Mfanyabiashara Matei apata ajali na kufariki

Mfanyabiashara Matei apata ajali na kufariki

Wakuu, posti #27 (picha ya 4 kulia gari ikionekana kwa nyuma) imeonyesha moja ya chanzo cha ajali.

Hiyo gari (Mark X 'jipya' tu halafu) ilikuwa inatumia gurudumu la dharura upande wa kulia nyuma. Hili liwekwapo hupaswi kuendesha mwendo mkali. Gari, kawaida, inatakiwa kuwa na gurudumu zinazofanana kote kwa usalama. Katika spidi kuanzia 80kph, gurudumu huongezeka uzito sana na kama zimetofautiana aina na kiwango cha uchakavu, gari huserereshwa upande hivyo dereva kushindwa kulidhibiti. Ninahisi, ndicho kilichowaponza. Ulevi ulichangia kuwasahaulisha kanuni za usalama wa gari.

RIP kina Matei na poleni wafiwa. Watu wengi huangamia kwa kukosa au kukaidi maarifa!!
 
Vifo vingine Ni kuomba mungu aepushie mbali imagine unakufa huku unazini au unakufa umelewa. Rip wote mliofariki.
 
How about airbags?
Wataalam plz fungukeni kuhusu msaada wa airbag maeneo kama haya.
au gari haikua na airbag?
bcoz niliwa kuishuhudia ajari1 SA-SONDTON gari BMW lilipondeka kabisa,but jamaa alitoka na majeraha kidogo sana mpaka nikashangaa.
 
Mkuu, kwa jinsi ilivyokanyagwa hasa hapo kwa dereva, air bag ingepasuka tu.
Inawezekana ilifunguka maana katika hizo picha ya kwanza kabisa juu inaonekana dereva kainamia kitu cheupe.
 
Tujifunze kupitia hizi ajali jamani mwendo kasi ni hatari bora kuchelewa kufika kuliko kuwahi mochwari kuna sifa za kijinga sana eti unakuta watu wanasifiana kwa kitumia muda mfupi kwa safari zao mathalani dar moro au moro dom ati masaa mawili wengine saa na nusu sifa za kijinga na kipuuzi sana hizi haya oneni hao sijui nao walikuwa kwenye haya makundi
 
Wakuu, posti #27 (picha ya 4 kulia gari ikionekana kwa nyuma) imeonyesha moja ya chanzo cha ajali.

Hiyo gari (Mark X 'jipya' tu halafu) ilikuwa inatumia gurudumu la dharura upande wa kulia nyuma. Hili liwekwapo hupaswi kuendesha mwendo mkali. Gari, kawaida, inatakiwa kuwa na gurudumu zinazofanana kote kwa usalama. Katika spidi kuanzia 80kph, gurudumu huongezeka uzito sana na kama zimetofautiana aina na kiwango cha uchakavu, gari huserereshwa upande hivyo dereva kushindwa kulidhibiti. Ninahisi, ndicho kilichowaponza. Ulevi ulichangia kuwasahaulisha kanuni za usalama wa gari.

RIP kina Matei na poleni wafiwa. Watu wengi huangamia kwa kukosa au kukaidi maarifa!!

...asante mkuu kwa kutupatia maarifa.
 
Pole zao ila jamani tuheshimu sheria za udereva, mwendo kazi ukiwa umelewa ni hatari sana
 
...asante mkuu kwa kutupatia maarifa.

Tuko pamoja kbm. Wengi gari wanalijua kunyonga tu usukani baada ya kuliwasha... Vile vipingi vya BP vilisaidia sana ila kwa sasa Puma ndo hivyo tena...
 
Walienda kumnzika mwenzao moro wakati wana rudi ndio na wao wamepata ajali hata marehemu waliokuwa wamemsindikiza nae alipata ajali na kufariki
 
Kuna taarifa kuwa katika ajali hiyo pia amefariki Wakili wa kujitegemea ambaye pia ni mwalimu wa Business Law wa Chuo Kikuu cha St. John's hapo Dodoma Bwana Joshua Oguda, mwenye taarifa zaidi atujuze tafadhali

Ni part time SJUT
 
nikajua bilionea mwengine wa Arusha ametutoka
 
Daaah!, masikini Mheshimiwa Wakili Bwana Oguda, huyu ndugu alikuwa ana dharau na mnyanyasaji mkubwa wa wanafunzi pale St. John's University hasa akina dada wamenyanyasika sana kijinsia na huyu Mungu mtu!.

Hata hivo watanzania hatuna tabia wala tamaduni ya kufurahia matatizo ya binadamu wenzetu.

Nilipokuwa Rais wa Serikali ya wanafunzi hapo chuoni ndugu Oguda ulisimama kidete kutengeneza fitna ili nifukuzwe Chuo eti kwa kuwa nilipinga sana tabia yako ya kuwaonea wanafunzi hasa wa kike na mpaka Israel anainyemelea roho yako leo nina kesi na Chuo hicho ambapo wewe kwa kiherehere chako ndo wakili unaesaini viapo vya chuo!, natamani upone haraka ili ushuhudie nitakavo wahenyesha hapo Mahakama Kuu ya Dodoma.

Mungu akunusuru Wakili Msomi Joshua Oguda, nimeguswa na kusikitishwa sana kama binadamu kwa kweli nakuombea upone haraka lakini ujue dunia ni mapito mheshimiwa hivo si uungwana kuharibu ndoto za watoto wa watanzania wenzio!

Kumbe ulikuwa Raisi wa wanafunzi?
 
Marehemu na wenzake walikuwa wanatoka Morogoro kwenye party flan hivi na walikua wamelewa vizur tuu, na Matei Lounge mwenyewe ndiyo alikuwa anadrive kwa mbwembwe huku akishndana na fuso...

Inasemekana ulikuwa ni mwendo hatari kiasi kwamba gari ilipinduka na Fuso likaja kwa juu. Mmoja wa abiria alikuwa ni Wakili Joshua Oguda ambaye amefariki masaa machache baada ya mwenzie kupumzishwa motuary ya General Hospital Dodoma.

Sio kwenye pati ni msibani mwenzao amefariki kwao moro
 
Back
Top Bottom