungu ni Baba waliona anakufuru.
 
Ili utafsiri Kiswahili au kiingereza unabidi kujikita katika kimantiki yaani utafsiri neno ili lieleweke na kutoa maana na sio ili litoe maana bila kueleweka.
 
Wadau wote wa JF nawasalimu kwa jina la Bwana

Niseme wazi kuwa tafsiri ya Yohana ( John) 1:18 kwenda lugha ya kiswahili imepotoshwa kwa makusudi kukidhi Imani za watu wanaoamini kwenye fundisho la Utatu

Neno "the only begotten Son" tafsiri yake sahihi Kwa lugha ya kiswahili ni "Mwana Pekee wa Mungu" na siyo MunguMwana.

Nimeweka fungu hilo kwa lugha zote mbili kwa rejea yenu.

Baraza la Kiswahili Tanzania naomba msaada wenu tafadhali
Niwatakie sabato njema

•No man hath seen God at any time; the only begotten Son, which is in the bosom of the Father, he hath declared him•

•Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua. Ushuhuda wa Yohana Mbatizaji•
Fungua kanisa ustaadh uwe unatafsiri Bible kwa usahihi.
 
Kwa nini Bakita mkuu......Kwa nini usiende kwenye original manuscripts....Au una ajenda nyingine.....Bakita inaweza kutoa taafsri yoyote kwenye Maandiko ya dini....Inaweza kufanya hiyo kwenye Quraan.....?
 
Kwani tofauti ya Mungu Mwana na Mwana Pekee wa Mungu ni nini?
Fahamu kwa asili Mwana wa Mungu ni Mungu! Yaani amezaliwa au ametokana na Mungu mwenyewe! Kwa hiyo ni sahihi kusema Yesu Kristo ni Mungu Mwana.
Kama hukubaliani na hilo, soma, Yohana5:17-18, Yohana10:30-36
Katika maandiko haya Wayahudi walitaka kumpiga mawe Yesu kwa kumwita Mungu ni Baba yake! Walijua Mwana wa Mungu ni Mungu sawa na Mungu Baba.
Kwa hiyo waliamini Yesu Kristo ni binadamu tu wa kawaida! Kwa kumwita Mungu ni Baba waliona anakufuru.
Mwana wa Mungu na MunguMwana unaona inamaana moja?
 
Jinsi miaka inavyozidi kwenda, Idadi ya watu wanaotilia shaka hizi dini inazidi kuongezeka.
Ikifika mwaka 2,500 kutakuwa hakuna kanisa wala msikiti. Sisi tutaonekana leo tulikua vituko kwa kuamini hizi dini. Watatuona tulipumbazwa mno. Hakutakuwa na mwanazuoni hata mmoja. Dunia itakuwa sehemu nyingine kabisa. Wanawake hawatabeba mimba matumboni. Mtu ataishi London na kufanya kazi Zanzibar. Watashangaa Mungu ndio kitu gani na amewahi kufanya nini.
 
Mkuu TOHATO:

Mwanadamu ni religious being! Dini haziwezi kufa kabisa, ziko ndani ya mwanadamu! Ulitoka wapi, kwa nini unaishi, kunamaisha ya baada ya kifo, kuna nguvu nyingine juu ya maisha mwanadamu itaendelea kumsumbua mwanadamu.
Karl Max, mwaka 1843 alisema dini ni bangi, katika kijitabu chake kimoja, iko kumfanya binadamu ajisahaulishe matatizo yake kwa muda, na kungojea furaha za milele! Na aliamini kabisa dini zitakufa natural death...! Leo ni miaka mingapi dini zimeshindwa kufa! Sisemi Ukristo wala Uislamu! Dini za kila aina zimegoma kufa! Zinapanda zinashuka, na zinakuja kwa njia nyingi mno.....!

Hivyo mkuu licha ya kutilia shaka, kila kukicha mauzo ya vitabu vya dini, licha ya watu kujaribu kuonyesha mapungufu yake, ndio inazidi kuongezeka.
 
Hawaongezeki ila wanapungua sana.

kama tukipata twakwimu sahihi za kipindi cha mwanzo na sa hivi utaona jibu

Pia watu huwa nazo kwasababu maalumu
Kama vile ndoa, kuzikwa na wengi ni tumerithi kutoka kwa wazazi ila watu tayari washaaanza kuzilitia mashaka sana.

