Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
1.
FMES mkuu, heshima mbele, naomba nikusahihishe kidogo Mengi na Mkapa ni paka na panya.

- Hiii ni sasa baada ya Mengi kuanza kufichua uchafu wa Mkapa akiwa rais, swali la Mkapa in private ni kwamba Mengi amem-betray, unafikiri inaweza kua ni nini hasa?

- Na besides, kwa maoni yako wewe unafikiri Mengi anatoa wapi nyeti za biashara za Mkapa akiwa Ikulu, maana kumbuka kua ni magazeti yake Mengi ndio yamekuwa ya kwanza alyways, kutoa hizo habari?


2.
Mengi hafanyi siri ya kuwa Mkapa alimwekea vikwazo katika mipango yake mingi sana ya biashara lakini kilichobaki kama doa na kufanya Mengi aweke kinyongo kwa Mkapa ni Kilimanjaro hotel alafu Kiwira. Nadhani wewe mkuu unaweza kupata taarifa zote kuhusu ishu hii bila mimi kuweka zaidi hapa. Asante

- Ni kweli kabisa maneno yako, my point ni kwamba ninajua for a fact kwamba huko nyuma walikuwa marafiki, nimewaona mara nyingi sana wakiwa pamoja huko majuu, inawezekana kuwa walikosana somewhere, lakini haibadili ukweli kuwa wamewahi kuwa close friends, ikiwa ni pamoja na kusaifir pamoja kwenye ndege ya rais au?

Otherwise sina tatizo kukubali hoja yako ya msingi kuwa sasa hawaelewani, au?
 
Date::12/6/2008
Waziri Masha asema hataki malumbano na Mengi
Na Leon Bahati

MVUTANO wa Mambo ya Ndani Lawrence Masha na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi , sasa umechukua sura mpya baada ya Waziri Masha kukataa kujiuzulu na kusisitiza kuwa Mengi asipowasilisha utetezi atakiona cha moto.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Masha alisema kuwa hataki kuingia katika malumbano na Mengi hivyo kama hataki kupeleka uthibitisho huo, asubiri atakiona cha mtemakuni.

“Mimi nasema, sitaki kujiingiza kwenye malumbano na Mengi. Kama yeye hataki, aache, aone kitakachofuatia,” alisema Masha.


Mengi alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akizungumza kupinga notisi ya siku saba aliyopewa na Masha kuthibitisha madai yake na kaeleza kwamba yupo tayari kutoa ushahidi wa kutishiwa kuuawa kwamba endapo atautoa basi Masha ajiuzulu .

Alifafanua kuwa yeye kama mwenye dhamana ya kulinda maisha ya raia wote, ana jukumu la kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata haki bila kuonewa.

Kwa sababu hiyo, asingependelea kuona kuna mtu anaonewa kulingana na maelezo aliyotoa Mengi.

Mengi juzi alimtaka Masha kuweka wazi endapo yuko tayari kujiuzulu wadhifa wake iwapo atathibitisha maelezo yake.

Juzi Masha alisema maelezo ya Mengi kuwa waziri kijana alitoa ushauri kwenye kikao nyeti akiitaka serikali immalize kibiashara yanajenga hisia kwa wananchi kuwa serikali inaweza kupanga mkakati wa kumuonea mtu.

“Hizi ni tuhuma kali… Unapoituhumu serikali na unapomtuhumu waziri, ni lazima uwe na uthibitisho,” alisema Masha akifafanua:

“Siyo tu aendelee kueleza hivi hivi tu, aje na amtaje waziri huyo ni nani, na aje na ushahidi. Asipothibitisha, tutamchukulia hatua.”


Waziri Masha, ambaye wizara yake inahusika moja kwa moja na kazi kuu ya serikali ya kusimamia usalama wa watu na mali zao, alimtaka Mengi kuwasilisha ushahidi huo moja kwa moja kwake ama kulipelekea Jeshi la Polisi ili lichunguze na kuchukua hatua zinazotakiwa.

Masha alisema kuwa kama atabainika kweli kuna waziri mwenye mpango huo, atachukuliwa hatua ili kudhihirisha kuwa nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria.

Juzi Masha alimuandikia Mengi notisi ya siku saba akimtaka athibitishe maelezo yake aliyoyatoa Jumatano iliyopita kwa vyombo vya habari kuwa kuna waziri kijana aliyeshawishi serikali imbambikize deni kubwa la kodi ili akishindwa kulilipa afilisiwe.

