Membe: Tunasubiri talaka Jumuiya Afrika Mashariki

Membe: Tunasubiri talaka Jumuiya Afrika Mashariki

Kabisaaaa... na hii ndiyo sababu wenzetu Kenya, Uganda na Rwanda wameona wafanye haraka ili kuistua Tanzania iliyolala usingizi wa pono. Tatizo si kututenga ni uzembe wa Watanzania wanaoanya mambo yao kama kinyonga. Na ati anarudia ataendelea na mwendo wao wa pole!
Diplomasia gani hii ya kitoto. Hatujasikia Kenya, Uganda ama Rwanda wakizungumzia Tanzania katika hili. Kwa nini? Siyo usiri bali unyeti wa suala lenyewe. Ilitarajiwa partner anayelalamika (Tanzania) awasiliane na wenzake na kumaliza jambo hili. Lakini siku hizo zote wako kimya, wanazinduka tu kama mtu akojoaye kitandani na kuanza kutulisha mambo ambayo yametokana na uzembe wao. Wao eti kulalamika kama watoto. Likisemwa hili Kenya, lile Kenya, mara Rwanda aibu gani hii jamani. Kama Kenya ina nguvu kiuchumi, huyu ndiye wa kushika tupate ujuzi na manufaa mengine sisi tulio dhaifu. Mara oh wanataka ardhi yetu! Upuuzi gani huu? Mbona hata hii tunayodai yetu imeshamalizwa na makampuni ya nje au msiyemtaka ni Kenya tu katika kundi hilo la wapora ardhi?
Hebu fikiria upuuzi huu, unaposikia waziri, afisa ama mbunge wa Tanzania analalamika ati Kenya wanatangaza mlima Kilimanjaro uko Kenya. Du! Sisi Tanzania aliyetuzuia kutangaza kwamba mlima huo upo Tanzania ni nani? Tulitangaza Kenya ikatukataza? Aibu! Mmelala fofofo kwa nini wenzenu wasichukue nafasi hiyo?
Ati, wanamtuma Afisa Mawasiliano wa Wizara ya Ushirkiano wa Afrika Mashariki kuzungumzia suala nyeti kama hilo. Kweli hawa ni wati makini kweli?

wewe ni raia wa nchi gani?...maana hueleweki kua ni mtz au mkenya?....nijibu kwanza hilo then nikupe majibu yako
 
Mzalendo wa kweli wa Tanzania anapaswa kuongea kwa uchungu kama ulivyo onesha ktk maandishi haya! Watu ambao kutokana na kushindwa kwao kuongoza wameliingiza Taifa ktk ugomvi na majirani hawastahili pongezi zozote

Waziri mzima eti majirani wanatuchukia kwasababu tumetembelewa na wakubwa wa dunia!! Kwamba hajui wamefuata nini hapa?! Heri Chief Mangungo alikua hakwenda shule kuliko hawa wajinga
 
Mimi sijaona kosa la Membe, angekuwa bosi wake anahojiwa asingeeleza mambo yote hayo.
 
Huyu Membe sijui alipewa huo uwaziri wa Mambo ya nje kwa kigezo gani. Naona ametumia stori za kuunga unga mtaani na kuishia kupmba talaka. Kama waziri wa mambo ya nje analalamika ina maana ana rais wake pia analalamika. Sa itabidi na sisi wananchi tuendelee kulalamika kwani watu wa kutusemea wanalalamika.
Mkuu kwani unafikiria stori za mtaani huwa zinatoka wapi..
 
Tunaogopa kuungana na Waafrika wenzetu eti wanatamani utajiri wetu lakini tumekuwa radhi kuwaachia Wageni (Wazungu,Wachina,Waarabu) watuibie hizi rasilimali zetu kisha wakajenge kwao Ulaya,Asia na Arabuni.Juzi kuna Mchina inasemekana ameonwa na Madini ya TANZANITE.It doesn't make any sense to me!We are so mean and stingy against our fellow Africans but in the mean time we look very generous towards the Foreigners.This is totally absurd and ridiculous!
Bora ao wazungu na wachina wako hapa kwa muda; yes watatuachia mashimo ambayo tutafukia (joke) Hawa majirani wakichukua ardhi yetu ndio ntolee hiyo...hivi unadhani Mzanzibari unaweza kumfukuza bara muungano ukivunjika au Mbara unaweza mrudisha Tnganyika bila vita?...Ndio kitakachotokea tukiuza ardhi yetu kwa hawa majirani...once they are in there is no way out.
 
