Kitabu cha Rais Xi Jinping kuhusu “Utawala wa China” toleo la lugha ya Kiswahili chatolewa

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
bnvcnvnvcn.jpg


Kitabu cha Rais Xi Jinping chenye jina la “The Governance of China” toleo la Kiswahili, kimetolewa kwa wasomaji kwenye hafla fupi iliyofanyika Agosti 14 mjini Nairobi. Hii ni juzuu ya kwanza ya mfululizo wa juzuu nne, kikiwa na mkusanyiko wa hotuba na maagizo mbalimbali ya Rais Xi Jinping katika vipindi mbalimbali tangu awe Rais wa China.

Kitabu hiki ambacho jina lake la Kiswahili ni “Utawala wa China”, ni kitabu cha kwanza cha kiongozi wa China kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili, na kufanya hafla maalum ya kutolewa kwa kitabu hicho kwa ajili ya wasomaji wa lugha ya Kiswahili. Kitabu hicho kinatarajiwa kuwawezesha wasomaji wa lugha ya Kiswahili kupata uelewa wa jumla kuhusu mambo mbalimbali ya kisiasa na ya utawala ya China, yaliyomo kwenye hotuba mbalimbali zilizotolewa na Rais Xi.

Umaalum wa kitabu hiki ni kuwa kwanza, sehemu kubwa ya kitabu ni tafsiri inayotokana na toleo la lugha ya kichina ambalo ndio toleo halisi, kwa hiyo maana yake ni maana inayotokana na maneno ya kichina ya mkusanyiko wa hotuba za Rais Xi Jinping. Hii ni tofauti na kama ingekuwa ni tafsiri kutoka lugha ya kiingereza, yaani tafsiri ya tafsiri, ambayo ingekuwa na upungufu fulani. Pili, ni kwa sababu watu waliotafsiri kitabu hiki ni wachina wenye uelewa wa kutosha wa lugha ya Kiswahili, kwa hiyo wameweza kufikisha ujumbe kama ulivyokuwa kwenye toleo la asili.

Wasomaji wa kitabu hiki wanaweza kupata uelewa wa jumla kuhusu kazi za utawala wa nchi zinavyofanywa nchini China. Ikumbukwe kuwa baadhi ya sehemu zinagusia chama tawala cha China (yaani chama cha Kikomunisti), nafasi yake katika mfumo wa kisiasa wa China, pamoja na vyama vingine vya kisiasa ambavyo havifahamiki sana kwa nchi za nje.

Baadhi ya sehemu zinagusia bunge la umma la China ambalo utendaji wake na utaratibu wa kuchagua wajumbe wake, na hata mikutano yake inaendeshwa kwa mtindo tofauti na mabunge ya nchi za jumuiya ya madola kama ilivyo kwa Kenya na Tanzania. Wakati huohuo, jambo la kufurahisha kwenye kitabu hiyo ni historia ya utumishi wa umma ya Rais Xi Jinping mwenyewe, tangu alipoanza uongozi akiwa katibu wa chama ngazi ya kijiji, hadi kufikia nafasi ya katibu wa chama ngazi ya taifa. Wasomaji wanaweza kupata uelewa kupitia hotuba mbalimbali alizotoa.

Wachambuzi na wanahabari wa baadhi ya nchi wanapenda kusema kuwa uongozi wa nchi wa China hauko wazi na utendaji wake haieleweki vizuri, lakini hii ni kutokana na kukosa uelewa kuhusu mfumo wa utawala wa China, na kutojua desturi za viongozi wa China. Kupitia kitabu hiki msomaji anaweza kujua kuwa kila kipindi cha mwaka mpya wa jadi wa China Rais wa China huwa anafanya nini, na kila kipindi cha mkutano wa bunge la umma na mkutano wa baraza la mashauriano ya kisiasa (kipindi kinachoitwa kipindi cha mikutano miwili) Rais huwa anafanya nini.

Mbali na mambo hayo kuna baadhi ya mambo ambayo huenda ni muhimu sana kwa mazingira ya sasa ya nchi za Afrika. Kwa mfano, kuna hotuba kadhaa za Rais Xi akizungumzia kazi za kupamba na umaskini, kazi za kuhakikisha usafi wa mazingira, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, na jambo la muhimu zaidi ni mambo ya ushirikiano kati ya China na Afrika, na kati ya China na nchi mbalimbali za Afrika.
 
Back
Top Bottom