Bila ya kutaja jina, Mengi alieleza kuwa waziri anayefanya njama hizo ni kijana, lakini serikali imehamaki haraka baada ya mmoja wa wajumbe wa Baraza la Mawaziri kushushiwa tuhuma hizo nzito, ambazo kama zikithibitishwa itakuwa ni kashfa kubwa dhidi ya serikali ya awamu ya nne.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, mmoja wa mawaziri vijana katika baraza la mawaziri wa serikali ya awamu ya nne, alisema kama Mengi atashindwa kuthibitisha hilo, serikali itachukuliwa hatua, zikiwepo za kutaka kusababisha uvunjifu wa amani nchini.

Mengi pia aliwaambia waandishi kuwa kuna watu wasiojulikana ambao walimtumia ujumbe mfupi wa maneno wenye maelezo ya kumtishia maisha, na Masha alisema tayari tukio hilo limeripotiwa polisi, ambao wanalishughulikia kikamilifu na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua.

Mengi hakupatikana jana kuzungumzia agizo hilo na ilidaiwa kuwa alikuwa akihudhuria mkutano.

Hii si mara ya kwanza kwa Mengi kuingia kwenye mzozo na wanasiasa katika serikali za awamu ya tatu na ya nne. Hivi karibuni, Mengi pia aliwahi kueleza kuwa alitishia maisha na hivyo kupewa ulinzi mkali.


Wow! huyu kijana sasa ameamua - lakini maji kama atakuwa ameyavulia nguo, sharti ayakoge. Pole sana kama yatakuwa ya moto yakamnyofoa ngozi.
 
1.

- Ahsante mkuu na heshima ikurudie pia, ingawa nilishamua kutoka hii mada lakini sina taizo kukujibu kwa kadri ya uwezo wangu wa kuelewa.

2.

- Ina maana msimamo wako huu ni kwa sababu una mgongano wa kimasilahi na waziri wa ndani, au?

3.

- Kutofautiana kwetu mawazo haina maana ya ushabiki wa anything, ila ni ku-practice demokrasia to the fullest, mtizamo wako ni kwamba hapa kuna kushabikia mtu, mtizamo wangu ni kwamba hapa kuna utata wa kisheria unahitaji kutatuliwa na pande zote mbili zipewe haki kisheria na ni lazima hii ishu iende kwenye sheria, kusiwe na anything less ili kupata ukweli wa kina na kwa faida ya wananchi in the future.

- Eti waziri wa jamhuri anachemka kwa kusimamia sheria za jamhuri ya kuwalinda wananchi wake ndani ya taifa?


4.

- Mkuu taifa limedumaa kwa sababu ya kutotii sheria, hakuna anayemkatalia Mengi kuwa ana uhakika na anachokisema, lakini ninasema hivi lazima kuwa na utaratibu kisheria, Mengi ana uhakika basi aupeleke kwenye sheria ili kama ni waziri mwenye makosa aabike not only kisheria bali hapa sasa hoja ya kumtaka ajiuzulu inakua na nguvu akifikia mahali akiabika kisheria,

- Sina tatizo na Mengi as individual anajua hilo, lakini nina tatizo kubwa na the way alivyoi-handle hii ishu, in fact toka ile ishu ya mashehe nilishaanza kua na wasi wasi naye na agenda zake, mkuu hili litakua ni taifa la namna gani ambalo wananchi watakurupuka tu na kuwarekodi wengine kwenye video na tapes, halafu kwenda kwenye media na kuwatishia nazo, wewe huoni kuwa huo ni u-Banana Republic? Sheria iko wapi?

- Sasa mwananchi anadai kuna waziri anamhujumu, kudai wkangu sheria itumike kuamua ukweli wa hii tuhuma kunanifanya niwe na beef na kampuni za Mengi? Hujanitendea haki hapo mkuu!

Mkuu FMS
Niliposisitiza kwa wino mweusi,mimi nilianza kupata wasiwasi tangu ITV ilipofoji SAHIHI ya Mtikila.
 
Ushauri wa Bure kwa Mz Mengi!!!!

Acha kuwa chaudeko!!!!!!


Kama una malalamiko ya msingi, peleka mbele ya vyombo vya usalama/sheria. Pia kuwa wazi, kama umeweza kutaja kuwa waziri kahusika, washindwa nini kumtaja jina???? Hata kama sheria haitakutendea haki, basi wana-inji tutajua haki iko wapi.