Miaka ya nyuma siku ya kanisani ukikuta vile vijiji ambazo dini iko moja ilikuwa ni watu wote wako kanisani hata ukitaka fanya biashara hiyo siku hupati kitu. Ila leo wengi huja na misemo nitasalia hata nyumbani,mara hoo kanisani michango mingi, mara kinachotakiwa ni imani.
Hapa ni uhalisia ukakasi wa dini umeanza pungua.
 
Mkuu Dini nini hasa? Chochote ambacho unaweka matumaini yako kinaweza kuwa ni dini.....Unashangaa huko vijijini unakosema hawaonekani misikitini na makanisani.....Ngoja wafariki.....Ndugu watajaribu kutafuta maziko ya Kikiristo au Kiislamu....Ujawahi kukuta watu wanagombania mwili wa marehemu wamzike kidini? Umesikia au mewahi kuona mtu kazikwa bila kuwa na taratibu za kidini? Hata za jadi yetu ya Kiafrika hakuna kabisa....
 
Ikifika mwaka 2,500 kutakuwa hakuna kanisa wala msikiti. Sisi tutaonekana leo tulikua vituko kwa kuamini hizi dini. Watatuona tulipumbazwa mno. Hakutakuwa na mwanazuoni hata mmoja. Dunia itakuwa sehemu nyingine kabisa. Wanawake hawatabeba mimba matumboni. Mtu ataishi London na kufanya kazi Zanzibar. Watashangaa Mungu ndio kitu gani na amewahi kufanya nini.
kuna miji haina maduka' mingne haina umeme ' mingne haina hospital' mingne haina huduma zozote za kijamii' LKN MJI USIOKUWA NA MAHEKALU NA MISIKITI mimi sijawahi iona
 
Yesu ni Mungu mafungu mengi tu. Umeamua kumshtaki Bakita. Hahahaha

New International Version
No one has ever seen God, but the one and only Son, who is himself God and is in closest relationship with the Father, has made him known.
👌👌👌
Kashtaki na kwa Bakita za ulaya pia.
 
Ikifika mwaka 2,500 kutakuwa hakuna kanisa wala msikiti. Sisi tutaonekana leo tulikua vituko kwa kuamini hizi dini. Watatuona tulipumbazwa mno. Hakutakuwa na mwanazuoni hata mmoja. Dunia itakuwa sehemu nyingine kabisa. Wanawake hawatabeba mimba matumboni. Mtu ataishi London na kufanya kazi Zanzibar. Watashangaa Mungu ndio kitu gani na amewahi kufanya nini.

Mkuu Sean: Binadamu ni religious being......atagundua dini nyingine......labda aache kwenda kaburini....Karl Marx aliamini sayansi ingeua imani......akiamka leo toka kaburini atashangaa.....
 
Wadau wote wa JF nawasalimu kwa jina la Bwana

Niseme wazi kuwa tafsiri ya Yohana ( John) 1:18 kwenda lugha ya kiswahili imepotoshwa kwa makusudi kukidhi Imani za watu wanaoamini kwenye fundisho la Utatu

Neno "the only begotten Son" tafsiri yake sahihi Kwa lugha ya kiswahili ni "Mwana Pekee wa Mungu" na siyo MunguMwana.

Nimeweka fungu hilo kwa lugha zote mbili kwa rejea yenu.

Baraza la Kiswahili Tanzania naomba msaada wenu tafadhali
Niwatakie sabato njema

•No man hath seen God at any time; the only begotten Son, which is in the bosom of the Father, he hath declared him•

•Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua. Ushuhuda wa Yohana Mbatizaji•
Mbelea kutumia tafsiri tofauti pale ambapo unaona huelewi na pana kuchanganya juu ya kile unachokisoma katika Biblia kwa mfano BHN imeandikwa hivi.
‭‭Yohane‬ ‭1:18‬ ‭BHN‬‬
[18] Hakuna mtu aliyemwona Mungu kamwe. Mwana wa pekee aliye sawa na Mungu ambaye ameungana na Baba, ndiye aliyetujulisha habari za Mungu.
 
Back
Top Bottom