Kumbukizi muhimu ya mwanariadha John Steven Akhwari

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
375,861
Reaction score
870,823
John Steven Akhwari ni mwanariadha mstaafu. Alizaliwa mwaka 1938 kule Mbulu- Mkoani Manyara. Aliiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Olimpic mwaka 1968 nchini Mexico, katika mashindano ya riadha ya kilomita 42. Washiriki walikuwa 75, lakini waliomaliza shindano ni 57 pekee, huku John Steven Akhwari akimaliza wa mwisho kabisa.
Kwa nini alimaliza wa mwisho? Baada ya mbio kuanza, walipofika kilomita ya 19, mshiriki mojawapo alimparamia, kumsukuma na kuanguka vibaya mno. Aliumia begani, na goti la mguu wa kulia lilitenguka. Gari la huduma ya kwanza lilimfikia na kumpa matibabu, akaweza kusimama tena na kuendelea na riadha.
Umaarufu wake duniani . Watu waliomhudumia walimlazimisha kuaihirisha shindano na apande kwenye gari lakini alikataa katakata. Aliendelea na riadha huku akichechemea. Alifanikiwa kumaliza kilomita zote 42, jioni ya saa 1 kwa saa za Mexico. Watu wachache waliokuwa wamebakia uwanjani walimshangilia sana.
Mwishoni kabisa, waandishi wa habari walimuuliza, Kwa nini aliendela kukimbia ili hali ameumia kiasi hicho? Aliwaambia Nchi yangu Tanzania haikunituma maili 5000 kuja Mexico kuanza hili shindano bali walinituma kumaliza shindano.
Katika mashindano ya Olimpic na mpaka hivi leo Bwana John Stephen Akhwari anatambulika kama
'The Greatest Last- Place Finish Ever' . Japo hakushinda tuzo yoyote lakini ameonyesha uvumilivu, ujasiri na wenzetu wamekuwa wakimtumia kufundishia watoto na vijana wao kwamba they must struggle to finish the race, not just to start it.
Kwa bahati mbaya sana, watanzania walio wengi hawamjui. Huyu ni mfano wa kuigwa, ilistahili kauli yake hiyo ingekuwa nukuu muhimu kwa vijana wetu.
John Stephen Akhwari - Inspirational Story - Athslife
John Stephen Akhwari - Wikipedia

Heshima kubwa kwake
FB_IMG_1683391619913.jpg
FB_IMG_1683391625198.jpg
 
Najana nilikuwa Babati Olimpic A kumsapoti huyu Shujaa....

Hawa mashujaa kuna umuhimu sana Taifa kuwatumia kutengeneza future za vizazi vyetu....
 
kwa hiy huyu Shujaa anapatikana babati ningependa kuonana naye. Hii ni moja ya tunu za taifa yaani ukienda nje ya nchi somo lolote la Perseverance ( yaani kuvumilia mpaka mwisho) mzee ni mfano hai unaotumwa kuwa jinsi gani binadamu anaweza kushinda vipigamizi na uzuri kuna video
 
Ila nabii hatambuliki kwao
 
Juzi kuna mbongo kafanya vizuri Boston marathon
Naona watu huku,viongozi wako kimyaa hawana habari naye
[emoji1]
Tuko bize na wakina mandonga mwijaku babalevel wapiga kelele

Ova
 
Sifa kwa taifa lakini habari zake hazijapewa kipaumbele kabisa
 
John Stephen tulikuwa tunasoma wote Kurasini Primary School. Shule ya Salvatorian Sisters. Siku hizi siyo shule ya msingi tena. Imechukuliwa na Kanisa Katoliki. In fact,ndio HQ ya Kanisa Katoliki Tanzania.
Pale ndipo John Steven alipoinuka kuwa international star.
No coach,no nothing. It was just his personnal initiative. It was what I was discussing with him the last time I saw him. Nilikuwa nashangaa kwamba wale Masista walikuwa wanafundisha light athletics but he became a marathon runner.
 
kwa hiy huyu Shujaa anapatikana babati ningependa kuonana naye. Hii ni moja ya tunu za taifa yaani ukienda nje ya nchi somo lolote la Perseverance ( yaani kuvumilia mpaka mwisho) mzee ni mfano hai unaotumwa kuwa jinsi gani binadamu anaweza kushinda vipigamizi na uzuri kuna video
Karibu Mkuu Babati ukifika ulizia tu Olympic A Olympic B mpaka Chaa
 
John Stephen tulikuwa tunasoma wote Kurasini Primary School. Shule ya Salvatorian Sisters. Siku hizi siyo shule ya msingi tena. Imechukuliwa na Kanisa Katoliki. In fact,ndio HQ ya Kanisa Katoliki Tanzania.
Pale ndipo John Steven alipoinuka kuwa international star.
No coach,no nothing. It was just his personnal initiative. It was what I was discussing with him the last time I saw him. Nilikuwa nashangaa kwamba wale Masista walikuwa wanafundisha light athletics but he became a marathon runner.
Mkuu sorry ni ile Kurasini shule ya msingi ya Serikali karibu na kanisa Katoliki?
 
Back
Top Bottom