Kwa sasa tafsiri nyingi zaweza kuwa sahihi!!!! Mojawapo ni kuwa Unajihami kutokana na malimbikizo na ukwepaji kodi!!!
 
All shenanigans aside, it pains me to see us getting back into the unconstitutional commands of Mremaism, from a leaned brother no less.

Granted, Mengi is an obfuscating IPP ombudsman, but what will Masha do if Mengi is not able to clarify in seven days?

Pundit i like your comments sometimes but i'm worried if often communicate - plz just learn to use alittle more simple english!
Mawazo yangu tu lakini mkuu, heshima yako!
 
Ni vizuri kuwa hapa kuna uhuru wa kufikiri na kutoa maoni. Mh Masha anajiaibisha na kuabisha vijana. Yeye alitakiwa kuwa mmoja kati ya viongozi damu mpya ambao wataacha politics za magazetini, au politics za mipasho kama wanavyoita wengine, angaechapa kazi kwenye wizara yake kupambana na uhalifu mwingi uliopo tanzania, maslahi duni ya askari polisi, wauaji wa albino nk. sasa mheshimiwa anaanza kupambana na Mengi sijui lengo lake ni nini, inaonekana naye ameengia kwenye mtego wa siasa tunazokataa na zilizodumaza Tanzania. Suppose kama huyu jamaa angekuwa PM sijui ingekuwaje? Nadhani kuna mmnaomjua sana huyu mheshimiwa lakini kwa watu tusiomjua nadhani tunaona kuwa anajidhalilisha na kujiaibisha.
 
Pundit i like your comments sometimes but i'm worried if often communicate - plz just learn to use alittle more simple english!Mawazo yangu tu lakini mkuu, heshima yako!

Teh...teh...duhh!...yaani Bw.njoomloli umenichekesha sana! i suppose on that note you have spoken for many....Mie nilishaamua kujichukulia the 'Oxford Dictionary'. kaazi kweliX2!.
 
I'm not a lawyer but here is my 2 cents:::

1.Mengi made allegations against people who he did not name as a citizen.
2. Mengi said he has forgiven those people.
3. Let for the sake of discussion say Mengi had no point whatsover, what is he liable for???? As a citizen let us say he had no basis for what he said but rather he is just paranoid, is that illegal???

Masha as a minister has given Mengi 7 days, what if Mengi does nothing within those 7 days?? what will Masha do??? Has it become a crime for citizens to make allegations nowadays?? If the allegations are false, si we just ignore au??????

Masha U are doing things personally while using Govt weight which is a disaster waiting to happen. We know why U are mad son, but U have lost this battle because U are fighting the battle against a citizen who can not lose by merely making allegations no matter how far fetched the allegations are.


Well said Moelex23

Mkuu FMES


Raia akitoa tukuhuma; anayetakiwa kufanya uchunguzi wa kuthibitisha hizo tuhuma kama ni za kweli na iwapo sheria ya nchi imevunjwa ni huyo Raia (katika hili Mengi), Polisi au Waziri wa Mambo ya Ndani?
 
Mkuu FMES

Raia akitoa tukuhuma; anayetakiwa kufanya uchunguzi wa kuthibitisha hizo tuhuma kama ni za kweli na iwapo sheria ya nchi imevunjwa ni huyo Raia (katika hili Mengi), Polisi au Waziri wa Mambo ya Ndani?

Date::12/6/2008
Waziri Masha asema hataki malumbano na Mengi
Na Leon Bahati

1. MVUTANO wa Mambo ya Ndani Lawrence Masha na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi , sasa umechukua sura mpya baada ya Waziri Masha kukataa kujiuzulu na kusisitiza kuwa Mengi asipowasilisha utetezi atakiona cha moto.

2. Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Masha alisema kuwa hataki kuingia katika malumbano na Mengi hivyo kama hataki kupeleka uthibitisho huo, asubiri atakiona cha mtemakuni.

3. "Mimi nasema, sitaki kujiingiza kwenye malumbano na Mengi. Kama yeye hataki, aache, aone kitakachofuatia," alisema Masha.

4. Mengi alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akizungumza kupinga notisi ya siku saba aliyopewa na Masha kuthibitisha madai yake na kaeleza kwamba yupo tayari kutoa ushahidi wa kutishiwa kuuawa kwamba endapo atautoa basi Masha ajiuzulu .

5. Alifafanua kuwa yeye kama mwenye dhamana ya kulinda maisha ya raia wote, ana jukumu la kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata haki bila kuonewa.

