Mfumo ule ule unataka kurudi kupitia UKAWA!

Mfumo ule ule unataka kurudi kupitia UKAWA!

Leo tunaaminishwa tatizo si mtu ila tatizo ni mfumo,tunaambiwa EL alikua fisadi,mla rushwa,mnyonyaji na muhujumu uchumi sababu ya mfumo.Huku tukiendelea kuona walewale waliotoka kwenye mfumo mbovu wakiendelea kumiminika kuandaa unaoitwa mfumo thabiti.Tena hawafuati chama ila wanafuata madaraka.
Inashangaza kuhama kwao kwa masharti.
"mimi nakuja ila nipeperushe bendera,au mimi nakuja ila tukishinda niwe PM".
Ni dhahiri kwa wana UKAWA kumuachia EL rungu awasaidie kuwapeleka magogoni wenyewe wameshindwa.Nidhahiri huwezi taka msaada kwa kitu ambacho wewe unakiweza.
Mwanzo tulizungumza mtu mmoja EL lakini sasa ni kundi la watu tena wenye tabia zakufanana,
Ni kweli mtu mmoja hawezi kukamilisha mfumo kwani mfumo unahitaji muunganiko wa watu,
Lakini sasa si EL pekeyake tena,kila uchao tunashuhudia watu kutoka kwenye unaoitwa mfumo mbovu kuja UKAWA hivyo kwa wingi wao wata play part kubwa kukamilisha mfumo,
Ikumbukwe pia ushahidi wakimaabara(DNA) imeonesha EL ufisadi upo kwenye damu,
Kama hivyo ndivyo kwa vyovyote iwavyo kwa nafasi alionayo ndugu EL ambaye tumepata uthibitisho wakimaabara kwamba ufisadi upo kwenye damu tutarajie mfumo uleule unaopigiwa kilele.
Ni wendawazimu watu waliohusika kwa kiwango kikubwa kuandaa mfumo unaoitwa Mbovu waje kutuletea mfumo thabiti kwa hili UKAWA mnatuhadaa wananchi na hapa ndipo shaka inapokuja kwamba mwenyekiti ameshadaka mshiko na kukiuza chama kwa mafisadi huku wengine tukiendelea kukaririshwa habari za mfumo.
Mkuu yaani unataka kusema huoni kabisa tofauti ya chadema na ccm?hivi kinachomtofautisha mkiristo na mwislam huwa ni nn?Pole my brother naona ccm imekuharibu sana katika harakati zake za kuharibu nchi yetu.
 
Wanasiasa wanatufanya mabwege sana.Sioni jipya zaidi ya uroho wa madaraka tu.Wale tuliowachukia na waliounda mfumo huu dhaifu na wa kimagumashi ndio hao leo wanaokuja kujidai wanasaidia mabadiliko.Wale wale waliotupigia na kutuulia ndugu zetu leo hii wanajidai wanasaidia ukombozi.Hii ni big joke yaani ni kama vile Netanyahu aungane na Abass ili kuwakomboa wapalestina.Ndio maana watanzania waliukataa mfumo wa vyama vingi kwani wanasiasa wetu ni wasanii.Ndio maana nchi ilikuwa inayumba kisa kuna vikundi ndani ya ccm venye uroho wa madaraka.Dawa yao ni kuwatosa tu.
Uroho wa madaraka siku zote ndio unaopelekea machafuko ya kisiasa katika nchi nyingi na kuondosha amani ya nchi, CCM imekuwa mstari wa mbele kupigania uwepo wa amani kwa miaka zaidi ya hamsini sasa. Japo wengi hawajui ni kwa nini CCM inafanya hivyo, ningewaomba tu wasiojua kwa nini CCM inafanya hayo yote, watembelee tu nchi za jirani hapo CONGO, RWANDA NA BURUNDI, MISRI, LIBYA n.k wajionee, halafu watajua umuhimu wa kudumisha amani. Ninathamini amani, na ninathamini CCM, MAGUFULI na WATANZANIA. Hivyo basi sioni haja ya kutokifanya chama cha mapinduzi kuwa madarakani.
 
