Mfahamu mwanariadha Feyisa Lilesa aliyeuangusha utawala wa Dictator Haile Maryam

py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,471
4,424
Mwaka 2016 kwenye mashindano ya olimpics yaliyofanyika Rio nchini Brazil mwana riadha kutoka Ethiopia Feyisa lilesa alifanya jambo la kishujaa na litakalokaa kwenye kumbu kumbu kwa jamii ya wa oromo waishio Ethiopia.Feyisa amekuwa stepping stone towards the liberation of oromia from the suppression of Dictator Haile Maryam


Binafsi ni mpenzi wa mbio za riadha haswa za kimataifa na kwenye olimpic nilikuwa nafuatilia riadha pamoja na mpira basi...kwenye mbio ndefu za marathon zinazochukua takriban masaa 2 ,mwana riadha kipchoge alikuwa anaongoza huku Feyisa lilesa kutoka Ethiopia akifuatia wa pili lkn kipchoge alimuacha kwa takriban metre 40-60 Feyisa kama sijakosea kwa kumbukumbu zangu.Mwana riadha kipchoge alimaliza akishika nafasi ya kwanza huku mwana riadha Feyisa akifuatia wakati Feyisa anakaribia mstari wa kuhitimisha mbio alikuwa anaonyesha ishara kama ya X kwa kutumia mikono yake watu wengi hawakuielewa alama ile isipokuwa wa oromia.

e50da1d2156baf67661ab7da45ca760f.jpg


98e7445dec15f48f2c84a716ee1df4bc.jpg


Alitoa ishara hii kuiambia dunia kuwa wa oromia watu wa jamii yake wanateseka Ethiopia,serikali ya Dictator Haile maryam imewaua mamia kama sio maelfu ya kaka ,baba,Dada zake na mamia ya ndugu zake wamefungwa jela kwasababu ya kisiasa na freedom of speech

Baada ya Feyisa kupewa medali ya silver bado aliendelea kutoa ishara ile na ndani ya dakika chache Twitter iliwaka moto na hashtag ya freeOromo ,Feyisa aligoma kurudi kwao Ethiopia akidai Waziri mkuu Haile maryam atamuua kama sio kukamatwa na kupelekwa jela hivyo akabaki Rio ,wana oromia duniani kote walifanya fundraising na kufikisha dollar 500,000 apatiwe lelisa na aombe hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa nchi yeyote ile


Feyisa alikuwa shujaa kupitia olimpics aliujulisha dunia mateso ya kaka,Dada,mama,baba zake wanazozipata huko Ethiopia


Media zote ,Twiiter mada ilikuwa Oromia,Ethiopia na Haile maryam, jumuiya za kimataifa wakataka kwenda kuangalia hali ya kisiasa nchini Ethiopia mwanzo Haile maryam alikataa kwa kuaema Ethiopia ni nchi huru hivyo hatoruhusu ila jumuiya za kimataifa zilivyoshinikiza Haile maryam hakuwa na Jinsi

Wafungwa wa kisiasa mamia na mamia wameachiwa na Dictator Haile maryam kwa shinikizo ya jumuiya ya kimataifa na shujaa akiwa Feyisa lilesa

NB:Oromo ni jamii inayokandamizwa sana Ethiopia ,Amharic ndio wanaopendelewa na hawa oromo wamepigwa sana ndio hawa tunaowaona wakipita Tanzania kwa makundi kwa makundi kwenye malori kukimbia makucha ya Dictator Haile maryam
47bdd7dcbbbcf4a9b8523e890e4139f9.jpg
 
Sasa hawa wanaopita kwetu ni bora kuwapa hifadhi
Ukiona binadamu anakimbia kwao mhurumie sana, ujue amepatwa na misiba ya kila aina
Anyway sio kwamba sijaelewa mada ila hili limenigusa zaidi
 
Back
Top Bottom