Meseji niliyoikuta kwenye simu ya mke wangu

Meseji niliyoikuta kwenye simu ya mke wangu

Kama hutaki msaada wa mawazo basi tayari umeshapitisha hukumu. Basi tupe hints kuhusu hiyo hukumu. Vinginevyo kutua yaliyo moyoni ni pamoja na kutafuta ushauri + sympathy.

Binafasi nimeguswa sana na pole kwa yaliyo kukuta. Ukiweza kulimaliza hili basi huenda hutakuwa na mtihani mwingine mkubwa maishani. Time and locations are key to healing. Jipe muda na ikiwezekana chukua likizo ukae mahali tofauti ili uweze kulitafakari hili jambo!
Ingekuwa Mimi ndoa ingevunjikia happy hapo mgahawani
 
pole sana,
Huhitaji ushauri lakini fikiria kuwa kama na wewe unacheat YEYE NI MWANADAMU PIA .pole sana inauma.
Wewe rekebisha kauli hapo...mwanaume kucheat ni kutimiza wajibu wa kikatiba kijinsia....mwanamke ni kosa la jinai kufanya hvyo.....usirudie tena kusema hiyo kauli unaniudh.
 
Yawezekana kabisa kuwa Coleman ni mtu ambaye yupo kwenye PB ya mkeo, ila chunguza pengine na yeye (Coleman) alikuwa akituma kwa mtu wake ila bahti mbaya ikatelezea kwa mkeo.
Je hiyo sms ndio ilikuwa imeingia au ilikuwa ni ya kitambo?
Kama ni ya muda mrefu ni ya lini haswa?
Ulichotakiwa kufanya ni kutafuta kwe Outbox mkeo alimjibu nini ili upate pahali pa kuanzia.
yes....angepata kujua mkewe alijib nn....angepata pa kuanzia
 
hakika hii ishu imenitokea mimi binafsi na si mtu mwingine mchana huu wa leo
Huyo jamaa anakufaa sana, anamfanya mkeo awe na furaha ndio maana urudipo kazi mkeo hukupokea kwa fura coz keshapewa kimoja, mtafute umpongeze tu
 
Sikupi pole Mzee kwasababu inawezekana hiyo msg iliingia kwa makosa haikuwa kwa ajili ya Mkeo. Binafsi nilishawahi kutumiwa msg na msichana kwenye simu yangu kwa makosa na ilikuwa ina ujumbe mzito sana kama ingetokea Mke wangu kuiona ingekuwa balaa kenye ndoa yangu mpaka ukoo mzima wangeipata. MSG ilikuwa inasema "JANA UMENIFANYA KOTE HALAFU HELA YENYEWE KUMBE HUNA, USIPONIPA HELA YANGU LEO NAKUJA DAI MBELE YA MKEO".
soma msg vzr uelewe ni coleman ndo katuma..
 
Duh haya ndio maisha kaka.....sio kula peremende tu bali na machungu pia. Kuna mambo mengi binafsi naweza kushauri.

Mtazamo wa suala lenyewe

1. Ni vizuri ukatumia muda na busara zako kujiridhisha juu ya uhalisia wa hiyo message i.e. je imekosewa mlengwa au ilikuwa intended kwa mkeo. Kama ni suala la kukosea namba hicho ni kitu cha kawaida.....mengi yametokea mfano kutuma muda wa maongezi kusikohusika n.k.

2. Kama ilikuwa intended kwa mkeo, ni vizuri kujiridhisha kuwa ilitumwa kwa makusudi ya kukugonganisha au ni mawasiliano ya kawaida baina ya wapenzi. Kupata namba ya mtu sio kitu kigumu sana, watu wengi wametumia fursa hiyo kutuma ma-ujumbe ya ajabu-ajabu ili kuleta mtafaruku kwenye nyumba za watu (usisahau mkuu ndio maana pamoja na mambo mengine hawa jamaa wanataka kusajili namba za simu zetu kutokana na kero kama hizo).

3. Kama ilitumwa kwa minajili ya kubadilishana salamu za kimapenzi baina ya wapenzi, hapo ndipo kwenye tatizo na fursa. Tatizo ni kuwa mkeo ameteleza...na fursa ni kuwa umefahamu hilo na uko katika nafasi ya kulirekebisha. Ni mapenzi ya Mungu umejua hilo sasa na ni wajibu wako kurekebisha kasoro hiyo.

Ushauri wangu

1. Ikiwa na kukosewa namba au sms ya kukugombanisha....just ignore it! Binafsi nikupe kisa live. Siku tulikesha kikazi somewhere...ilipotimu saa tisa alfajiri mfanyakazi mwenzetu mmoja akapokea forwarded sms toka kwa mkewe ikielezea kuwa jamaa amelala kwenye nyumba ndogo. Alichokifanya yule bwana ni kumpigia mkewe simu instantly na kutupatia tuongee nae, shemeji yetu aliridhika na alituomba radhi kwa kutokuwa mstahimilivu

2. Ikiwa mkeo ameteleza....ni vizuri ukae nae chini umtake ajirekebishe. Hataweza kukubali kuwa anafanya mchezo huo....lakini muombe atunze heshima yako na umwambie mjitahidi kurekebisha tatizo hilo mapema. Usiwe na maswali ya kipolisi, ujikakamue uweke msimamo wako imara. Kuoa au kuolewa sio mwisho wa kupenda....hivyo huwezi kuzuia kupenda kwa mabavu bali kwa hekima na werevu. Inauma sana lakini ndio maisha....sisi sote binadamu tuna udhaifu na mapungufu....ni budi kutumia busara zetu kurekebisha mapungufu pale yanapotokea. Endelea kumpenda mkeo kwa heshima kubwa uliyonayo kwa watoto wako
mpuuzi wewe si ajabu ht demu huna huwezi jua uchungu wa mke
 
Back
Top Bottom