6. Kwa sababu hiyo, asingependelea kuona kuna mtu anaonewa kulingana na maelezo aliyotoa Mengi.

7. Juzi Masha alisema maelezo ya Mengi kuwa waziri kijana alitoa ushauri kwenye kikao nyeti akiitaka serikali immalize kibiashara yanajenga hisia kwa wananchi kuwa serikali inaweza kupanga mkakati wa kumuonea mtu.

8. "Hizi ni tuhuma kali… Unapoituhumu serikali na unapomtuhumu waziri, ni lazima uwe na uthibitisho," alisema Masha akifafanua:

10. "Siyo tu aendelee kueleza hivi hivi tu, aje na amtaje waziri huyo ni nani, na aje na ushahidi. Asipothibitisha, tutamchukulia hatua."

11. Waziri Masha, ambaye wizara yake inahusika moja kwa moja na kazi kuu ya serikali ya kusimamia usalama wa watu na mali zao, alimtaka Mengi kuwasilisha ushahidi huo moja kwa moja kwake ama kulipelekea Jeshi la Polisi ili lichunguze na kuchukua hatua zinazotakiwa.

Masha alisema kuwa kama atabainika kweli kuna waziri mwenye mpango huo, atachukuliwa hatua ili kudhihirisha kuwa nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria.

12. Juzi Masha alimuandikia Mengi notisi ya siku saba akimtaka athibitishe maelezo yake aliyoyatoa Jumatano iliyopita kwa vyombo vya habari kuwa kuna waziri kijana aliyeshawishi serikali imbambikize deni kubwa la kodi ili akishindwa kulilipa afilisiwe.


13. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, mmoja wa mawaziri vijana katika baraza la mawaziri wa serikali ya awamu ya nne, alisema kama Mengi atashindwa kuthibitisha hilo, serikali itachukuliwa hatua, zikiwepo za kutaka kusababisha uvunjifu wa amani nchini.

14. Mengi pia aliwaambia waandishi kuwa kuna watu wasiojulikana ambao walimtumia ujumbe mfupi wa maneno wenye maelezo ya kumtishia maisha, na Masha alisema tayari tukio hilo limeripotiwa polisi, ambao wanalishughulikia kikamilifu na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua.

15. Hii si mara ya kwanza kwa Mengi kuingia kwenye mzozo na wanasiasa katika serikali za awamu ya tatu na ya nne. Hivi karibuni, Mengi pia aliwahi kueleza kuwa alitishia maisha na hivyo kupewa ulinzi mkali
 
hivi kuna sheria inayompa madaraka mtu binafsi au kiongozi wa serikali kumlazimisha mtu mwengine kumtaja mtu aliyemtuhumu?
mimi nilidhani nguvu za kisheria za kufanya hivyo zipo mahakamani (hakimu au/na jaji).

sidhani lugha kama "atakiona cha moto" au "atakiona cha mtema kuni" zinasaidia sana katika hili zaidi zaidi tu itaonekana ni vitisho vya serikali. napenda kuamini haya maneno ni tafsiri ya waandishiwa habari tu.

kama hayo ya kutishia ni maneno yake mheshimiwa waziri je yanaweza kutumiwa mahakamani kama ushahidi wa vitisho vya serikali naamini wanasheria wanaweza fafanua.

naona sakata hili tutajifunza mengi tu kuhusu haki za raia na majukumu ya serikali.
 
Teh...teh...duhh!...yaani Bw.njoomloli umenichekesha sana! i suppose on that note you have spoken for many....Mie nilishaamua kujichukulia the 'Oxford Dictionary'. kaazi kweliX2!.


Tunaita communication break down.Kwenye communication skills walitufundisha jinsi ya kuongea kulinga na watu unaoongea nao.
Kwa wale wanao ishi kwenye nchi ambazo english ni lugha ya kwanza (kama USA,UK ..) utaona jinsi ilivyo simple .Sio kama hizi jargon tunazokutana nazo toka kwa bongo wenzetu (mnojawapo Pundit)tehe tehe tehe!

Ukitumia technical term muda mwingine unaambiwa "speak english" hata kwenye interview wanashauriwa kujua unayezunguza naye kuwa ni mtu wa field yako or just a HR staff ili usije kumuacha kwa technical terms zako mwishowe asikuelewi na usifikie lengo la kutuma ujumbe wako,pia ukaonekana com skill yako poor.Sasa hapa tunapata zaidi ya technical terms ni full of vocabulary.Hta kiswahili tulichozaliwa kina misamiati ambayo bado ni kiswahili ila mtu akiwa anatumia nusu ya maneno misamiati basi anavunja mawasiliano.