Umeona eeh...tatizo tumewakaribisha majirani (kwa roho yetu nzuri) wamejua Kiswahili na sasa humu kuna wachangiaji wala si Watanzania ila ni fluent in Kiswahili. Hicho kilikuwa kizazi cha Nyerere sasa Hivi wa Tanzania tumekuwa makini ndio maana wanatoa povu...hakuna ujamaa tena...ardhi ya Tanzania ni kwa watanzania.
wewe ni raia wa nchi gani?...maana hueleweki kua ni mtz au mkenya?....nijibu kwanza hilo then nikupe majibu yako
 
hivi huyu kiongozi ana diplomasia kweli? napata shaka na uongozi wake nadhani ana mapungufu sana ktk uwasilishaji wa hotuba na ujibuji wa maswali kwa jamii. yaan hayana uvumilivu hata chembe.
 
wafike salama hiyo safari yao,wanao mponda membe humu ndani hao ni wakenya waganda wanyarwanda, hata hamtunyimi usingizi.
 
Huyu hafai urais,Suala dogo linamsumbua yeye na 6 ONDOENI NCHI KTK KITU INAITWA EAC

huwezi kuiondoa nchi kirahisi rahisi hvyo.kijiografia TZ ndio nchi yenyewe kabisa ya EA.sasa uiondoe kwanini?pia wale wanafanya mambo nje ya EAC chini ya wizara za mambo ya nje.Halafu ukiitoa TZ utawapa urahisi wa kufanya ujinga wao,acha nao waumize vichwa.
 
Membe umesema ukweli na bado haujaoteshwa kuwa rais wa nchi hii subiri ukioteshwa tutajitoa kimya kimya hadi wao watufate wenyewe na wakija tuwape masharitio yetu
 
Kuna watu hapa wanaipinga kauli ya Mh. Membe lakini hawatoi political, economic and social alternative.

Waziri Membe yuko sawa na uamuzi wa serikali unapaswa kupongezwa. Serikali "dhaifu" imesimama kidede kutetea maslahi ya Taifa. Tanzania haiathiriki chochote katika mikutano ya hawa Marais na ndiyo maana serikali inawaangalia tu ikisubiri watoe maamuzi mazito na siyo haya mepesi ya kujificha ficha.

Kwanza hili shirikisho kwa kiwango kikubwa liko based na matakwa ya marais badala ya wananchi kupitia taasisi zake kama bunge au direct representative (referendum).

Think about EAC after Pres. Museveni and Pres. Kagame ikichukuliwa kuwa hata misingi ya kidemokrasia katika nchi zao haiko imara achilia mbali kuwepo kwa makundi based on tribe and political debarment.

Siwezi hata kuongea juu ya Pres. Kenyatta kwa sababu anasumbuliwa na naively.

The entire episode is a talking shop.

Kwa mara ya kwanza nakubaliana na unalosema.you have a point,wao wenyewe political stability yao haieleweki,wana makundi kibao ya waasi then wanaharakisha shirikisho la kisiasa.
Mbele naona giza tu.
As u said hii ni maamuz ya marais na sio wananchi,kila rais ana lake pale
-museven anataka kutimiza ndoto zake kuwa rais wa kwanza wa shirikisho
-kenyatta ni tamaa ya kibiashara ya bandari
-kagame huyo anapenda vita anataka kuchafua ukanda mzima
Pierre hajielewi anataka nini anaburuzwa tu
 
Tofautisha unity na shirikisho wanalolitaka hawa

Isome article tena. Mwalimu anasononeshwa na hii mipaka tuliyorithi kwa wakoloni na anaona kama kuendeleza humiliation ya mwafrika. Pia anawalaumu viongozi wanopinga muungano , hawa ni wasaliti wanalinda masilahi yao binafsi.
 
Alisononeshwa mwanzoni, lakini baada ya kugundua ukweli alifunga mipaka mwenyewe, uliza nani alimbembeleza kuufungua mpaka na Kenya. Hapo mwalim asitumike kama pretext.
Kama asingeona umhimu wa mipaka ya wakoloni angeuacha tu mpaka wazi, baada ya wajanja kumunyang'au nafikiri alikumbuka logic ya wakoloni.
Tusidanganye hapa, hata kabla ya wakoloni tulikuwa na mipaka tena mipaka ya wkati huo ilikuwa very strictly, na ilikuwa huwezi kuuvuka mpaka, watu msipotoshe. Mfano, Mpaka wa chief Mirambo ama Isike pale Tabora kulikuwa hakuna namna vijana wa mwanamarundi wa Mwanza wangeweza kuuvuka huo mpaka. Na kulikuwa hakuna viza, viza ilikuwa ni vita. Nyie vipi bwana, mkoloni alichofanya ni kuipanua tu mipaka.
 
Back
Top Bottom