Kwa mtu anayemfahamu Mengi na biashara zake ukweli uko wazi kwamba kwa kipindi cha 1995 mpaka 2005 amekuwa kinyume kabisa na upinzani nchini. Vyombo vya habari vya Mengi particularly ITV vina nguvu sana-kama angeunga mkono CHADEMA mambo yangekuwa tofauti sana. Lakini ilikuwa kinyume chake.
CHADEMA bado haijaamua mgombea urais wake, kusema kwamba Mengi ni mgombea wa CHADEMA wakati hata sio mwanachama ni kutokututendea haki.
Baadhi mmeunganisha msimamo wa CHADEMA kuhusu pesa za NSSF ama shutuma za ndesamburo na Mengi na uchaga. Huku nako ni kutukosea haki na kuhamisha mjadala wa msingi. CHADEMA tumesimamia mambo mengi ya kitaifa na tunaendelea kuyasimamia. Wakati tunapinga ununuzi wa ndege ya rais sikusikia mtu akisema anayepingwa ni Mramba Mchaga. Wakati tunapinga ununuzi wa RADA haya hayajitokeza. Wakati tunamshambulia Lowasa kuhusu Richmond sijasikia yoyote hapa akisema kwamba huo ni UKASKAZINI.
Bottomline, hapa kuna watu wanataka kututoa kwenye kujadili masuala ya vyanzo(source issues)- kwenye suala la NSSF/PSPF-suala la msingi ni je, bilioni 83 za michango ya walipakodi ziliwekezwa vizuri au zilizochotwa kutokana na ufisadi? NSSF/PSPF/Manji nk wanawajibu wa kujibu?
Ndesamburo ameweka bayana madai ya rushwa na amesema chanzo ni nini, Mengi na Lowasa. Lowasa ni kiongozi wa umma, hajajitokeza kujibu. Rais amesema serikali haitajibu. Kuna nini hapa kinafichwa? Hili ni suala hapa! Tulijadili na kuhoji
Ya Mengi na Manji tuwaachie wenyewe wameshapelekana mahakamani kwa tuhuma za kukashifiana. Tusiingilie uhuru wa mahakama.
Lakini haya matumizi ya pesa za walipa kodi na tuhuma za rushwa; ni ya kwetu haya, tuyajadili kweli kweli...
CHADEMA si chama cha wachaga: rejea tamko rasmi la chama kuhusu suala hili http://www.chadema.net/tamko/2007/mwanri.php
Kwa hiyo mtanzania yoyote ana haki ya kuwa ndoto ya kugombea urais kupitia CHADEMA 2010: awe msukuma, awe mhaya, awe mchaga, awe mjita:wote karibuni ili mradi tu uendani na misingi ya falsafa ya nguvu ya umma http://www.chadema.net/nyaraka/falsafa.php na itikadi ya mrengo wa kati http://www.chadema.net/nyaraka/itikadi.php
JJ
Hawa jamaa hata wakiburizwa mahamani haitoshi, hizo hela wanazoiba ni nyingi mno! Think of 83 billion shs, in other words, USD 83 million sasa jamani hata tunaweza kuwaburuza. Hizo hela labda ziko ulaya tayari. Is real painful. Muhindi anakuja tanzania na dollar 2000 anachonga misheni anatoka na dollar million 80!! Mie sometimes huwa naona hata akina mwamwindi hawakuwa na makosa!! Samahani lakini! Mie siona kama na sisi ni nchi yetu hii! Tuna rais, tuna mawaziri, tuna polisi, na hiki chombo chao PCB (Protection of Corrupt Bureau!) better go to hell!!
WANAJF MIMI NASHANGAA SANA KUONA KUWA WATU KAMA DR. DAU BADO WAKO MADARAKANI:Posting ifuatayo nimeikutauta Darhotwire forums.Ni kuhusu Mengi lakini aliyeiposti huko anaonekana dhahiri kuwa Mujahidina flani jast like huyu "Tafiti Then Jadili"
😕
JIHADIST AGENDA?
Hata mimi haijaniingia vema kichwani. Kazi ipo!Yeye anajiona/anaonekana kijogoo wa ufisadi na HAKUNA WA KUMFANYA KITU na HANA CHA KUPOTEZA mambo yanayompa KIBURI cha kujitokeza. Eti anasema analipa kwa kuwa yeye ni sawa na mnunuzi wa gari ambalo kumbe liliibwa na kupita mikono mingi, lakini hivi jamani FEDHA unaweza kuzifananisha na gari ama mifugo. Maneno hayo ndiyo yaliyosemwa na IGP katika mkutano wake na waandishi. Mwizi wa gari anaenda kuuza, mwizi wa fedha anatumia, sasa fedha jamani ndizo ameuziwa MANJI? Mbona haieleweki?
Kifo, mbona hata tuliiambiwa na kuimbiwa kuwa Dr. Dau is the best next thing to happen in Tanzania na wengine walipiga kampeni kuwa ndiyo anapaswa kuwa Gavana Mpya Benki Kuu? Ina maana tulikuwa tunaghilibiwa?
Labda nimuombe ndugu kifo atuletee Ushahidi au maelezo kuwa Dau Mdini na Mkabila. Lete nafasi zote za NSSF na tuone!!! Mwenzako mmoja alisema Ifakara kumejaa udini kisa BOSI mwislam!!! zilipoletwa posts zote, wakristo ndo walikuwa wengi...
WANAJF MIMI NASHANGAA SANA KUONA KUWA WATU KAMA DR. DAU BADO WAKO MADARAKANI:
1. ANAHUSIKA KUHAKIKISHA MANJI ANAKOPESHWA BILA MASHARTI 9B
2. ANAHAKIKISHA MANJI ANAUZA MRADI WA 9B KWA 39B KWA NSSF
3. ANAHAKIKISHA MADARAKA NDANI YA NSSF YANAENDA KWA UDINI
4. ANAWAPUMBAZA WAANDISHI WA MAGAZETI YA TANZANIA KWA KUWAANDALIA MASHINDANO YASIYO NA TIJA KILA MWAKA ILI WASAHAU KUANDIKA HABARI ZA NSSF
5. NI MUHUBIRI MZURI WA DINI NSSF
6. ANAJARIBU KUINGIZA MAMBO YA CHAMA KTK NSSF KWA KUMUUNDIA MBOWE DENI LISILOLIPIKA
7. ANA UKABILA WA DHAHIRI
8. HASHAURIKI NA HILI LIMEKUWA TATIZO NSSF KWA MUDA WOTE WA MADARAKA YAKE
9. ANAHUSIKA KTK KUIMPLEMENT SYSTEM ISIYOISHA YA ORACLE
10. BAYA ZAIDI NI LAST WEEK TU AMEHAMISHA OFISI ZA NSSF KUTOKA BI. TITI ROAD (CHEAPER AREA) KWENDA JENGO JIPYA (AZIKIWE) ILI TU AWE ANAKAA FLOOR YA 17 NA KUWA CEO ANAYEKAA OFISI ZA JUU ZAIDI TZ. JENGO HILO LA AZIKIWE LINGEWEZA KUIINGIZI NSSF HELA NYINGI ZAIDI YA JENGO LA BI. TITI-NADHANI HAFAI
NAWAKILISHA