Ethiopia imeshachelewa kuzuia Somalia kuibuka kama taifa lenye nguvu za ushawishi wa Kisiasa na Uchumi kwa pembe ya Afrika

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,056
49,743
Hivi karibuni Ethiopia imeanza kufanya hujuma Kwa Somalia Kwa kuingia makubaliano haramu ya kuimega Somalia ilimradi wapate Bandari.

Suala la Bandari ni kisingizio tuu ila lengo kubwa ni kuizuia Somalia kuibuka kuwa Taifa lenye ushawishi wa Kisiasa na kiuchumi Kwa Pembe ya Afrika ambapo Ethiopia ilitawala Kwa miaka Mingi.

Mizozo ya Wenyewe Kwa wenyewe ndani ya Ethiopia na kuimarika Kwa Uongozi wa Mogadishu kumeitisha Ethiopia na kuanza kuwa na hofu ikizingatiwa kwamba Kuna jamii kubwa sana ya Wasomali huko Ethiopia.

Hivi karibuni Somalia ilifitiwa deni lake lote na Wadaiwa na ikaondolewa vikwazo vya kununua silaha.On top of that ikajiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo kutumia salamu huko Addis kwamba Hatimaye Somalia Inaanza kusimama tena.
Screenshot_20240104-065308.jpg

Uongozi wa Sasa wa Somalia umeweza pakubwa kupambana na Al Shabaab kiasi ya kuwafurahisha Jumuiya ya Kimataifa ikiwemo Marekani.Kwa muelekeo Mpya huenda USA akaelekeza Nguvu Mogadishu badala ya Ethiopia.

Ikumbukwe kwamba Somalia ipo kwenye eneo la kimkakati kiusalama hasa kwenye biashara na Ina Rasilimali nyingi ambazo hazijatumika kutokana nazozo wa vita wa miaka mingi.
Screenshot_20240104-065223.jpg

My Take
Kusimama tena Kwa Somalia ni habari njema sana Kwa Afrika.
Screenshot_20240104-065334.jpg
 
Somalia haiaminiki kwa lolote lile, Ethiopia tayari ana makubaliano na Somaliland kutumia bandari yake, na pia kuweka kituo cha kijeshi.

Somaliland inahitaji kuwa huru, na imekuwa imara kiusalama kwa muda mrefu, ikiwa na fedha yake.

Somalia haiwezi kukohoa mbele ya Ethiopia.

Pia Ethiopia ana option ya kutumia mlango wa bandari wa Djibout ambako kuna reli ya moja kwa moja kwenda Ethiopia.

Ethiopia, baada ya kutemgana na Eritrea, ilikosa njia ya moja kwa moja kwenda baharini.
 
Somaliland ndio nani? Hiyo ni Mali ya Somalia
 
Duu umeandika ujinga gani huu

Hizi takataka zinazofuga magaidi ndio zijilinganishe na Ethiopia?

Somalia anahitaji miaka 50 kumfikia ethiopia

Madhara ya kumpigania mud
 
Hivi karibuni Ethiopia imeanza kufanya hujuma Kwa Somalia Kwa kuingia makubaliano haramu ya kuimega Somalia ilimradi wapate Bandari.

Suala la Bandari ni kisingizio tuu ila lengo kubwa ni kuizuia Somalia kuibuka kuwa Taifa lenye ushawishi wa Kisiasa na kiuchumi Kwa Pembe ya Afrika ambapo Ethiopia ilitawala Kwa miaka Mingi.

Mizozo ya Wenyewe Kwa wenyewe ndani ya Ethiopia na kuimarika Kwa Uongozi wa Mogadishu kumeitisha Ethiopia na kuanza kuwa na hofu ikizingatiwa kwamba Kuna jamii kubwa sana ya Wasomali huko Ethiopia.

Hivi karibuni Somalia ilifitiwa deni lake lote na Wadaiwa na ikaondolewa vikwazo vya kununua silaha.On top of that ikajiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo kutumia salamu huko Addis kwamba Hatimaye Somalia Inaanza kusimama tena.
View attachment 2862461

Uongozi wa Sasa wa Somalia umeweza pakubwa kupambana na Al Shabaab kiasi ya kuwafurahisha Jumuiya ya Kimataifa ikiwemo Marekani.Kwa muelekeo Mpya huenda USA akaelekeza Nguvu Mogadishu badala ya Ethiopia.

Ikumbukwe kwamba Somalia ipo kwenye eneo la kimkakati kiusalama hasa kwenye biashara na Ina Rasilimali nyingi ambazo hazijatumika kutokana nazozo wa vita wa miaka mingi.
View attachment 2862460

My Take
Kusimama tena Kwa Somalia ni habari njema sana Kwa Afrika.
View attachment 2862462

nadhani unashida kwene kutafusiri kingereza wanavosema new powered somalia wanamaanisha nchi inayopona taaratibu kutoka kwene machafuko!!

hiyo nguvu na ushawishi imevitoa wap wazee walojaa siasa za ukoo na ugaidi
 
Somaliland ndio nani? Hiyo ni Mali ya Somalia

unaijua Historia ya somaliland au unaongozwa na mihemuko!!

Somaliland ilitawaliwa na british
Somalia na italy

baada ya vita ya pili itali ikatawala zote somaliland na somalia ndo mwanzo wa kupata uhuru pamoja lakini hawa watu wapo tofauti kijamiii na kimtazamo wanachoshare n kabila tu
 
Back
Top Bottom