Merry Patrick Daniel afariki Dar es Salaam, Ndugu zake wanatafutwa

Merry Patrick Daniel afariki Dar es Salaam, Ndugu zake wanatafutwa

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
61,918
Reaction score
38,244
Merry Patrick Daniel, ambaye kwa mujibu wa taarifa zilizopo amefariki dunia na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Dar es Salaam, aliwahi kusema akiwa hai kwamba yeye ni mwenyeji wa Arusha. Hata hivyo, bado haijafahamika alikuwa akishi au anatokea eneo gani ndani ya Arusha.

Kwa mtu yeyote anayemfahamu Merry Patrick Daniel, hasa ndugu, jamaa au marafiki zake wa Arusha, anaombwa kutoa taarifa ili ndugu zake waweze kupatikana.

Kwa taarifa zaidi: +255 689 848090 Tafadhali sambaza taarifa hii ili kuwasaidia ndugu zake kupatikana.

1791354905949.jpg
 
Dada pichani kwa jina Merry Patrick Daniel, mkaazi wa mtaa kingugi amefariki kwa maradhi na mwili wake umehifadhiwa hospitali ya Temeke

Hajulikani ndugu yake yeyote wakati wa uhai wake marehemu alidai ametokea mkoa wa Arusha na hana ndugu hapa mjini

Tunaomba tusambaze taarifa hii ktk ma group mbali mbali na media mbali mbali,wapatikane ndugu zake popote walipo

Mawasiliano 0713267121/0789267121
M/kiti wa serikali ya mtaa wa Kingugi.

Au toa taarifa kituo chochote cha polisi.

Taratibu za mazishi zinaendelea kwa kibali cha jeshi la polisi kituo cha kizuiani (Maturubai)

Asante 🙏
 
rip
Merry
D
 

Attachments

  • 1791355187786.jpg
    1791355187786.jpg
    152 KB · Views: 7
Alifikaje,Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, akalazwa,akatibiwa, na walio mpokea hawajui chochote kuhusu marehemu?

Mjini DSM.
wako wanawake na wanaume wengi wanaofanana na Marry.
Tofauti ni kuwa wao hawajafa ila Marry amefariki (RIP).

Mtu amekuja mjini kutafuta maisha.
Labda kaz za ndan au muhudumu wa bar nk.
Kajibana akaweza kupanga , ana marafiki na majiran (ambao ndio walikuwa wanamtibia na kumpeleka hosp) . Ila sio ndugu.
Unafikiri mtu wa namna hii akifariki atazikwa na majiran au marafiki?.

Hapana. Ni lazima ndugu zake watafutwe.

Kwahiyo ishu sio nan kampeleka hosp. Ishu ni ndugu wajitokeze wakamzike ndugu yao kama inavyostahili.
 
Kuna wale watu utawasikia wakisema SITAKI MAWASILIANO YOYOTE NA NDUGU NIMEWAKATIA LINE. haya ndio yanaweza kuwa matokeo yake.
 
Back
Top Bottom