Mfumo ule ule unataka kurudi kupitia UKAWA!

Mfumo ule ule unataka kurudi kupitia UKAWA!

Ndo maana wasiwasi wangu ni kama ikitokea UKAWA wanashindwa, ina maana hawa akina Johnny-come-lately watahama upinzani na kurudi tena CCM?

.

Ngosha are you a betting man? Dili zima linategemea CHADEMA kushinda; lakini wakishindwa... hawa waliokuwepo wapo hawatakuwepo tena!
 
Lengo la kwanza ni kupiga chini hili limbuyu, hayo mengine baadae mbele ya safari na Mungu anatusaidia...... Mkuu watanzania wanataka mabadiliko ambayo kiuhalisia ndani ya CCM yameshindikana......
 
Waliokuwa wapigwa kuwa ni mafisadi leo hii ni malaika, huu ni upumbavu wa hali ya juu na UKAWA WAMETIA FORA.

Sasa ccm imekuwa safi sana, kwani mafisadi yameamua kukimbilia chadema, make huku Makufuri ni moto wa kuotea mbali afadhali wamekiacha chama chetu cha wanyonge na wafanyakazi, haya makongoro Nyerere aliyasema hapa karibuni.
 
Wanasiasa wanatufanya mabwege sana.

Sioni jipya zaidi ya uroho wa madaraka tu.Wale tuliowachukia na waliounda mfumo huu dhaifu na wa kimagumashi ndio hao leo wanaokuja kujidai wanasaidia mabadiliko.

Wale wale waliotupigia na kutuulia ndugu zetu leo hii wanajidai wanasaidia ukombozi.

Hii ni big joke yaani ni kama vile Netanyahu aungane na Abass ili kuwakomboa wapalestina.

Ndio maana watanzania waliukataa mfumo wa vyama vingi kwani wanasiasa wetu ni wasanii.

Ndio maana nchi ilikuwa inayumba kisa kuna vikundi ndani ya ccm venye uroho wa madaraka.

Dawa yao ni kuwatosa tu.

nimeamua kustaafu siasa rasmi...maana nikiendelea miaka miwili ijayo nitakuwa chizi kamili...
Nimea
 
Hawa jamaa wanatufanya wananchi kama mazezeta kabisa wakati tumesoma na elimu zetu sasa hatudanganyiki tunabaki hukohuko ccm maana wametimuliwa CCM kwajili ya ufisadi wao leo wanajifanya eti ni wema na wanataka kuwasaidia kumbe wanataka ulaji kwa mara nyingine nawaomba twendeni leo jangwani saa tano tukasikilize sera bora tuachane na ukawa wasaka tonge mungu ibariki ccm mungu bariki dr magufuli.#HAPAKAZITU
 
Wanasiasa wanatufanya mabwege sana.

Sioni jipya zaidi ya uroho wa madaraka tu.Wale tuliowachukia na waliounda mfumo huu dhaifu na wa kimagumashi ndio hao leo wanaokuja kujidai wanasaidia mabadiliko.

Wale wale waliotupigia na kutuulia ndugu zetu leo hii wanajidai wanasaidia ukombozi.

Hii ni big joke yaani ni kama vile Netanyahu aungane na Abass ili kuwakomboa wapalestina.

Ndio maana watanzania waliukataa mfumo wa vyama vingi kwani wanasiasa wetu ni wasanii.

Ndio maana nchi ilikuwa inayumba kisa kuna vikundi ndani ya ccm venye uroho wa madaraka.

Dawa yao ni kuwatosa tu.

Mfanya biashara akiona biashara haimpi faida anayotaka huwa anaacha na kuhamia biashara nyingine...ila kama faida ipo na anaona haitoshi atafanya tu kubadili wateja. wasaka tonge ndo wanaotuharibia siasa
 
Lengo la kwanza ni kupiga chini hili limbuyu, hayo mengine baadae mbele ya safari na Mungu anatusaidia...... Mkuu watanzania wanataka mabadiliko ambayo kiuhalisia ndani ya CCM yameshindikana......

Ndugu amka naona bado umelala fofofo hata hujitambui huyu mtu alie kuharibia nchi yako na kutumia pesa zako leo anakuja kwa upande wa pili akidai ni msafi, hata mabadiriko hayako kihivyo bora baki na ccm tu na uchague magufuli ambae ni mpenda kazi naamini atatufanikisha watanzania #HAPAKAZITU
 
Mimi nataka niseme kitu kimoja, nchi nyingi za kiafrika zimekuwa zikipata tabu sana kutokana na mifumo ya vyama vingi ambayo tumekubali kuipokea, na ndani yake humo pametokea watu miongoni mwetu wanatumia fursa hiyo kujinufaisha kwa kuanzisha vyama vya siasa na kuweka humo watu ovyo, kwa lengo la kutuharibia utaratibu mzuri wa vyama vilivyo madarakani. Mfano mzuri ni pale libya, ndg gadafi watu wake walikua katika hali nzuri, lakini kwa ujinga wao wa kutaka kujarib hivi sasa wanaishi maisha ambayo hata mtanzania wa hali ya chini ana afadhali. Tuwe makini, kujaribu jaribu hakufai. Mimi naridhika na mfumo uliopo madarakani, na kura yangu nampa magufuli, na ccm iendelee kutawala.
 
