Membe: Tunasubiri talaka Jumuiya Afrika Mashariki

Membe: Tunasubiri talaka Jumuiya Afrika Mashariki

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema nchi za Rwanda, Kenya, Burundi na Uganda hazina haja ya kuanzisha shirikisho lao la siri kwani Tanzania itakapofikia hatua ya kutaka kujiondoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), suala hilo litapelekwa Bungeni ili lijadiliwe na wabunge wataliridhia.

Akihojiwa jana asubuhi na Cloud Radio, Membe alisema kuwa nchi hizo hazina sababu ya kufanya mambo kwa siri kwani kama wameshindwa na ni vema kuieleza Tanzania. “Kama ni talaka moja watupe tu. Sisi tunasubiri kupewa talaka.”

Afafanua msimamo wa Tanzania baada ya nchi hizo kuonekana zikifanya jitihada za kuanzisha shirikisho lao na kuitenga Tanzania, Membe alisema nchi hizo ziwe wazi na wakweli kama zinaona kuna jambo ambalo hazilidhiki nalo ambalo Tanzania inalifanya na busara itumike kulizungumza kwenye mikutano badala ya hivi sasa zinapoamua kuanzisha muungano wao wa siri.

“Tutakapoamua ku-suspend relationship (kusimamisha uhusiano) na Afrika Mashariki, tutakapoamua kujiondoa kwenye utaratibu huu wa shirikisho la haraka haraka, tutapeleka suala hili bungeni. Bunge litajadili na nina uhakika wabunge wataangalia busara ya kutokuharakisha wala kudhulumiwa wala kuburuzwa, tutawaacha waendelee kwa raha mustarehe, ila sisi tunachoomba tu wawe wakweli, wawe wawazi si kutengeneza muungano wa siri siri,” alisema.

Alipoulizwa kama hali hii inachangiwa na nini hasa, kama ni kutokana na msuguano baina ya Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Rwanda Paul Kageme, wa hivi karibuni au ni msukumu wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kutaka kutimiza azma yake ya kuwa rais wa kwanza wa Shrikisho hilo, Membe alisema yanawezekana.

Hata hivyo, alifafanua kuwa kuna mambo kadhaa yanachangia, moja, ni msimamo wa Tanzania kukataa suala la ardhi kuingizwa katika mambo ya Jumuiya na kwamba ni jambo ambalo serikali haiwezi kukubali hasa ikizingatia kuwa ardhi ndiyo dhahabu ya nchi.

Alisema jambo la pili linalolalamikiwa na nchi hizo ni hatua ya Tanzania kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) na Katibu Mkuu wa Sadc kuwa ni Mtanzania. “Hivyo wanaona Tanzania damu yao ipo Sadc, kitu ambacho ni kweli, lakini hata hivyo, nao wasilalamike kwa sababu wapo IGAD na Comesa.”

Aliongeza kuwa jambo jingine linalolalamikiwa ni hatua ya Tanzania kupeleka majeshi yake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kuwapa kipigo kizuri kikundi cha waasi cha M23 kati ya Agosti 26 na 28 mwaka huu hatua ambayo nchi hizo zinakiona ni kama kudhoofisha Muungano wa Afrika Mashariki.

Kuhusu jinsi gani kitendo cha kuwapiga M23 kinavyodhoofisha muungano alisema: “Kwa sababu wale M23 Tanzania inakwenda kwa principle (misingi) inayosema tunapoona nchi ya Afrika Mashariki au ya Sadc inakwenda kinyume cha matakwa ya wananchi au haifuati kanuni za uongozi bora, sisi huwa tunaingilia, siyo maana kwamba tunavunja Jumuiya Afrika Mashariki.”

Membe alisema nchi za Rwanda, Uganda, Kenya na Burundi baada ya kuona Tanzania haitaki suala la ardhi kuingiza EAC, na bado ni wanachama wa Sadc na kwamba haitaki kuanzisha Shirikisho la Afrika Mashariki haraka haraka na baadhi ya viongozi wa dunia kufanya ziara Tanzania, waliamua kuanzisha shirikisho lao la siri.

Viongozi wakuu duniani waliotembelea Tanzania mwaka huu pekee ni Rais wa China, Xi Jinping, na Rais wa Marekani Barack Obama..

