meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,464
- 4,828
- Thread starter
- #141
Wanasiasa wanatufanya mabwege sana.
Sioni jipya zaidi ya uroho wa madaraka tu.Wale tuliowachukia na waliounda mfumo huu dhaifu na wa kimagumashi ndio hao leo wanaokuja kujidai wanasaidia mabadiliko.
Wale wale waliotupigia na kutuulia ndugu zetu leo hii wanajidai wanasaidia ukombozi.
Hii ni big joke yaani ni kama vile Netanyahu aungane na Abass ili kuwakomboa wapalestina.
Ndio maana watanzania waliukataa mfumo wa vyama vingi kwani wanasiasa wetu ni wasanii.
Ndio maana nchi ilikuwa inayumba kisa kuna vikundi ndani ya ccm venye uroho wa madaraka.
Dawa yao ni kuwatosa tu.
Cha msingi chagua mbunge wa upinzani mengine baadae:mvutaji:
Kinachotokea hivi sasa ni muhimu sana na tena kilichelewa. Kwa kuwa watanzania ni wale wale imelazimu wajigawe mara mbili au hata tattu washindane. kinachotakiwa ni kushindana kwa faida ya nchi. Mchezo wa SEE SAW hauwezi kuendelea ikiwa upande mmoja utazidi sana upande wapili. sasa mchezo utabanceWalishindwaje kuwatumikia wananchi miaka 12 iliyopoita halafu waweze leo?
Tena kiazi haswaaaaa, ukawa kichwa cha mwendawazimu, kila mtu anajifunzia kunyoa.
Cha msingi chagua mbunge wa upinzani mengine baadae:mvutaji:
Ni vema ukapima yaliyotekelezwa ndani na hawa mawaziri wakuu watatu (3)
1. Sumaye
2. Lowassa
3. Mizengo Pinda
Ukiishapima ufanye tathimi ya kashfa kubwa zilizolipotezea taifa mabillion ya shillingi zilitokea katika kipindi cha Waziri Mkuu yupi baada ya hapo sidhani kama hiki ulichokiandika kitakuwa na thamani tena kwako na hao wapambe wako.
Poor analysisWanasiasa wanatufanya mabwege sana.
Sioni jipya zaidi ya uroho wa madaraka tu.Wale tuliowachukia na waliounda mfumo huu dhaifu na wa kimagumashi ndio hao leo wanaokuja kujidai wanasaidia mabadiliko.
Wale wale waliotupigia na kutuulia ndugu zetu leo hii wanajidai wanasaidia ukombozi.
Hii ni big joke yaani ni kama vile Netanyahu aungane na Abass ili kuwakomboa wapalestina.
Ndio maana watanzania waliukataa mfumo wa vyama vingi kwani wanasiasa wetu ni wasanii.
Ndio maana nchi ilikuwa inayumba kisa kuna vikundi ndani ya ccm venye uroho wa madaraka.
Dawa yao ni kuwatosa tu.
Ahadi zaViongozi wa Siasa ni uongo mtupu. Vipi Ahadi ya Kiongozi wenu aliyesema Hivi ninanukuu (MAISHA BORA KWA KILA M-TANZANIA) Haya kuna maisha gani bora Tangu Huyu Mkuu atangaze hiyo iKampeni au ilani yake ya Uchaguzi tangu ashike Madaraka kuna maishagani bora hapo Tanzania? kam Sias sio uongo wa hali ya juu ni kitu gani? Nenda kasome tena Shule wewe sijuwi umesoma chini ya muembe wewe ? Mutadanganywa na Viongozi wa Siasa wao Viongozi wananufaika nyinyi walal hoi munazidi kuumia kazi kwako au kazi kwenu Walala Hoi ni Siasa za Viongozi wa kisia za uongo mtupu.Nasikitika kwa mwalimu wako kukuganganya na ningekushauri urudi shule tu.kama siasa ni uongo niambie nani anaamua barabara fulani ijengwe au na kwa mujibu wa mwalimu wako barabara pia ni uongo?shule ni uongo?Pole ndugu
Poor analysis
Mimi sioni tatizo kabisa hao watu wanaotoka CCM na kujiunga na upinzani.
Ndo uhalisia wa siasa huo.
Watu huhama na kubadili kambi mara zote na si Tanzania tu bali ni duniani kote.
Kama wana nia ya kweli ya kuimarisha upinzani na kujenga upinzani wenye nguvu basi mimi sina tatizo kabisa.
Acha tu watoke huko CCM.
a. Suala la kutokuweka timetable vizuri ya uchaguzi hadi miezi tu kabla ya Uchaguzi imetengeneza wanasiasa uchwara sana. Fikiria kwa mfano, sheria ingesema kwa mfano wagombea wa nafasi mbalimbali wawe wamejitokeza na kujulikana angalau miezi 12 kabla ya Uchaguzi Mkuu na wawe angalau wanachama wa vyama husika mwaka mmoja kabla hawajagombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma (public office).
Ilivyo sasa, utaoana kuwa wengi wanaohama hakuna anayehama kwa sababu hasa amepingana kifikra au kiitikadi na chama chake. Fikiria hivi.. leo hii kuna kundi la "ulipo tupo"; kundi hili ni wazi halijaifuata CDM hata kidogo bali wamemfuata yule bwana alipo. Sasa ikitokea hayupo au anaamua kujitoa tu.. unafikiria wale wa "ulipo tupo" wataendelea kumpigia kura mgombea au wagombea wa CDM tena? si watasema "hayupo na sisi hatupo"?
Hatari kubwa ni mwisho wa siku fikra tulizozikataa kwa watawala wa sasa zinaweza kabisa kuibukia kwa watawala wajao... ndio maana ni muhimu sana kupinga (dissent) pale inapoonekana ni lazima.