Nadhani kwa hili kosa hata sio mfumo kuwa ule ule. Ni kuwa watu wale wale waliokuwa na makashfa kibao ya ubadhirifu wa mali za uma wametoka CCM na kuhamia vyama pinzani.
Kutoka kwao hakuwasafishi na lolote kwani walikuwa wachafu hata walipokuwa ndani ya CCM...kudhani kuwa kuhamia upinzani ni wao kuwa wasafi ni kujidanganya. Sanasana wanacghotaka kukifanya ni kujijengea na kujihakikishia wana misingi imara ya kushika uongozi wa juu wa nchi ili watakapoingia madarakani wawe ni watu wenye falsafa moja ya wizi, udanganyifu, unyang'anyi, uporaji na kudhulumu watu wa hali ya chini kwa kujilimbikizia wao tu, kama sisi wengine walala hoi hatuna haki. Yaani tuwachague sisi wenyewe na watuadhibu pia kwa kufanya hivyo.
 
Nilipokuwa kwenye daladala leo asubuhi kumezuka mjadala mkali baada ya kusikika Katibu Mkuu wa CCM akizungumza kwenye redio ya Clouds kuhusu ufunguzi wa Kampeni na namna Chama chao kilivyojipanga kwenye kampeni ya Uchaguzi mkuu.

Mjadala huo ulikuwa na maudhui ya watu kukata tamaa ya Maisha, kwa maana baada ya Katibu Mkuu kumaliza kuongea watu walisikika wakisema kuwa hawa jamaa hawana jipya, tumewachoka. Lakini wengine wakauliza sasa tunaenda wapi maana UKAWA ndio kichaka kipya cha wanaCCM waliotufikisha hapa. Ndio wanaokwenda kuchukua nafasi na kutaka wapewe nafasi za kugombea na kudictate maamuzi ya UKAWA.

Watanzania wanataka mabadiliko, wamechoka na CCM lakini UKAWA wamewachosha zaidi, maana wamewakatisha tamaa, matumaini ya Watanzania kuona Uongozi mpya wenye hulka na matendo tofauti yamepotea kabisa..wanakuja watu wale wale waliotufikisha hapa na wao wakisema MTUAMINI sisi UMEME utawaka, AFYA itakuwa BORA, watoto WATASOMA bure na kila ahadi tamu, wakati walisema hivyo hivyo wakiwa CCM na hakuna walichofanya.

Wananchi wamechanganyikiwa, WANAAMINI kabisa kuwa LOWASSA ni Mwizi, ni FISADI aliyekubuhu, lakini wanaambiwa kuwa FISADI huyo kwa sasa ndie MUSSA atakayetukomboa.

Wanapata Mashaka kuona Viongozi waliodumu kwenye Serikali kama watendaji wakuu, yaani Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya tatu aliyeshiriki mauaji ya Wazanzibar mwaka 2001, Mauaji ya Mwembechai mwaka 1998 na kila ovu, mtu mwenye kashfa ya UFISADI na kujimilikisha maelfu ya hekari za ardhi leo anapokelewa UKAWA kama mkombozi wa WATANZANIA.

Watanzania wanaona kuwa zipo chupa mbili za SUMU, na moja imeandikwa SUMU na NYINGINE imeandikwa MAJI....

Chupa yeyote utakayokunywa hauna SALAMA.,lazima UMAUTI ukukute...!
 
Chama cha mapinduzi kina mifumo mizuri ya uongozi na viongozi wake ni waadilifu. Magufuli ndo mwenyewe. Jangwani muda huu mtasioma namba
 
Mkuu yaani unataka kusema huoni kabisa tofauti ya chadema na ccm?hivi kinachomtofautisha mkiristo na mwislam huwa ni nn?Pole my brother naona ccm imekuharibu sana katika harakati zake za kuharibu nchi yetu.

Kimsingi huwezi kusema flani ni mrefu kama pasingekuepo na mfupi.Hapa namaanisha tunahitaji kumpata wakumlinganishia ndipo tutambue urefu au ufupi wa mmoja wao.
Tunaposema Husein Bolt ni bingwa wa dunia sababu wapo tuliomlinganisha naye ila kama angekimbia peke yake tusingepata majibu,
Kwaujumla namaanisha upo ulazima wa siku moja upinzani ushike dola ili tuweze kupima kati ya hawa wawili hili ni muhimu,
Tatizo hapa ni kutumia mtu yuleyule ambaye tunamuhamisha kutoka CCM kuja ukawa.
Kama alipo kua CCM tulimpata navurefu wa 30M atakapokuja UKAWA hawezi ongezeka chochote.
Kwakumalizia hapa tunachofanya ni kuhamisha UFISADI kutoka CCM kuja ukawa jambo ambalo si lengo.
 
