Vitisho vya Godbless Lema kwa wafanyabiashara ni aibu tupu

Irene Darton

Member
Feb 25, 2024
18
21
Na Joseph Maziku, Arusha

Mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na mbunge wa zamani wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema ameingia katika rekodi nyingine ya kushangaza kutokana na utaratibu anaoutumia kuomba michango ya fedha kutoka kwa wafanyabiashara Jijini Arusha kwa madai ya bajeti ya maandamano.

Wafanyabiashara wanao uhuru wa kuwa na vyama vya siasa lakini utaratibu wa kuwatishia ili waweze kutoa fedha na kwamba asiyetoa fedha atatajwa katika mkutano wa hadhara ili kumchonganisha na serikali ni Utaratibu usiokubalika unaopaswa kukemewa na watu wote. Majina ya wafanyabiashara 45 waliochangishwa fedha kwa kutishwa yatatolewa kwa vyombo vya habari.

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA wa kanda ya Kaskazini wamehoji namna inayotumika kukusanya fedha hizo na mtu binafsi bila kuhusisha viongozi wengine. Mpaka kufikia siku ya leo jioni ya tarehe 24 Februari 2024 tayari kiasi cha takribani Milioni 135 kiko mfukoni kwa Ndugu Godbless Lema kana kwamba anayo mamlaka yote juu ya fedha hizo za michango.

Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kanda ya Kaskazini wamehoji sababu ya Godbless Lema kujiamini kupitiliza na kukumbushia kitendo cha dharau alichoonyesha katika kikao kilichohudhuriwa na N/Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, baada ya mvutano juu ya uamuzi wa Chadema makao makuu kutotoa fedha za bajeti ya maandamano.

Habari za ndani zinaeleza kuwa Ndugu Godbless Lema ameweka wazi kuwa hata weka fedha zinazokusanywa mezani kwaajili ya bajeti na badala yake atatoa fedha yeye mwenyewe kila inapohitajika na kwamba watu wa makao makuu wanahujumu kazi zake na hivyo hataruhusu waguse kitu chochote katika mipango na utekelezaji wa bajeti ya maandalizi ya maandamano.
 
Back
Top Bottom