Meya wa Kinondoni afanya ufisadi

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,185
56
Naona gazeti la fisadi Rostam Azizi limeanza kuanika ufisadi wa mafisadi watoto. Ufisadi huanza kidogo kidogo na baadaye kufikia hatua ya kuiba mabilioni na kuanza kuua watu.

Masahihisho tu kwa nyie waandishi, hakuna kitu kinaitwa jiji la Florida hapa Marekani.



http://www.newhabari.com/mtanzania/habari.php?id=2238&section=kitaifa
 
Kama kweli huyu ni kiongozi mwadilifu, angejiuzulu mara moja. Sababu ziko nyingi lakini kubwa zaidi ni kutumia vibaya madaraka yake kwa sababu binafsi (kuuza viwanja, kuwafagilia wanawe kwenda Marekani kwa fedha za serikali pasipo na ustahili, kutumia safari ya kiserikali kibiashara). Yaani ni kweli, ufisadi huanza kidogo kidogo kama hivi na Londa afanzwe fundisho!!
 
Hii inchi inanuka rushwa in all departments!

Inaelekew Watz sasa wanaanza kuzoea wala rushwa!

Kwa nini huyu jamaa asijiuzulu?
 

Wewe kama Kikwete mwenyewe anafanya wizi na ufisadi hadharani basi unategemea mameya wake wafanye nini!
 
PCCB wanasubiri nini? kupewa amri na Kikwete ya kuunda tume ya uchunguzi? TZ inachosha kwa kweli!
 
Meya anachaguliwa na wananchi. Huyo sio Meya wa Kikwete ni Meya wa wakazi wa Kinondoni.

Richard alishinda big brother na ccm wakamuandalia maandamano na kusema ni matokeo ya "uongozi bora wa ccm" the same thing kwa meya wa kinondoni kuwa meya wa ccm na meya wa Kikwete at the same time - LOGIC 101
 
Richard alishinda big brother na ccm wakamuandalia maandamano na kusema ni matokeo ya "uongozi bora wa ccm" the same thing kwa meya wa kinondoni kuwa meya wa ccm na meya wa Kikwete at the same time - LOGIC 101

Aunt hivi watu huko nyumbani uwa wanakula kweli ukiwa umekasirika?
 
This is the power of ICT... kila aliyekula atajulikana tu... muda muafaka ukifika
 
Aunt hivi watu huko nyumbani uwa wanakula kweli ukiwa umekasirika?

Mmarekani mtarajiwa. Naombea hukumaanisha nilivyokuelewa. Kama ni hivyo kwa mwendo huu utaishia lupango huko unakoishi. Naomba naomba unifahamishe hasa ulikuwa na maana gani au umwombe msamaha huyu dada yetu. Kama ni mimi mwenye mawazo mabaya naomba unisamehe.
 
Jamani hapa ni watu wako kazini . Ia Londa ana historia kubwa ya ufisadi , udini na uchafu kibao. Londa nilimuona na wana CCM wenzake pale kwenye msiba wa Marehemu Chifupa huwezi kuamini . Nilishangaa msiba ulikiwa kama kampeni. Londa ni mchafu sana sana .Lakini nani wa kumweleza ? CCM ndiyo hivyo tulivyo .Kujuana na tunajuana bwana na kubebana .
 


Ina wenyewe hiyo......
 
Swala la Londa lina utata kiasi cha mwezi mmoja gazeti hili hili la Mtanzania liliandika habari mbaya ya Londa kuwa kawapa kiwanja Qiblatain.

wakati huo huo Londa ana kesi ya muda mrefu kashitakiwa na waislam kuwa kawadhulumu kiwanja, jengo na msikiti wa waislam na kukifanya kuwa soko na stendi ya bus.wasilam walikwenda hadi kwa Ritta Mlaki kupeleka kilio chao. vipi haya hayasemwi?

kiwanja hicho kiko TEGETA. kwa waislam wanamshutumu kwa kuwadhulumu mali zao na MTanzania linamshutumu kuwa mdini.hapa kuna vita ya kisiasa wilaya ya Kinondoni ambako kuna Mhaya anatumia mtandao wa Kihaya kumshambulia LONDA na gazeti la Mtanzania lina Ukagera.

cha ajabu makala zote amekuwa akiandikwa kama ALHAJI LONDA kwenye issue hizi mbili.
 


Mtalii:

Waislam na watanzania wengine mmeliwa. Na hayo mambo ya dini ni huku mitaani lakin mafisadi hawana dini na wanacheza show tu. Hii ni story:

Londa kachaguliwa diwani mpaka Meya na hakuwa na hakuwepo kwenye mzunguko wa mafisadi lakini na yeye akataka kunyonya. Kujitafutia ujiko, wanaCCM wakamwalika Ben Mkapa huko kwenye mkutano wa wanaCCM Kinondoni. Kwenye mkutano akamwambia rais na mwenyekiti wa CCM kuwa leo tunakuletea zawadi kutoka chama cha upinzani. Zawadi alikuwa Dr. Masumbuko Lamwai.

Mzee Mkapa akapata wazo zuri la kumtumia Mkereketwa Alhaji. Wakati wa uchaguzi Alhaji akapewa kazi na Ben. Kazi yenyewe ni lazima Mama Mlaki ashinde uchaguzi. Mama akashinda na chati ya Alhaji ikapanda na mirija ya kunyonya akapewa tena kutoka Ikulu.

Mnaolalamika na kwenda kumshitaki kwa mama Mlaki mnazunguka tu. Watu wale ni kundi moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…