Alisema nchi hizo zilipaswa kutumia utaratibu kama kuna mambo yanawakera ambayo Tanzania inayafanya ukiwamo.

Hatua hizo ni pamoja na kuiita Tanzania kuzungumza kwani msimamo wa serikali ni kwamba haiwezi kuburuzwa kuingia katika Shirikisho la Afrika Mashariki.

“Msimamo wetu hatuwezi kugawa ardhi yetu, hatuwezi kuwa waangaliaji, hivyo vingezo vyote wanataka tuvitake,’ alisema na kuongeza:

“Wala wasingepata shida yote hii, tungekutana kwenye kikao tukatoa kibali wakaendelea na utaratibu na sisi tukarudi tukaendelee na utaratibu wetu wa mwendo wa pole.”

Membe alisema katika kufikiwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki kuna hatua kadhaa za kufuata, moja ni soko la pamoja, ushuru wa forodha, sarafu moja na mwisho shirikisho la kisiasa.

“Hadi sasa bado tunahangaika na hatua hizi za awali, hatujaweza hata kufikia sarafu moja, sasa wenzetu wanataka shirikisho la kisiasa,” alisema Membe na kuongeza:“Mimi sioni hata hiyo monitory union (sarafu moja) ikifikiwa sasa hivi. Sisi bado tunaikataa.”

Alifafanua kuwa hata Waingereza wakati Umoja wa Ulaya wanakiunga kwenye sarafu ya Euro wao walibaki na sarafu yao, na mpaka sasa wanaendelea nayo. Hivi karibuni Tanzania imeonekana kuwekwa kando na nchi nyingine nne kati ya tano zinazounda EAC.

Tayari marais wa nchi hizo, Kagame, Museveni, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Pierre Nkurunzinza wa Burundi wamekwisha kufikia makubaliano ya kuanzisha mchakato wa kuandikwa kwa Rasimu ya Katiba ya Shirikisho la Kisiasa la nchi wanachama wa EAC, bila kuishirikisha Tanzania.

Waziri wa Serikali za Mitaa wa Rwanda, James Musoni, amekaririwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo akieleza kuwa makubaliano ya kuanzishwa kwa mchakato wa kuandikwa kwa Rasimu ya Katiba ya Shirikisho la Afrika Mashariki, yalifikiwa Septemba 12 mwaka huu, mjini Kampala na marais wa Rwanda, Kenya na Uganda na hivi karibuni Rais wa Burundi ambaye alialikwa katika mkutano huo na kushindwa kuhudhuria, naye sasa amethibitisha ushirika wake katika shirikisho hilo jipya.

Tayari nchi za Kenya, Uganda na Rwanda zimeshaanzisha mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Kenya hadi Rwanda.

Vile vile Bandari ya Mombasa nchini Kenya imeshafanyiwa upanuzi kuruhusu nchi za Uganda na Rwanda kupitisha mizigo yao.

Kufuatia hali hiyo ,Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, hivi karibuni alisema licha ya hatua zinazochukuliwa na nchi wanachama wa EAC za kuitenga Tanzania katika baadhi ya mambo, itabakia na msimamo wake na haitakubaliana kuingia kwenye Shirikisho la Kisiasa huku masuala ya ushuru wa forodha, soko la pamoja na sarafu moja, hayajatengamaa.

Waziri Sitta pia alieleza kuwa Tanzania imeiandikia barua sekretarieti ya baraza la mawaziri wa nchi wanachama wa EAC, ikilalamikia baadhi ya mambo yanayoendeshwa kwa usiri na baadhi ya nchi wanachama.

Kikao kingine cha viongozi wa nchi hizo kinatarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu jijini Kigali, Rwanda bila kuishirikisha Tanzania.
 

Attachments

  • Membe.JPG
    Membe.JPG
    134.3 KB · Views: 1,054
Huyu Membe sijui alipewa huo uwaziri wa Mambo ya nje kwa kigezo gani. Naona ametumia stori za kuunga unga mtaani na kuishia kupmba talaka. Kama waziri wa mambo ya nje analalamika ina maana ana rais wake pia analalamika. Sa itabidi na sisi wananchi tuendelee kulalamika kwani watu wa kutusemea wanalalamika.
 