Ila wengine humu wanatumia english ya kawaida inayotumia day to day wanatusaidia kukuza english zetu kwa sisi tunaojifunya bado.
 
Date::12/6/2008
Waziri Masha asema hataki malumbano na Mengi
Na Leon Bahati


Masha alisema kuwa kama atabainika kweli kuna waziri mwenye mpango huo, atachukuliwa hatua ili kudhihirisha kuwa nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria.



Mkuu FMES

Angalia hiyo para; Je Masha ana mamlaka ya kumchukulia hatua Waziri?
 
JokaKuu,

Hapo juu hauko sahihi. Fuatilia data za watu ambao walikuwa wanajisomesha au wanasomeshwa na mashirika yasiyo ya kiserikali, nao ilikuwa lazima waonyeshe vyeti vya JKT.

Kuna watu walisoma international schools toka utoto wao na bado walienda JKT.

Ni kwa wale tu ambao hawakuwa raia au walikuwa na sababu zingine, hiyo requirement haikuwa muhimu. Kwa Mtanzania hiyo ilikuwa ni lazima bila kujali unataka udhamini wa serikali au la.

Kuna kitu Masha anaficha ndio maana ni muhimu kwa waandishi wa habari kuhakikisha wanapata majibu sahihi.

Nacho ni "Masha ana uraia wa marekani" japo alizaliwa Tanzania
 
- Serikali haina haraka, waziri ndio kwanza amerudi jana usiku kutoka South Africa, kwenye ziara ya kikazi kwa hiyo hili la barua kupelekwa sio tatizo,

tatizo ni kuna tunaotaka kuona haki inatendeka kisheria kwa pande zote mbili, yaani serikali na Mengi, kwa faida ya wananchi at large in the future!

Isingekuwa na haraka isingetoa siku saba
 
Kila wakati Masha akiongea ndio kwanza anazidi kujifunga kamba za miguu... bora akae kimya tu, itamsaidia...
 
Masha ana hasira sana and he is not diplomatic. Mzee FM umemtetea sana hadi nikakaribia kujiridhisha na utetezi wako, lakini baada ya hii habari ...mmmhhh. Msaidie huyu bwana mdogo please. Mwanzoni mtu angeniuliza baada ya Kikwete who is our potential president ningemtaja Masha bila hata kusita. Lakini sasa nabaki kujiuliza angekuwa yeye ndio Rais sasa hivi Mengi sidhani kama angepewa hata masaa 7 ya kujieleza wacha hizi siku 7 za sasa.

Hivi Masha ni nani wa kutoa vitisho magazetini katika karne hii ya demokrasia ya uhuru wa kujieleza na kutoa duku duku? Eti Mengi atakiona cha mtema kuni? Ina maana Masha sasa kadhihirisha kumbe yeye ndio mtoa vitisho? Sasa hapa jamani Mzee Mengi anahitaji kupeleka ushahidi gani tena polisi? Ushahidi si ndio huo tayari Masha kautoa mwenyewe? Tayari huu kwa Mengi ni ushaidi tosha ya kwamba ametishiwa na Waziri Kijana kwamba "atakiona cha moto" "Atakiona cha mtema kuni".

Msaidieni huyu bwana mdogo. Anakaribia ukingoni.
 
Masha hasifikiri tuko Misungwi hapa. Kama nchi hii inaongozwa kwa utawala wa sheria kwa nini alikubali cheo cha uwaziri huku akijua upupu aliofanya yeye (Deep Green na IMMA). Kwa nini hasijiuzuru kwa kuhusishwa na tuhuma chafu. Kwa nini asiachie ngazi kupisha uchunguzi dhidi yake na Deep Green.
Hakuna utawala wa sheria Tanzania. Kila mtu anajifanyia mambo yake. Nchi inaongozwa na MANYANG'AU. Ndiyo nimesema Manyang'au. Nchi inaongozwa kwa share, FISADI like RA ana uwezo hata wa kumtikisha Prezidaa. Kwa hiyo tusidanganyane hapa. MASHA WAJIBIKA.
 
Ikibainika kama Masha ndiye aliyetoa hivyo vitisho atajishughulikia mwenyewe?? Very interesting.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom