DOKEZO Meneja wa NHIF Dodoma na Watumishi waliokiri kuiba fedha hawajachukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

independentiabien

New Member
Jan 28, 2023
1
8
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri wa Afya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Mwaka 2022 zililipotiwa taarifa za Wizi wa fedha za Umma zilizosganywa na Meneja wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Watumishi wa Mkoa huo kufanya ubadhirifu wa fedha za Umma kupitia safari hewa za kikazi. Wizi huu ulifanywa kwa miaka mine kuanzia 2018 hadi 2022.

Taarifa hii iliwasilishwa TAKUKURU na Taasisi hii ikafanya uchunguzi. Meneja wa Mkoa pamoja na Watumishi hao walikiri kulipwa fedha wakiwa Ofisini kila mmoja akilipwa wastani wa Tshs 1,000,000 kila mwezi. Watumishi hao ni;

Bw. Stephen Shauritanga (Meneja wa Mkoa Dodoma)
Linus Kaana (Afisa Uanachama)
Sunday Matoi (Afisa Uanachama)
Emmanuel Magese (Mhasibu Mwandamizi)
Zuena Hassan (Afisa Uanachama)
Ashiel Faustine Afisa (Uanachama)

Hivyo, Meneja wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Watumishi hawa kila mwaka kila Mtumishi analipwa malipo hewa ya Tshs. 12,000,000 kwa kazi za nje za Ofisi za kutafuta Wanachama na lakini hawasafiri bali wanabaki Ofisini. Baada ya Watumishi hawa kuhojiwa na TAKUKURU walikiri kupokea fedha hizo na hiyo Taasisi ilithibitisha kwamnba WIZI huu ulikuwa unafanyika.

Kutokana na uchunguzi huu, Murugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Ndg. Bernard Konga na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Ndg. Lameck Kabeho wana taarifa ya WIZU huu. Kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma Kifungu cha 42 (1) Aya ya 1,2,8 na 13, kwa kutumia ushahidi wa TAKUKURU watumishi hawa walipaswa kupewa Notisi pamoja na Hati za mashitaka kutokana na WIZI huu. Kitendo cha kutowachukulia HATUA ZA KINIDHAMU NA KISHERIA licha ya KUIBA, KUIABISHA SERIKALI KWA UMMA NA KUSHINDWA KUFANYA KAZI KWA KIWANGO KINACHORIDHISHA kinadhihirisha kwamba Watumishi hawa wanalindwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya pamoja na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Utumishi wa Umma ya 2002, Kanuni za Utumishi wa Umma za 2003 na Kanuni za Utumishi wa Umma za 2022. Aidha kutowachukulia hatua ni kinyume na Maadili ya Viongozi wa Umma.

Naomba kuwasilisha ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi ya Watumishi hawa wasio waaminifu.
 
Angekuwepo Mzilankende Mnyago Chap, Watu Wanazoa Pesa Za Mfuko Unadoda Dawa Hakuna, Vipimo Ubabaishaji
 
Na huo ni mkoa mmoja tu ambao mambo yapo hadharani jumlisha mikoa mingine ambayo huenda pia ina ubadhirifu.. huo mfuko unapoteza shillingi ngapi?
 
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri wa Afya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Mwaka 2022 zililipotiwa taarifa za Wizi wa fedha za Umma zilizosganywa na Meneja wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Watumishi wa Mkoa huo kufanya ubadhirifu wa fedha za Umma kupitia safari hewa za kikazi. Wizi huu ulifanywa kwa miaka mine kuanzia 2018 hadi 2022.

Taarifa hii iliwasilishwa TAKUKURU na Taasisi hii ikafanya uchunguzi. Meneja wa Mkoa pamoja na Watumishi hao walikiri kulipwa fedha wakiwa Ofisini kila mmoja akilipwa wastani wa Tshs 1,000,000 kila mwezi. Watumishi hao ni;

Bw. Stephen Shauritanga (Meneja wa Mkoa Dodoma)
Linus Kaana (Afisa Uanachama)
Sunday Matoi (Afisa Uanachama)
Emmanuel Magese (Mhasibu Mwandamizi)
Zuena Hassan (Afisa Uanachama)
Ashiel Faustine Afisa (Uanachama)

Hivyo, Meneja wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Watumishi hawa kila mwaka kila Mtumishi analipwa malipo hewa ya Tshs. 12,000,000 kwa kazi za nje za Ofisi za kutafuta Wanachama na lakini hawasafiri bali wanabaki Ofisini. Baada ya Watumishi hawa kuhojiwa na TAKUKURU walikiri kupokea fedha hizo na hiyo Taasisi ilithibitisha kwamnba WIZI huu ulikuwa unafanyika.

Kutokana na uchunguzi huu, Murugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Ndg. Bernard Konga na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Ndg. Lameck Kabeho wana taarifa ya WIZU huu. Kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma Kifungu cha 42 (1) Aya ya 1,2,8 na 13, kwa kutumia ushahidi wa TAKUKURU watumishi hawa walipaswa kupewa Notisi pamoja na Hati za mashitaka kutokana na WIZI huu. Kitendo cha kutowachukulia HATUA ZA KINIDHAMU NA KISHERIA licha ya KUIBA, KUIABISHA SERIKALI KWA UMMA NA KUSHINDWA KUFANYA KAZI KWA KIWANGO KINACHORIDHISHA kinadhihirisha kwamba Watumishi hawa wanalindwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya pamoja na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Utumishi wa Umma ya 2002, Kanuni za Utumishi wa Umma za 2003 na Kanuni za Utumishi wa Umma za 2022. Aidha kutowachukulia hatua ni kinyume na Maadili ya Viongozi wa Umma.

Naomba kuwasilisha ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi ya Watumishi hawa wasio waaminifu.
Ulinzi shirikishi ndio huu. Ufanyieni kazi.

Polisi, TAKUKURU, serikali, mnapenda kusema tutoe ushirikiano. Ukimjua gaidi, mwizi wa TV, jambazi wa kuvunja mtaani watajie polisi wakambebe ghetoni kwake.

Lakini Kwenye ma ujambazi ya kiuchumi kama haya wakitajiwa wanauchuna!

Hivi raia asiyelipwa mshahara wa serikali anakuwaje mzalendo kuliko Waziri wa Afya, IGP, Waziri Mkuu, RPC, Rais, Mkuu wa Usalama, CEO NHIF, Mkuu wa TAKUKURU tunaowapisha barabarani kwenye ma Land Cruiser wanayopanda bure ??????
 
Watakua wamejiridhisha kuwa ni majungu kazini kwahiyo wametupilia mbali.
 
Back
Top Bottom