Magufuli Hakika anatoshaaaa hao wengine tunawaacha wanaangaiko sasa Kutafuta mgombea mwisho wao October.... Ccm itawaburuza chang'anyang'a... Chapachapa ndembendembe
 
Acheni upuuzi nyie watu. Sumaye alikuwa mbunge wa Hanang kwa miaka 15. Lowassa alikuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM na Kamati kuu kwa zaidi ya miaka kumi. Wote wazeee wana miaka sitini na kitu. Wamelelewa CCM. Utakuwa mwenye AKILI NDOGO sana kama ukiamini mabadiliko yataletwa na Wazee MAKAPI ya CCM.

AMKENI jama.
 
Wanasiasa wanatufanya mabwege sana.

Sioni jipya zaidi ya uroho wa madaraka tu.Wale tuliowachukia na waliounda mfumo huu dhaifu na wa kimagumashi ndio hao leo wanaokuja kujidai wanasaidia mabadiliko.

Wale wale waliotupigia na kutuulia ndugu zetu leo hii wanajidai wanasaidia ukombozi.

Hii ni big joke yaani ni kama vile Netanyahu aungane na Abass ili kuwakomboa wapalestina.

Ndio maana watanzania waliukataa mfumo wa vyama vingi kwani wanasiasa wetu ni wasanii.

Ndio maana nchi ilikuwa inayumba kisa kuna vikundi ndani ya ccm venye uroho wa madaraka.

Dawa yao ni kuwatosa tu.

wangekua wa maana sana kama wangehamia upande wa pili tangu kitambo, leo hii ni dhahiri kabisa wanaishu zao binafsi and we all know that.....tusidanganyike
 
  • Thanks
Reactions: nao
Leo tunaaminishwa tatizo si mtu ila tatizo ni mfumo,tunaambiwa EL alikua fisadi,mla rushwa,mnyonyaji na muhujumu uchumi sababu ya mfumo.Huku tukiendelea kuona walewale waliotoka kwenye mfumo mbovu wakiendelea kumiminika kuandaa unaoitwa mfumo thabiti.Tena hawafuati chama ila wanafuata madaraka.
Inashangaza kuhama kwao kwa masharti.
"mimi nakuja ila nipeperushe bendera,au mimi nakuja ila tukishinda niwe PM".
Ni dhahiri kwa wana UKAWA kumuachia EL rungu awasaidie kuwapeleka magogoni wenyewe wameshindwa.Nidhahiri huwezi taka msaada kwa kitu ambacho wewe unakiweza.
Mwanzo tulizungumza mtu mmoja EL lakini sasa ni kundi la watu tena wenye tabia zakufanana,
Ni kweli mtu mmoja hawezi kukamilisha mfumo kwani mfumo unahitaji muunganiko wa watu,
Lakini sasa si EL pekeyake tena,kila uchao tunashuhudia watu kutoka kwenye unaoitwa mfumo mbovu kuja UKAWA hivyo kwa wingi wao wata play part kubwa kukamilisha mfumo,
Ikumbukwe pia ushahidi wakimaabara(DNA) imeonesha EL ufisadi upo kwenye damu,
Kama hivyo ndivyo kwa vyovyote iwavyo kwa nafasi alionayo ndugu EL ambaye tumepata uthibitisho wakimaabara kwamba ufisadi upo kwenye damu tutarajie mfumo uleule unaopigiwa kilele.
Ni wendawazimu watu waliohusika kwa kiwango kikubwa kuandaa mfumo unaoitwa Mbovu waje kutuletea mfumo thabiti kwa hili UKAWA mnatuhadaa wananchi na hapa ndipo shaka inapokuja kwamba mwenyekiti ameshadaka mshiko na kukiuza chama kwa mafisadi huku wengine tukiendelea kukaririshwa habari za mfumo.

MKUU kichwa cha habari yako kinatosha kuelewa una maana gani ndiyo maana sikuchukua hata mda kusoma contents zake.
JIBU:
Mzee Mandela alimtumia De Clark kuuzamisha utawala wa makauburu pamaoja na mfumo wake! Watu kama nyie ni wanafiki na wanaotaka kutumia propaganda kuwachanganya watanzania wanaotaka mabadiliko. Watanzania na hasa vijana hawadanganywi na huu UNAFIKI. Labda tafuta santuri nyingine na wala hii haiuziki.
 
Hoja dhaifu mwenyewe dhaifu, je kama ni uroho wa madaraka kwa ccm wanang'ang'ania mdarakan na wako tayari kushinda kwa goli la mkono? Kama si waroho si wawaachie wapinzani? Kama si waroho kwa nn wanatumia police kuangamiza upinzani?
Acha kufikiri kwa makalio kijana.
 