Aiseee!! Kweli Tanzania bila UKAWA inawezekana.
 
Ndugu amka naona bado umelala fofofo hata hujitambui huyu mtu alie kuharibia nchi yako na kutumia pesa zako leo anakuja kwa upande wa pili akidai ni msafi, hata mabadiriko hayako kihivyo bora baki na ccm tu na uchague magufuli ambae ni mpenda kazi naamini atatufanikisha watanzania #HAPAKAZITU

ha ha ha kwa mfumo upi? au ndio huo wa mtindo wa rimoti then controller ni wengine!!! Magufuli anatosha kuwa waziri lakini katu hajatosha na hatoshi kuwa rais wa nchi hii na hili nitalisimamia siku zote.
 
Ndugu amka naona bado umelala fofofo hata hujitambui huyu mtu alie kuharibia nchi yako na kutumia pesa zako leo anakuja kwa upande wa pili akidai ni msafi, hata mabadiriko hayako kihivyo bora baki na ccm tu na uchague magufuli ambae ni mpenda kazi naamini atatufanikisha watanzania #HAPAKAZITU

Umechelewa sana Mkuu, tumeshafanya maamuzi tayari!
 
Aiseee!! Kweli Tanzania bila UKAWA inawezekana.

Wote walihudumu katika nafasi ya waziri Mkuu Nani asiyefahamu sumaye kesi ya Rada na mikataba ya mere meta na Tangold alikuwepo au sisi ni wepesi wa kusahau zimwi likujualo halikukuli likakumaliza Zinduka mtanzania
 
Muulize huhuru kenyata kama mfumo ni uleule......aliouacha baba yake au?????? Ccm out!!!!!!!
 
mfumo sio uleule..
kuna tofauti kati ya nchi kutawaliwa na chama kimoja na maamuzi kua ya chama kimoja..
UKAWA ni mfumo wa kisiasa wenye vyama vingi vyenye mchanganyiko wa wanachama wa vyama vingi..
maamuzi hapa ni ya vyama vingi sio chama kimoja..
na hata wizi hapa huwa ni vigumu cause hawatoaminiana na wanaweza kuogopana hivyo kunaweza kujenga uadilifu na uchapa kazi.
 
Leo tunaaminishwa tatizo si mtu ila tatizo ni mfumo,tunaambiwa EL alikua fisadi,mla rushwa,mnyonyaji na muhujumu uchumi sababu ya mfumo.Huku tukiendelea kuona walewale waliotoka kwenye mfumo mbovu wakiendelea kumiminika kuandaa unaoitwa mfumo thabiti.Tena hawafuati chama ila wanafuata madaraka.
Inashangaza kuhama kwao kwa masharti.
"mimi nakuja ila nipeperushe bendera,au mimi nakuja ila tukishinda niwe PM".
Ni dhahiri kwa wana UKAWA kumuachia EL rungu awasaidie kuwapeleka magogoni wenyewe wameshindwa.Nidhahiri huwezi taka msaada kwa kitu ambacho wewe unakiweza.
Mwanzo tulizungumza mtu mmoja EL lakini sasa ni kundi la watu tena wenye tabia zakufanana,
Ni kweli mtu mmoja hawezi kukamilisha mfumo kwani mfumo unahitaji muunganiko wa watu,
Lakini sasa si EL pekeyake tena,kila uchao tunashuhudia watu kutoka kwenye unaoitwa mfumo mbovu kuja UKAWA hivyo kwa wingi wao wata play part kubwa kukamilisha mfumo,
Ikumbukwe pia ushahidi wakimaabara(DNA) imeonesha EL ufisadi upo kwenye damu,
Kama hivyo ndivyo kwa vyovyote iwavyo kwa nafasi alionayo ndugu EL ambaye tumepata uthibitisho wakimaabara kwamba ufisadi upo kwenye damu tutarajie mfumo uleule unaopigiwa kilele.
Ni wendawazimu watu waliohusika kwa kiwango kikubwa kuandaa mfumo unaoitwa Mbovu waje kutuletea mfumo thabiti kwa hili UKAWA mnatuhadaa wananchi na hapa ndipo shaka inapokuja kwamba mwenyekiti ameshadaka mshiko na kukiuza chama kwa mafisadi huku wengine tukiendelea kukaririshwa habari za mfumo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom