Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 59
Naona gazeti la fisadi Rostam Azizi limeanza kuanika ufisadi wa mafisadi watoto. Ufisadi huanza kidogo kidogo na baadaye kufikia hatua ya kuiba mabilioni na kuanza kuua watu.
Masahihisho tu kwa nyie waandishi, hakuna kitu kinaitwa jiji la Florida hapa Marekani.
http://www.newhabari.com/mtanzania/habari.php?id=2238§ion=kitaifa
Masahihisho tu kwa nyie waandishi, hakuna kitu kinaitwa jiji la Florida hapa Marekani.
na masyaga matinyi
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Kinondoni Alhaji Salum Londa, anatuhumiwa kughushi nyaraka ili kumuwezesha binti yake kwenda Marekani, Julai mwaka jana.
Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA umebaini kuwa, Londa alitumia
vibaya madaraka yake kumjumuisha Amina Salehe Londa, katika orodha ya madiwani vijana, ili aweze kwenda Marekani.
Madiwani vijana kutoka Manispaa ya Kinondoni walikuwa wamealikwa nchini jijini Florida, Marekani, mwezi Julai mwaka jana na Taasisi ya Sister City International.
Lakini jitihada za Londa kumpeleka mtoto wake, ziligonga ukuta, baada ya Ubalozi wa Marekani kumnyima kibali cha kuingia nchini humo (VISA), tarehe 11 ya mwezi huo.
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa, kabla ya kufanyika kwa safari hiyo, mtoto huyo tayari alikuwa ameshalipwa fedha za safari kiasi cha Sh milioni 6, na manispaa hiyo.
Katika orodha ya madiwani vijana walioteuliwa kutoka kata 27 za Manispaa ya Kinondoni Julai 2005, ambapo kila kata ilitoa wawili, katika Kata ya Kawe ambayo Londa ni diwani wake, nafasi zote mbili zilichukuliwa na watoto wake.
Watoto hao ni Haji Londa, na Amina Salehe, ambaye katika orodha hiyo ameandikishwa kama Amina Abdallah. Majina ya Meya huyo ni Salum Saleh Londa.
Katika safari hiyo ambayo Alhaji Londa naye alikwenda Marekani, pia anatuhumiwa kurejea nchini na kompyuta ndongo (laptop) 20, na kuziuza kwa manispaa.
Mstahiki Meya huyo aliuza kompyuta hizo kwa Sh milioni 3 kila moja, bei ambayo inalalamikiwa kuwa ni kubwa, kulinganisha na bei ya soko.
Mwanzoni mwa wiki hii, madiwani katika manispaa hiyo walielezea kutokuwa na imani na kiongozi huyo kutokana na kutuhumiwa kwa vitendo mbali mbali vya ufisadi katika utekelezaji wa majukumu yake.
Walisema kuwa kuna mpasuko mkubwa miongoni mwao, kiasi cha kukwamisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Madiwani hao pia wanamtuhumu Londa kwa kujaribu kuupa sura ya udini mgogoro wa kiwanja namba 965, kilichopo Kata ya Kawe, katika manispaa hiyo.
Katika sakata hilo la kiwanja, Londa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kawe, anatuhumiwa kukiuka Sheria ya Ardhi Mijini ya mwaka 1999, kifungu namba 4.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, mwekezaji yeyote kabla ya kumilikishwa eneo, anapaswa kulipa fidia kwa mujibu wa bei ya soko kwa wakati husika.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika, kiwanja hicho chenye ukubwa wa mita za mraba 36,667, kilipaswa kulipiwa fedha zisizopungua Sh milioni 200, lakini malipo hayo hayajawahi kufanyika.
Kiwanja hicho kwa sasa kinamilikiwa na Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Masjid Qiblatain, na tayari kimezungushiwa ukuta, huku ujenzi wa msikiti, shule, na majengo mengine ukiendelea.
Kiwanja hicho kinapakana na kingine kilichouzwa na manispaa hiyo mwaka juzi, na kuzua tafrani kubwa kati ya wakazi wa eneo hilo, na mwekezaji aliyekusudia kujenga shule.
Katika sakata hilo la awali lililohusisha wakazi wa eneo hilo, ambapo walifikia hatua ya kuvunja ukuta uliokuwa ukijengwa na mwekezaji aliyeuziwa eneo, Meya Londa, alilaumiwa kuhusika na uuzwaji wa kiwanja hicho, ambacho ni mali ya manispaa.
Wakizungumza zaidi, wadiwani hao walisema imefikia hatua hata maamuzi yanayopitishwa na Baraza la Madiwani hayatekelezwi, yakiwamo malipo ya zabuni mbali mbali, ambayo yamekuwa yakizidishwa kwa malengo ya ubadhirifu wa fedha za walipa kodi.
Source Mtanzania;
http://www.newhabari.com/mtanzania/habari.php?id=2238§ion=kitaifa