Kubwa ni mfumo kama wangekuwa ndiyo wakwamishaji mbona mgombea urais kateuliwa na nguvu ya MTU mmoja
 
MKUU kichwa cha habari yako kinatosha kuelewa una maana gani ndiyo maana sikuchukua hata mda kusoma contents zake.
JIBU:
Mzee Mandela alimtumia De Clark kuuzamisha utawala wa makauburu pamaoja na mfumo wake! Watu kama nyie ni wanafiki na wanaotaka kutumia propaganda kuwachanganya watanzania wanaotaka mabadiliko. Watanzania na hasa vijana hawadanganywi na huu UNAFIKI. Labda tafuta santuri nyingine na wala hii haiuziki.

Jitambue kijana hakuna maendeleo katika makapi Kapi Daima alinatofauti na bidhaa ya kichina haiwezi kuimili wala kusaidia katika jambo lolote
 
Wanasiasa wanatufanya mabwege sana.

Sioni jipya zaidi ya uroho wa madaraka tu.Wale tuliowachukia na waliounda mfumo huu dhaifu na wa kimagumashi ndio hao leo wanaokuja kujidai wanasaidia mabadiliko.

Wale wale waliotupigia na kutuulia ndugu zetu leo hii wanajidai wanasaidia ukombozi.

Hii ni big joke yaani ni kama vile Netanyahu aungane na Abass ili kuwakomboa wapalestina.

Ndio maana watanzania waliukataa mfumo wa vyama vingi kwani wanasiasa wetu ni wasanii.

Ndio maana nchi ilikuwa inayumba kisa kuna vikundi ndani ya ccm venye uroho wa madaraka.

Dawa yao ni kuwatosa tu.

Yaani hapo ni mtu uangalie unachagua CCM A ama CCM B
 
Waroho wa madaraka na ambao wanatumia kete ya ukanda. Umekaa katika mfumo miaka 30 na ushee leo unakatwa na kusema ccm mbovu.
 
MKUU kichwa cha habari yako kinatosha kuelewa una maana gani ndiyo maana sikuchukua hata mda kusoma contents zake.
JIBU:
Mzee Mandela alimtumia De Clark kuuzamisha utawala wa makauburu pamaoja na mfumo wake! Watu kama nyie ni wanafiki na wanaotaka kutumia propaganda kuwachanganya watanzania wanaotaka mabadiliko. Watanzania na hasa vijana hawadanganywi na huu UNAFIKI. Labda tafuta santuri nyingine na wala hii haiuziki.

October itakapofika utatambua kwamba kumkarisha lowasa ni janga kwa UKAWA.Hakuna mtanzania mpu.mb.av kiasi hicho hata kama tumeitwa kichwa cha mwendawazimu,mtuapishe kwa viapo kwamba EL ni fisadi akiwa CCM halafu mje kutuamisha kwamba mfumo utamfanya awe msafi!!!
 
Unajua maana ya mfumo au unapayuka tu hawa wamekuja kujiunga na mfumo mpya wa kuwatumikia raia sio shetani uko hapo

shetani mbaya kuliko wote ni yule anayewasaliti watu kwa vipande vya shekeli,mbowe amekula shekeli ili awatose wenzie ndio maana humuoni slaa wala lipumba pale ukawa,mbatia amepata nafasi ya mwisho kutafutia ulaji maana bila hii hakuna tena ndoto ya ubunge ila sasa anawaza uwaziri,maalim seif bila shaka hii ndio kete yake ya mwisho na akiikosa ndio jua limezama kwa hiyo aliona ni bora amtose lipumba kuliko kuachia support ya hela ya EL.

na hata kina mnyika ,lissu,mdee,na wapambanaji wengine wako pale ili kutetea ubunge wao maana mwenyekiti amewageuka wakati muda wa mchakato wa ubunge ukiwa umekwisha pita na hivyo isingekuwa rahisi kwao kubishana na mwenyekiti.

lowassa akiupata urais kwa katiba ya tanzania anakuwa ndio kila kitu na hawa ukawa wote wanabaki na chama yeye anakuwa na serikali.....hivyo muelewe katiba inayotumika kwa kuendesha nchi itakuwa ile ile aliyoipigia kura Lowassa na sio ya chadema ya chadema itabaki na mbowe hadi kama Lowassa akiwa na uwezo wa kuanzisha mchakato wa katiba mpya na ikapitishwa.jambo ambalo kwa Lowassa halitawezekana kwani yeye ni mmoja wa watu wanaobanwa na katiba ya warioba.

tafakari
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom