Nijapolazimika kusimama mwenyewe, bado mimi nitatetea Tanzania iendelee kuwepo kwenye EAC. Tofauti ndogo tunazoziona sasa naamini zinatatulika na mchakato wa EAC ukaendelea mbele. Bado naamini shirikisho linaweza kuwepo bila kuathiri interests na rasilimali za Tanzania. Najua yapo mambo machache tunatakiwa tusacrifice kama tunataka kufaidika na EAC, huwezi kukumbatia maji kama jiwe.
Mkuu
Tuko madhumuni na matarajio ya Tanzania kutaka kuwepo kwenye EAC bado yako ndani ya hoja yako na hayajabadirika. Tanzania haijadandia gari la EAC bali ililitengeneza yenyewe na kuanza kuliendesha na kutokana na hivyo, inafahamu vizuri spare part zake, strength and weakness ya gari na hata njia na sehemu linakoelekea.
Kinachotokea kwa sasa ni baadhi ya abiria kuanza kugombania usukani ili waendeshe kwa kudhania wanafahamu kuliendesha na pia wanafahamu njia ya mkato kufika mwisho wa safari. Tanzania imeamua kukaa kando kuwaacha waliendeshe na kama itaona kuna hatari zaidi ya kupinduka basi haitakuwa na option zaidi ya kushuka na kuwaacha waendelee na safari. Hata kama wakitaka kuishusha kwa nguvu, basi haita hesitate kushuka.
Kuna wazee mpaka sasa ambao walikuwa watumishi wa iliyokuwa EAC hawajalipwa mafao yao baadaya kusarambatika hiyo jumuiya. Tutakuwa wajinga sana kama nchi tukianza kurudia makosa yaleyale yaliyosababisha kuvunjia kwa EAC. Kuna somo hapa linalohitaji kueleweka na Tanzania inaonekana kulielewa vizuri sana. Hakuna faida yoyote ya kuunda bora EAC kwa kuvidhiana badala EAC bora kwa sababu tulishajaribu kuunda bora EAC na tukashindwa.
Kinachonisikitisha ni pale viongozi wetu wanaposhabikia tofauti hizi ndogo bila kujua kuwa kuna leo na kesho. Kiongozi kama waziri huwezi sema "tunasubiri talaka"!!!. That is an arrogant type of speech isiyotakiwa kutolewa na mtu mwenye akili. Niliipenda zaidi taarifa iliyotolewa na wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki juzi (pamoja na mapungufu yake), kuliko huu utumbo uliojaa majivuno alioongea Membe. Unapokuwa waziri wa mambo ya nje, ina maana wewe ndiye afisa mahusiano wa nchi, na tunatarajia uwe diplomat mkuu wa nchi.
Ninashindwa kukuelewa unaposema tofauti 'ndogondogo' kana kwamba hazina impact kubwa kwa ustawi wa EAC.
Kauli kama hii ya Mh. Membe kwa mtu mwenye mtazamo mpana atagundua kuwa tatizo lililopo ni kubwa zaidi ya kinachoonekana nje na kwenye media.
Tanzania ina history ya kuwa reserved linapokuja swala la mahusiano ya kimataifa na pale Tanzania ikiamua kuongea kwa sauti ya juu basi lazima kuna kitu kikubwa ambacho hakiko sawa. Hii hupelekea nchi zingine kusikiliza kwa sababu kauli ya Tanzania huwa ina ujumbe mzito.
Maneno ya Mh. Membe yamebeba ujumbe mzito ingawa kuna watu hawayachunguzi na kulinganisha na historia ya Tanzania katika majukwaa ya kimataifa.
Neno "kusubiri taraka" unaweza kusema ni "arrogant type of speech" lakini halikutoka kwa bahati mbaya bali limetoka na ujumbe mzito kwa wadau wa EAC.
Huwezi kusema alichokisema Mh. Membe ni majivuno na ukaacha kuangalia kinachofanywa na watawala wa nchi za Kenya, Rwanda na Uganda. Hakuna majivuno zaidi ya haya ya kuwa na informal meeting inayobadirika na kuwa formal meeting bila taratibu na sheria zilizowekwa kusimamia njia kama hiyo, na kibaya zaidi ni kutowaarika hata wadau wengine ambao wataathirika kwa njia moja au nyingine na huo mkutano unaoitwa "informal meeting".
Kati ya mara 100 wanazohukumiwa watu kwa kuongea/kutokuongea, bila shaka mara 99 watu wanahukumiwa kwa kuongea wrong, na pengine mara moja wanahukumiwa kwa kutokuongea right. Membe alitakiwa achuje sana sentensi zake, hasa wakati huu wa tension na hao majirani zetu.
cc
Candid Scope
Kongosho
MkamaP
Mdondoaji
Ng'wamapalala timbilimu
Mh. Membe amechunga sana kwa muda mrefu emotion na opinions za Tanzania kama ilivyo kawaida ya Tanzania katika majukwaa ya kimataifa. Sentensi alizozitoa bila kumung'unya maneno ni nzito kama ilivyotakiwa ziwafikie walengwa ili iwe rahisi kwao kutambua msimamo wa Tanzania katika sakata hili na kuwarahisishia kufikia "easy decision".