Hawa akina Museveni, Kagame na Kenyata baada ya kupima kina cha maji ya Kikwete na kukuta yana kina ambacho hawawezi wala kuthubutu kuogelea, wamejikuta ndani ya minority group kwa siku zijazo, hivyo kuamua kivyao kujaribu kutafuta njia mbadala kujinusuru.

Jambo moja la Msingi ambalo Kikwete atakumbukwa siku za usoni ni hili la kuitangaza Tanzania kwa mataifa, Tanzania ya leo si ile ya siku za nyuma iliyotumiwa na Kenya vivutio vyake kutumika kupitishia watalii Kenya.

Binafsi naona tu njia walizotumia ni utashi wa viongozi wa juu wa nchi na wala si matakwa ya wananchi wao, hivyo mambo ya uchumi wa dunia ya leo unabaki kuwa huru na katu huwezi Kikwete hawezi niwekea mipaka mie kupitishia mizigo yangu bandari ya Beira - Msumbiji au kwengineko ndivyo yatakayowapata hawa viongozi wa utatu.

Tanzania inahitaji tu kuboresha njia za usafirishaji na hivyo ukaribu wa bandari ya Tanzania kwa nchi za Rwanda na Burundi una nafasi bado. Uganda nao wako katikati, lakini kuna kilichowavutia wakati ule kupitishia mizigo yao bandari ya Dar sijui kama sababu zimetoweka kwa hoja zipi.

Tishio la ugaidi la Wasomali lisipothibitiwa kutosha ni kitu kinachoweza kusitisha mipango ya kutumia bandari ya Mombasa.
 
Amezungumza jambo zito kwa lugha nyepesi. Amefanya vizuri sana maana angetumia ile lugha ya utawala na mamlaka ingeleta mhemuko na wasiwasi kwa nchi jirani hata baadhi ya wananchi. Lakini kama watz tumeelewa vizuri sana nchi yetu inavyolichukulia hili jambo. Bravo mko kwenye mstari sahihi....wakati ukifika tutaondoka tu.
 
Wakenya, Waganda na Warwanda ni waroho sana wa ardhi yetu. Na pia si watu wa kuwachekeachekea kabisa kwani ni hawana utu hata kidogo. Tukizubaa na kukubaliana na matakwa yao tutaishia kuwa watumwa ndani ya nchi yetu. Let them go, hatuna cha kupoteza na wala hatuwahitaji.
 
Akihojiwa jana asubuhi na Cloud Radio, Membe alisema kuwa nchi hizo hazina sababu ya kufanya mambo kwa siri kwani kama wameshindwa na ni vema kuieleza Tanzania. "Kama ni talaka moja watupe tu. Sisi tunasubiri kupewa talaka."
Tunapojadili mambo yanayohusu hatima ya nchi ha hasa mtu kama waziri inatupasa kuwa serious. Naanza kuamini kuwa hawa jamaa ni ndugu!
 
Membe yuko safi sana, hafichifichi mambo. Kwa muono wangu kaweka msimamo swafi. Kupewa talaka, si lazima uwe umeolewa na hata aliyeoa anapewa talaka. Kawaida anayetoa talaka ni yule anayeona kutoridhishwa na mwenzie.
 
Hizi ni kauli za viongozi wasiojua cha kufanya "eti tunaendelea na mwendo wetu wa pole"! Nonsense!
Mimi walichonifurahisha hawa marais ni kwamba hawakutaja neno Tanzania wakati wameanza hii mikakati yao. Viongozi wetu na baadhi hata humu ndiyo mnaojigonga kutaja hiki au kile. Waendelee kama sisi tulivyoendelea kuichagua Zanzibar kuungana nayo na tukaacha mikakati ya kuunganisha EA yote. Viva Museveni, Kagame na Kenyatta. Mtu anayechelewesha jambo lako achana naye na usimtaje unapoachana naye. Watanzania tuendelee kulumbana kama kawaida yetu.
 
Kuna watu hapa wanaipinga kauli ya Mh. Membe lakini hawatoi political, economic and social alternative.

