Mbunge Fatma Taufiq: Nataka Kufahamu Tamko la Serikali kwa Waajiri Wanaowanyima Safari Watumishi Wanaonyonyesha kwa Kigezo cha Kutumia Fedha Nyingi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
Serikali imewataka Waajiri wote katika utumishi wa umma kuwahudumia Watumishi wote kwa usawa na haki wakiwemo wale wanaonyonyesha kupewa safari na kulipwa posho ya safari bila ya kubaguliwa.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete ameyasema hayo Bungeni Dodoma wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge Fatma Taufiq aliyetaka kufahamu tamko la Serikali kwa Waajiri wanaowanyima safari Watumishi wanaonyonyesha kwa kigezo cha kutumia fedha nyingi kujikimu.

Amesema sera ya Menejimenti na ajira katika utumishi wa umma ya 2008 pamoja na kanuni za kudumu za utumishi wa umma zinaelekeza kuwa watumishi wanaosafiri kikazi wakiwemo wanaonyonyesha wanapaswa kupewa posho ya kujikimu.

photo_2022-03-14_14-37-40.jpg
 
Back
Top Bottom