NHIF: Mfumo wa uwasilishaji wa kadi kwa watumishi kupitia halmashauri ndio changamoto

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Meneja wa mfuko wa bima ya afya ya NHIF Mkoani Tabora, Salum Adam amesema NHIF haina changamoto ya uchelewashaji wa vitambulisho isipokua kuna changamoto ya kimazingira na mfumo wa uwasilishaji wa kadi kwa watumishi kupitia halmashauri.

Akizungumza na waandishi wa habari meneja wa NHIF amesema mchakato wa kuwafikishia kadi wanachama watumishi wa serikali umekua ukifanywa kupitia halmashauri zao kwahiyo muda wa kupata kadi unategemea umbali wa mwanachama na jografia ya halmashauri yake.

Salum amesema mtumishi akijaza fomu ya bima kwanza inapelekwa halmshauri kisha halmashauri inapeleka fomu NHIF na baada ya mchakato wa kadi NHIF hurudisha tena halmashauri mchakato ambao unaweza kuchelewesha kadi kufika kwa mwanachama aliye katika mazingira ya mbali.

Pia soma > DOKEZO - Tabia ya NHIF Tabora kuchelewesha kadi za Bima za Uanachama inatuumiza wengi
 
Back
Top Bottom