Pwani: Madiwani Mkuranga Wapitisha Azimio La Kuomba Kupewa Hadhi ya Manispaa. Wadai Vigezo Vimetimia

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
47,911
55,817
Mkuranga: Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga wamepitisha Azimio la Kuomba Serikali kuipandisha hadhi Wilaya hiyo kuwa Manispaa Kwa kile walichodai kwamba Wilaya Yao imetimiza vigezo.

Baadhi ya vigezo wanavyojinasibu kwao ni idadi ya watu na ukusanyaji Mapato.

My Take
Serikali ipitie Upya vigezo vya Miji.kupata hadhi ya Manispaa Kwa kuhakikisha wawe na uwezo wa kujitegemea kibajeti Kwa walau 60% na idadi ya watu zaidi ya 350,000 Kwa pamoja na sio kama ilivyo Sasa ambapo vigezo ni loose.

Matokeo ya sensa 20222
Screenshot_20240218-091552.jpg
Screenshot_20240218-091724.jpg


====


(𝐈𝐦𝐞𝐚𝐧𝐝𝐢𝐤𝐰𝐚 𝐍𝐚 𝐉𝐮𝐥𝐢𝐞𝐭𝐡 𝐌𝐤𝐢𝐫𝐞𝐫𝐢, 𝐌𝐊𝐔𝐑𝐀𝐍𝐆𝐀)
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani wamepitisha ombi la Halmashauri hiyo kupandishwa hadhi kuwa Manispaa.

Wamepitisha ombi hilo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Februari 14 ambapo wamwsema wamejipima vigezo vinavyostahili kupandishwa hadhi kuwa Manispaa na kubaini kuwa wanakidhi ikiwemo idadi ya wananchi ambao kwa sasa wako zaidi ya laki tano.

Wamesema Halmashauri hiyo Ina vigezo vya kuwa Manispaa, ikiwemo idadi ya watu huku wakielwza kwamba wakati Halmashauri hiyo inaanzishwa mwaka 2000 kulikuwa na Kata 15 na sasa tuna Kata 25.

Ametaja faida watakazonufaika nazo iwapo ombi hilo litapitushwa na TAMISEMI kuwa ni pamoja na kutengewa bajeti kubwa kutoka Serikalini ambayo itakuwa inawesesha kutekelezà miradi mikubwa itakayotatua vikwazo kwa wananchi

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Waziri Kombo amesema kuwa moja ya vigezo vinavyoweza kuwapa uwezekano wa kupata manispaa ni makusanyo ya mapato ambapo katika robo ya pili ya mwaka 2023/2024 wamekusanya sh.6.5 bilioni kati ya bajeti ya sh 13 bilioni

Kombo ametaja vigezo vingine kuwa ni uwepo wa huduma za kijamii Taasisi zinazotoa huduma za pesa uwepo wa viwanda viwanda na uwezo wa Halmashauri kujitegemea kwa asilimia 25 kwa bajeti.

#NipasheMwangaWaJamii #NipasheHabari
 
Panaitwa Mkuranga hivyo hivyo! Zaidi ya wapaa vijisamaki; wauza madafu; chapati na mihogo ya kukaanga hamna lingine la maana kiuchumi pale.
Basi vigezo vya idadi ya watu vimefikia maana mjini kutakuwa na watu wengi.

Wakifanya hivyo maeneo ya Vijijini yanayozungumka Mji ndio inakuwa Mkuranga DC na wao wanaitwa Mkuranga MC
 
Ametaja faida watakazonufaika nazo iwapo ombi hilo litapitushwa na TAMISEMI kuwa ni pamoja na kutengewa bajeti kubwa kutoka Serikalini ambayo itakuwa inawesesha kutekelezà miradi mikubwa itakayotatua vikwazo kwa wananchi.
.........Maokoto kutoka serikali kuu ndio lengo
 
Ametaja faida watakazonufaika nazo iwapo ombi hilo litapitushwa na TAMISEMI kuwa ni pamoja na kutengewa bajeti kubwa kutoka Serikalini ambayo itakuwa inawesesha kutekelezà miradi mikubwa itakayotatua vikwazo kwa wananchi.
.........Maokoto kutoka serikali kuu ndio lengo
Hii sababu ni mojawapo ya ujinga unatakiwa kufutwa.Manispaa zinatakiwa kujitegemea sio kudowea pesa za Serikali kuu
 
Nyie watu mnaijua mkuranga vizuri ama mnaropoka tu? Kuanzia mpakani kongowe, mwandege, vikindu, mwanambaya, kisemvule, mkuranga yenyewe na sasa kijiji cha mkiu ni viwanda vitupu. Hayo maokoto yanayotokana shughuli viwanda mmejifanya hamjui? Na kwa taarifa yenu shughuli za kiuchumi zinashika kasi sana hasa uwekezaji katika kilimo na ufugaji kwahiyo acheni roho mbaya paka nyie.
 
Azam amewekeza sana,ni sawa na leo Bagamoyo iliyokaribu na Dar pakiwekezwa,watu watakimbilia tu.mnaokataa mna hoja gani kama vigezo vya nchi vinavyotumia vimetimia?
 
Mazingira mazuri lkn mzunguko wa uchumi bado mdogo
Waongeze juhudi
Acha kukurupuka Mzee.

-Mkuranga ndio Wilaya inaongoza Kwa viwanda Pwani next Chalinze

-Mkuranga ndio Wilaya namba 2 Kwa Mapato Mkoa wa Pwani,nyuma ya Chalinze

-Mkuranga Iko mpakani na Dar na ndio Wilaya yenye watu wengi kushinda zote Mkoa wa Pwani na in fact Watu wanahamia Mkuranga.

With all hayo unasema hakuna mzunguko wakati ni Kati ya Wilaya 15 Tanzania Zenye makusanyo makubwa? Unaijua Bilioni 10 wewe?
 
Back
Top Bottom