Waziri Membe yuko sawa na uamuzi wa serikali unapaswa kupongezwa. Serikali "dhaifu" imesimama kidede kutetea maslahi ya Taifa. Tanzania haiathiriki chochote katika mikutano ya hawa Marais na ndiyo maana serikali inawaangalia tu ikisubiri watoe maamuzi mazito na siyo haya mepesi ya kujificha ficha.

Kwanza hili shirikisho kwa kiwango kikubwa liko based na matakwa ya marais badala ya wananchi kupitia taasisi zake kama bunge au direct representative (referendum).

Think about EAC after Pres. Museveni and Pres. Kagame ikichukuliwa kuwa hata misingi ya kidemokrasia katika nchi zao haiko imara achilia mbali kuwepo kwa makundi based on tribe and political debarment.

Siwezi hata kuongea juu ya Pres. Kenyatta kwa sababu anasumbuliwa na naively.

The entire episode is a talking shop.
 
Wakenya, Waganda na Warwanda ni waroho sana wa ardhi yetu. Na pia si watu wa kuwachekeachekea kabisa kwani ni hawana utu hata kidogo. Tukizubaa na kukubaliana na matakwa yao tutaishia kuwa watumwa ndani ya nchi yetu. Let them go, hatuna cha kupoteza na wala hatuwahitaji.

Hilo neno ndilo ninalolifikiria pia mdau mwenzangu, tusikubali utumwa katika nchi yetu wenyewe. Tuna mengi tu ya kujivunia, ulimwengu uko wazi mbele yetu, uchumi wetu hautegemei hao wa utatu, dunia nzima imetufungulia milango, hao wa utatu watakuja kutetereka soon maana walichokifanya ni ndoa ya mkeka isiyo na mizizi ya kutosha, sawa na zile mbegu za mpanzi zilizoangukia kwenye miamba ziliota kisha zikanyauka kwa sababu ya kukosa kupenyeza mizizi miambani.
 
Nimekuelewa sana Membe kwa kucheza na psycology ya hawa wahuni na sitashangaa baada ya kikao chao cha siri huko Kigari mwezi ujao sie huku tukaanda bunge letu kikao kijacho kupitisha azimio la nchi kujitoa rasim eac
 
Binafsi,

Namuunga mkono Membe kwa msimamo wake wa huu kama ni kweli na kama msimamo wa Serikali. Kama wanavyosema wachangiaji wengine Tanzania haina shida sana na EAC waendelee na mipango yao na sisi tunaendelea na mipango yetu. Mambo ya kisiasa na kiuchumi ni vitu viwili tofauti. Mfanyabiashara anaangalia ni wapi anaweza kufaidika na sio serikali imetoa kipaumbele. Ikiwa kama tunaweza kuboresha miundo mbinu yetu, kujenga uchumi ndani na kuboresha bandari zetu To hell with EAC!!!! We can stand on our own.

What I am seeing now ni kwamba hao watatu wanaangalia kiberiti hiki cha Tanzania kimejaa au la. Na ukweli kiberiti cha Tanzania kimejaa na hakitingishiki. Tunamatatizo yetu na dubwana la CCM na baadhi ya mafisadi but ukweli unabakia sote tunaipenda nchi yetu. Na mashirikisho na majumuiya lazima tulinde interest za watanzania kwanza ndio tunaangalie mengineyo. Ninavyoona tuboreshe bandari zetu na tusiishie bandari tatu (Tanga, Bagamoyo na Dar-es-Salaam) tuwe na tisa bandari za kisasa (Tanga, Bagamoyo, Dar-es-Salaam, Kilwa, Mbeya au Ruvuma maeneo ya Mbambabay, Rukwa au Kigoma, na Mwanza au Kagera au Mara). Tuboreshe reli zetu ya kati, kusini na Tazara pamoja na reli ya kaskazini. Tuachane na biashara ya malori inayochangia kwa kiasi kikubwa kuharibu barabara zetu na kuchelewesha mizigo.

Tukishaboresha miundo mbinu, uhakikishaji wa upatikanaji wa umeme na kukuza kiwango cha elimu na viwanda tutaona kama EAC ina umuhimu kwetu au la
 
Back
Top Bottom